Msajili aifutie usajili CCM kwakuwa kiongozi wao aliongoza kuchoma kadi za ACT kinyume na Sheria

Kasegela

Senior Member
Mar 24, 2019
127
261
Inamaana Msajili hakuona jinsi Katibu wa CCM kigoma mjini akivyoongoza zoezi la kuchoma kadi za ACT-Wazalendo?

Hii chuki inayopandikizwa na Msajili anajua hasara yake kwa taifa?

Hivi kama hutaki watu wawe na vyama vya siasa,na kila wanachofanya wewe unadhibiti unataka waanzishe vikundi vya Kigaidi?

Kama hataki vyama ambavyo ndio jukwaa la watu kufikia matarajio yao kwa njia ya amani unataka wafikie matarajio yao jwa njia za vurugu?

Hivi Jaji Mutungi anajua Gharama za Ulinzi wa Nchi yenye vikundi vya Kigaidi?

Bajeti za Wizara tano zinaweza kutumika kudhibiti ghasia visiwani pekee kama Lengo la Msajili la kupachafua litafanikiwa.

Mutungi akemewe na kila mpenda amani,wanaktuma Mutungi hawaipendi nchi yetu.

Maandamano Pekee ya Mange Kimambi yaliigharimu serikali fedha nyingi,Watu walianza kuishi kwa posho katika kipindi chote cha kujiweka tayari.

Maalimu Seif kwa sasa ni Taasisi visiwani Zanzibar,watu wenye shiba Zanzibar wanaamini zimeletwa na CCM hata kama Shida zingine zinatokana na uzembe na kutojituma.

Watu wenyeshida ni rahisi kuwaingiza vitani,kwa uadui tuliona na hawa Mabeberu,yakiitwa maandamano halagu ukaua watu mia tu,basi serikali zote zitaanguka.

Mabeberu wataingilia kati kama Mwewe.

Gadafi alikuwa na Fedha kuliko sisi,Gadafi aliwapa kila kitu wananchi wake,Gadafi alijivunia jeshi lake imara lililolipwa vizuri,lkn siku alipolewa madaraka na kuanza kuua watu wake,Mabeberu walimnyakua kama mwewe.

Walipiga kila kiunga cha LIBYA.

Hatimae mabeberu wakatengeneza mazingira kwa wananchi kumuua Gadafi kwa mkono wao.

Tusiwe wajinga,kila nchi inaweza kuchafuka muhimu ni kujiepusha na kika chokochoko,watu wana hasira,Mutungi usituingize kwenye Civil war.

Waache wanasiasa wafanye siasa,atakaeshinda kwa hoja na ushawishi ndie awaongoze wananchi,naevwakimchoka watabadilisha,jambo muhimu mutungi unapaswa kujua ni kuwa Wananchi hawaongozwi kwa mabavu.
 
Kuna kila dalili hivi sasa ccm inakwenda kuanguka. Ukimuanglia Katbu wao Mkuu ktk hotuba zake, ni wazi zimejawa na hasira kejeli na kashfa kwa viongozi mbalimbali waliwemo wa chama chake mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inamaana Msajili hakuona jinsi Katibu wa CCM kigoma mjini akivyoongoza zoezi la kuchoma kadi za ACT-Wazalendo?

Hii chuki inayopandikizwa na Msajili anajua hasara yake kwa taifa?

Hivi kama hutaki watu wawe na vyama vya siasa,na kila wanachofanya wewe unadhibiti unataka waanzishe vikundi vya Kigaidi?

Kama hataki vyama ambavyo ndio jukwaa la watu kufikia matarajio yao kwa njia ya amani unataka wafikie matarajio yao jwa njia za vurugu?

Hivi Jaji Mutungi anajua Gharama za Ulinzi wa Nchi yenye vikundi vya Kigaidi?

Bajeti za Wizara tano zinaweza kutumika kudhibiti ghasia visiwani pekee kama Lengo la Msajili la kupachafua litafanikiwa.

Mutungi akemewe na kila mpenda amani,wanaktuma Mutungi hawaipendi nchi yetu.

Maandamano Pekee ya Mange Kimambi yaliigharimu serikali fedha nyingi,Watu walianza kuishi kwa posho katika kipindi chote cha kujiweka tayari.

Maalimu Seif kwa sasa ni Taasisi visiwani Zanzibar,watu wenye shiba Zanzibar wanaamini zimeletwa na CCM hata kama Shida zingine zinatokana na uzembe na kutojituma.

Watu wenyeshida ni rahisi kuwaingiza vitani,kwa uadui tuliona na hawa Mabeberu,yakiitwa maandamano halagu ukaua watu mia tu,basi serikali zote zitaanguka.

Mabeberu wataingilia kati kama Mwewe.

Gadafi alikuwa na Fedha kuliko sisi,Gadafi aliwapa kila kitu wananchi wake,Gadafi alijivunia jeshi lake imara lililolipwa vizuri,lkn siku alipolewa madaraka na kuanza kuua watu wake,Mabeberu walimnyakua kama mwewe.

Walipiga kila kiunga cha LIBYA.

Hatimae mabeberu wakatengeneza mazingira kwa wananchi kumuua Gadafi kwa mkono wao.

Tusiwe wajinga,kila nchi inaweza kuchafuka muhimu ni kujiepusha na kika chokochoko,watu wana hasira,Mutungi usituingize kwenye Civil war.

Waache wanasiasa wafanye siasa,atakaeshinda kwa hoja na ushawishi ndie awaongoze wananchi,naevwakimchoka watabadilisha,jambo muhimu mutungi unapaswa kujua ni kuwa Wananchi hawaongozwi kwa mabavu.
Tatizo msajili anafanyakazi kwa kupata maelekezo toka CCM na Lipumba.
 
Bora kuwa kondoo lofa mwenye mkia mrefu na mnene wakuficha nduku lake kuliko kuwa mbuzi mjanja mjanja mwenye mkia mfupi wa kulifunua nduku lake km CCM
 
Tatizo kubwa sana Afrika na nchi za ulimwengu wa tatu ni pale madhalimu wanapoishi maisha mazuri na kupata hadhi kubwa na kujiona wana ulinzi mkubwa kabisa.

Dunia ya ulimwengu wa Kwanza walijitahidi sana kuwafanya wenye madaraka na maisha mazuri kupitia umma wawe wastaarabu watenda haki kwa umma unaowalipa kodi ili wapate mishahara minono na maisha mazuri.
Hali hiyo walijenga kwa kuwakataa kabisa watu katili kuwaongoza na kusimamia haki.

Sifa kuu ya Jaji Mbinguni na duniani ni kusimamia haki ambayo hata yeye angependa afanyiwe.
Jaji Mkuu ni Mungu Mwenyewe na ametuelekeza tusiwatendee wengine yale ambayo sisi wenyewe hatungependa tutendewe.

Jaji anayekanyaga jaki za wanyonge wenye shida na njaa ili tu kulinda cheo chake cha kuteuliwa na pia kulinda kundi la watu wachache waloshiba ni dhambii na uovu na chukizo kubwa kwa Mungu aliyewaumba wote ,wenye madaraka na wasio nayo, maskini na matajiri ,wanaCCM na wa vyama Mbadala, Majaji na watuhumiwa.

Jaji Mutungu akijua kuwa hii nchi imeumbwa na Mungu na kila cha asili kilichomo wakiwemo hao makada wa vyama na watawala basi ajiwekee akiba Mbinguni mana kama ni maisha bora amejaliwa kuwa nayo labda anataka kujiwekea akiba kubwa duniani ambapo wezi ,nondo na Kutu vinaharibu.

Nadhani tumekua na tatizo katika nchi nyingi za ulimwengu wa Tatu kuwa na majaji walioupewa ujaji kisiasa Mbadala ya sifa stahiki kama walivyokua akina Nyalali,Kisanga,Samata , Augustino Ramadhani na wengine ambao hata ukisoma hukumu zao unaona kabisa jua la haki likichomoza Afrika.

Mutungu atajenga hisia mbaya sana juu ya haki za kisiasa ambazo Mara nyingi zinaleta vurugu kwenye nchi.
Ni lazima tuheshimu furaha za watu kupitia vyama vyao.

Kuna vyama vinavyohubiri kudhuru watu lakini hatusikii vikikemewa wala kutolewa matamko mana naye ni miongoni mwao. Anafiliri sheria aliyoitunga ni ya kuwabana wapinzani tu huku chama cha mapinduzi kilichopewa dhamana ya kusimamia misingi ya amani na utawala bora kikitoa matamko yasiyojenga umoja na mshikamano wa watanzania.
Nani wa kulaumiwa.

Haki huinua Taifa Bali dhambi(dhulama) ni aibu kwa taifa zima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom