Msaidizi wa Nchimbi ajiengua adai amedhalilishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaidizi wa Nchimbi ajiengua adai amedhalilishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Oct 2, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  Msaidizi wa Nchimbi ajiengua adai amedhalilishwa
  Na Musa Juma, Tarime

  JINAMIZI la tuhuma za ufisadi alizoibua mjumbe wa Halmasharui Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Nape Nnauye ndani ya Umoja wa Vijana (UVCCM) linazidi kuitafuna jumuiya hiyo baada ya aliyekuwa katibu wake mkoa wa Tanga, Mwita Waitara, kutangaza kujiuzulu uongozi.


  Waitara aliwaambia waandishi wa habari jana kwenye hoteli ya G-five mjini hapa kuwa hatua hiyo imelenga kupinga uamuzi wa mwenyekiti wa UV-CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi kumhamishia makao makuu ya jumuiya hiyo kuwa karani wake.


  Alisema uhamisho huo sio wa heri bali unalenga kumdhalilisha kutokana na kupinga agizo la uongozi wa jumuiya hiyo makao makuu lililomtaka awaombe radhi watuhumiwa wa ufisadi baada ya kamati ya utekelezaji ya UVCCM mkoa wa Tanga kutoa tamko la kutaka wawajibishwe.


  “Nchimbi anataka kunidhalilisha kutokana na msimamo wangu wa kupinga mafisadi na kumuunga mkono Nape Nnauye na sitarudi nyuma na sitaenda makao makuu Dar es Salaam UV-CCM labda nikiwa nimekufa,” aliapa Waitara.


  Waitara alieleza kuwa ameamua kukataa kuomba kuwaomba radhi watuhumiwa hao wa ufisadi kwa kuwa anaamini tamko lililotolewa na kamati hiyo lilikuwa halali na sio batili.


  "Kama tamko hilo lilikuwa baya waliopaswa kuomba radhi ni kamati ya utekelezaji mkoa na mimi," alieleza na kubainisha:


  "Wakati mimi wananifanyia haya, mwenyekiti wa UV-CCM mkoa wa Tanga ambaye pia ni katibu mwenezi wa mkoa, Emmanuel Kiondo, ambaye hata katika kikao cha Baraza Kuu la Taifa alimuunga mkono Nape, wameshindwa kumgusa."


  Waitara alitaja sababu nyingine za kukataa kwenda kuwa karani wa Dk. Nchimbi ni nafasi hiyo kutokuwa ya kikatiba na kwamba elimu yake ni kubwa kuliko makatibu wengi wa jumuiya hiyo.


  "Mimi ni msomi na nina shahada. Makatibu wenye elimu ya aina hiyo ndani ya UVCCM ni wawili, siwezi kwenda kuwa karani lakini pia nafasi hiyo haipo kikatiba," alieleza.


  Alisema aliamua kujiunga na UV-CCM mara baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Dar es Saalam na kutunukiwa shahada ya Ualimu wa Sayansi ili kujiendeleza kisiasa na si kwenda kuwa karani.


  Alidai kuwa kitendo cha kuitwa makao makuu ya UV-CCM ni hila ya Dk. Nchimbi kutaka kumfukuza kwa aibu kwenye jumuiya hiyo kama alivyofanya kwa Nape Nnauye, ambaye alivuliwa uanachama na Baraza Kuu kwa madai kuwa alisema uongozi wakati alipotuhumu kuwa mkataba wa uwekezaji wa jengo la makao makuu ya UV-CCM haukupitishwa na vikao halali.


  “Hawa wanataka kunifukuza, nimegundua hilo na Dar es Salaam siendi... mimi ni msomi na nina msimamo... elimu yangu na uwezo wangu sio mtu wa kukaa kama karani na kusambaza chai kwenye vikao wakati kuna makatibu lukuki wenye elimu ya kidato cha nne tu na shule ya msingi,” alisema Waitara.


  Waitara, ambaye alikuwa rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (Daruso), anapinga kushushwa cheo akisema wakati wote wa utendaji wake hajawahi kufanya kosa lolote na kuandikiwa barua yoyote ya kuonywa na umoja huo.


  "Baada ya kujiunga na UV-CCM ilikuwa niwe katibu wa mkoa wa Dar es salaam, lakini kutokana na Nchimbi kunipiga vita ndio walinipeleka Tanga. Lakini sikupinga na nilifanya kazi kwa nguvu zangu zote," alisema Waitara.


  Waitara alibainisha kuwa ataendelea kupinga mradi wa Jengo la Umoja wa Vijana na anapinga kamati ya kuchunguza mradi huo tata kuongozwa na Andrew Chenge, ambaye anatajwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada, na mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa umoja huo, Edward Lowassa, ambaye alijiuzulu wadhifa wake wa Waziri Mkuu kutokana na kuhusishwa kwenye kashfa ya utoaji zabuni kwa kampuni ya ufuaji umeme wa dharura ya Richmond.


  Alisema anashangaa hivi sasa, badala ya viongozi wa umoja huo kujitokeza katika kampeni za ubunge hapa Tarime, wanajishughulisha na upangaji wa safu za viongozi kwenye uchaguzi ujao.
   
 2. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu nashukuru kwa bandiko lako.Nafikiri wapiganaji wote wa jf naomba kuwapa pongezi kwa kupandikiza fikra za kimapinduzi naomba tuendelee na moyo huu kuendeleza moto huu ambao unazidi kukolea ndani ya chama tawala.Nina imani kabisa sauti zikizidi kuongezeka hata JK atapata moyo wa kushughulikia masuala mazito yanyogubika nchi yetu.
  Sasa hivi tunamtwisha lawama nyingi wakati sisi wenyewe Bunge letu lilipoanzisha vuguvugu dhidi ya ufisadi kwa kuanzia na Richmond hatukurespond kwa maandamano ya kuunga mkono azimio la bunge.Ukimya wetu, ukawapa moyo mafisadi kuorganise maandamano ya kuwapokea kishujaa watuhumiwa wa ufisadi kama vile Monduli,Bariadi n.k.
  Ukiangalia mtiririko huo,tulitaka mkuu wa nchi afanye nini wakati wananchi hawaelewi wanachokitaka?Lawama hizi hazistahili kuelekezwa kwa Rais bali kwetu sisi tunaojiita Middle Class.Tunashuhudia vurugu zinazoendelea Tarime tumekaa kimya kama hakuna kinachoendelea,badala ya kuandamana na kuppaza sauti mpaka dunia iskie kuwa Demokrasia inanajisiwa kule Tarime.
  Ukimya wetu umejibiwa na wanasiasa waganga njaa akina Mtikila kuziba pengo linazidi kujitokeza kila kukicha.
  Wanaharakati ni wakati wakutafakari nini nafasi yetu kuipa muelekeo jamii yetu badala ya kuwa watazamaji.
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Mkuu Nsaji,

  Huwa ninaheshima sana na michango yako maana imetulia sana, saafi sana na ni changamoto nzito sana kwa jamii.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  CCM yapata uasi Tarime

  2008-10-02 11:04:40
  Na Mashaka Mgeta, Tarime

  Siasa za makundi zinazidi kukitafuna Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa mmoja wa makada wake aliyekuwa akimnadi mgombea wao katika uchaguzi mdogo wa Tarime, Mwita Mwikabe Waitara, amejitokeza hadharani na kutaka wananchi wamchague mgombea yeyote kuwa mbunge wao si lazima atoke CCM.

  Waitara alikuwa mmoja wa wapiga debe wa mgombe a wa CCM katika uchaguzi huo, Christopher Kangoye.

  Waitara aliyeshika nafasi ya tatu katika kura za maoni kuwania nafasi ubunge jimboni hapa (CCM), alisema dalili zinaonyesha kuwepo vitendo vinavyokinzana na matakwa ya wananchi wa Tarime katika kumchagua mgombea wanayemtaka.

  Hata hivyo, wakati akitoa madai hayo, Waitara alisema ofisi ya Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar ubunge jimboni hapa (CCM), alisema dalili zinaonyesha kuwepo vitendo vinavyokinzana na matakwa ya wananchi wa Tarime katika kumchagua mgombea wanayemtaka.

  Hata hivyo, wakati akitoa madai hayo, Waitara alisema ofisi ya Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar.

  imemuandikia barua ya kumbadilisha kazi, ambapo sasa atakuwa Katibu Myeka wa Mwenyekiti wa Taifa, Dk. Emmanuel Nchimbi.


  Alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari jana kuwa watu waachwe huru kufanya maamuzi yao, pasiwepo shinikizo lolote wala matumizi ya nguvu za dola.

  ``Kama watu wanataka kumchagua Kangoye, acha wamchague, kama wanamtaka Charles Mwera wa Chadema, waachwe huru kumchagua kwa maana hayo yatakuwa maamuzi yao yanayopaswa kuheshimiwa,`` aliongeza.

  Kauli ya Waitara imetafsiriwa na baadhi ya watu kama ni miongoni mwa viashiria vya kuzidi kumeguka kwa CCM wilayani Tarime.

  Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani jimboni hapa, kumekuwa na madai ya mgawanyiko ndani ya CCM, unaoyahusisha makundi ya mahasimu wawili wa kisiasa, Kisyeri Chambiri na Christopher Gachuma.

  Chambiri ni mbunge wa zamani wa Tarime akiwa ametumikia jimbo hilo kwa miaka 15 hadi 2005 aliposhindwa na Chacha Wangwe aliyefariki katika ajali ya gari Julai 28, mwaka huu. Gachuma ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

  Mgawanyiko huo uliosababisha baadhi ya viongozi wa CCM katika kata za Bumera, Turwa na Nanyungu kusimishwa nyadhifa zao.

  Waitara alisema wakati askari walipelekwa Tarime kusimamisha mapigano ya koo za Kikurya, kazi hiyo imeachwa na mapigano yanaendelea huku nyumba zikichomwa moto, lakini polisi wameelekeza kusimamia kampeni za uchaguzi.

  ``Lakini kuna nyumba zinachomwa moto huko Bhumera, wao wapo hapa mjini wamegeuka kukamata magari utafikiri ni trafiki,`` alidai.

  Aidha, alidai kuwa baadhi askari hao wanajihusisha na ukamatwaji wa wafanyabiashara, kwa kigezo cha kutaka kuthibitisha uhalali wake (biashara) na ikiwa wanalipa kodi na ushuru unaostahili.


  Alisema inavyoonekana, kampeni za CCM zimeanza kupoteza mwelekeo kutokana na uongozi wa Taifa kuhusika kupanga ratiba ya mikutano na kutoa fursa ya wapigadebe kutoka Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

  Aliwataja baadhi yao kuwa ni maofisa kutoka kitengo cha propaganda, Hiza Tambwe na Shaibu Akwilombe.

  ``Hawa wamepewa nafasi na kuonekana kuwa wazungumzaji wazuri, lakini lazima wajue kuwa siasa za Dar es Salaam ni tofauti na siasa za hapa Tarime,`` alionya.

  Mbali na Tambwe na Akwilombe, wapiga debe wengine waliopo jimboni hapa ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (TLP), Thomas Ngawaiya, ambaye hivi sasa ni kada wa CCM.

  Waitara alitoa mfano kuwa, kabla ya kuja kwa Tambwe na Akwilombe, alikuwa akihutubia mikutano ya kampeni za mgombea ubunge, Kangoye, lakini hivi sasa wamemhamishia katika kata ya Nyandoto.


  ``Hii ina maana mimi sina mchango wala uwezo wa kuzunguka na mgombea ubunge, lakini sasa hata wakiamua kunitoa kwenye kampeni zao itakuwa heri tu,`` alisema.

  Waitara alisema mgombea atakayechaguliwa anapaswa kujua vipaumbele vya Tarime, ikiwemo malalamiko yanayohusiana na mgodi wa dhahabu wa Nyamongo.

  ``Hapa hakuna uwezekano wa kutumia kifo cha Wangwe ili kushinda, huo ni uhalifu wa kisiasa, kuna mambo ambayo wananchi wanayataka, hivyo wanajua ni mgombea yupi anayewafaa,`` alisema.

  Waitara alisema licha ya CCM kupoteza mwelekeo wa kampeni hizo, kinakabiliwa na changamoto ya kujibu hoja zinazohusiana na kashfa ya ufisadi inayowakabili wanachama wake waandamizi.

  ``Huu ufisadi unaziathiri sana kampeni kwa sababu wapigakura wanataka kujua ukweli, hapa chama inabidi kijipange kwa maana masikini ni wengi kuliko matajiri wenye nguvu za maamuzi,`` alisema.


  Wakati huo huo, Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani Tanga, Mwita Mwikabe Waitara, amevuliwa wadhifa huo, na kuteuliwa kuwa Katibu Myeka wa Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya hiyo, Dk. Emmanuel Nchimbi.

  Waitara aliyewahi kutoa maoni ya UVCCM mkoa wa Tanga, kutaka wahusika katika kashfa ya ufisadi wavuliwe nyadhifa zao ndani ya CCM, amekataa kuyatambua mabadiliko hayo, na kusema hawezi kufanya kazi katika ofisi moja na Nchimbi.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Waitara alisema mabadiliko hayo yana ushahidi wa kimazingira, unaolenga kulipiza kisasi kuhusu tamko lao dhidi nya mafisadi, na msimamo wake binafsi wa kumtetea Nape Nnaye katika azma ya kugombea uenyekiti wa UVCCM.

  ``Nimepata barua ya kupelekwa kuwa Katibu Msaidizi (Myeka) wa Mwenyekiti wa Taifa, hii ni kusema sasa nikawe karani wa Dk. Nchimbi, hilo haliwezekani,`` alisema.

  Waitara alisema mabadiliko hayo ni sehemu ya mbinu za muda mrefu zinazofanywa na Dk Nchimbi, kutaka kuwakwamisha kisiasa vijana wenye msimamo kama wake (Waitara) na Nape.

  ``Hata nilipopelekwa Tanga, ilikuwa ni njama hizo hizo, zilizofanikisha akamleta ndugu yake anayeitwa Sixtus Mapunda wanaotoka sehemu moja,`` alidai.

  Kuhusu tamko la wahusika wa ufisadi, Waitara alisema viongozi waandamizi wa CCM (hakuwataja majina) walimtaka awaombe radhi hususan Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.


  ``Sikutekeleza agizo hilo kwa sababu niliamini katika tamko lililopitishwa na vijana wa CCM mkoani Tanga, kupitia vikao vya halali,`` alisema.

  Aliongeza: ``Sasa wanataka nikawe karani wa Dk. Nchimbi, yaani niwe namfungilia mlango akifika ofisini, kumuandalia chai na kupeleka maji kwenye vikao, hilo haliwezekani,`` alisema.

  Alisema kutokana na hali hiyo, hawezi kukanyaga katika ofisi za Makao Makuu wa UVCCM kutumikia wadhifa huo, na mabadiliko yaliyofanywa, yameashiria mwisho wake wa kushiriki kazi za jumuiya hiyo.

  Alisema mabadiliko hayo, yanajenga hisia za kumuweka katika mazingira, yatakayorahisishwa kuundiwa mizengwe ili afukuzwe UVCCM kwa aibu.

  Waitara alisema hoja iliyotolewa na Nape kuhusu ufisadi katika mradi wa ujenzi wa jengo jipya Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar es Salaam, zilikuwa sahihi, ingawa ni chanzo cha kumdhibiti (Nape) kisiasa.

  Alidai kuwa jitihada hizo zinamhusisha pia mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete.

  Kwa mujibu wa Waitara, Ridhiwan amezunguka mikoani, ikiwemo ya Mwanza na Singida, kwa lengo la kuendeleza vita dhidi ya Nape na kumsaidia Beno Malisa ili ashinde katika uchaguzi huo.

  Alidai Malisa ni miongoni mwa watu wanaohusishwa na ukiukwaji wa taratibu katika mradi wa ujenzi wa jengo la UVCCM.

  ``Wakati mkataba ule unaandaliwa, Malisa alikuwa Katibu Msaidizi Mkuu Utumishi mwenye taaluma ya sheria, huyo ndiye wanayemtaka kuwa Mwenyekiti wa UVCCM,`` alidai.

  Pia, Waitara alisisitiza msimamo wake wa kupinga hatua ya uteuzi wa Andrew Chenge, kuwa mmoja wa wajumbe watatu wa kuboresha mkataba wa ujenzi wa jengo jipya la UVCCM.

  Alisema Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (CCM), anakabiliwa na tuhuma za ufisadi wakati Lowassa ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la UVCCM, alijiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu kutokana na kashfa ya Richmond.

  SOURCE: Nipashe
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Oct 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Waitara kwa kusema kweli tupu bila kujali itakavyokuathiri ndani ya chama cha mafisadi. Kwa mara nyingine tena mafisadi (vongozi wakuu) ndani ya chama hicho wanazidi kuthibitisha kwamba CCM ni Chama Cha mafisadi.
   
 6. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Huyu ex Raisi wa DARUSO hana jipya kakosa vyeo alivyovitaka ndo maana!kwa nini wakati kampeni zinaaanza hakusema hayo?hamna kitu wewe MWITA MWIKWABE!uchu wa madaraka ndo unakufanya ulielie!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Hmmm! Pamoja na kuwa ana uchu wa madaraka lakini yote anayosema kuhusu chama cha mafisadi ni ukweli mtupu na Watanzania wengi wakiyasikia watakubaliana naye. Kusema kwamba kutumia kifo cha Wangwe kwa kampeni za uchaguzi ni kukosa mwelekeo ndani ya chama hicho na mengine mengi ya kweli ni uchu wa madaraka!!! Give a break! Siku yeyote ile nitamheshimu mtu mwenye uchu wa madaraka anayesema kweli tupu kuliko wenye uchu wa madaraka ambao ni wanafiki na mafisadi. Ni nani ndani ya Chama cha Mafisadi asiyekuwa na uchu wa madaraka na uroho wa utajiri wa haraka haraka? Kama wangekuwepo basi wangefanya kila wawezalo kukisafisha chama hicho ili kiache kukumbatia wanafiki na mafisadi lakini hakuna juhudi zozote zinazofanywa na 'viongozi' wa juu wa chama hicho. Uongozi umewashinda sasa chama chao kinaelekea kusambaratika taratibu. Kila anayesema kweli ama atafukuzwa ama kushushwa cheo. Kigumu chama cha mafisadi, Kigumu!
   
 8. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Humjui MWITA!Huyo ndo fisadi kabisa anajua aliyoyafanya alivyokuwa Raisi wa DARUSO pale mlimani!hapo anatapatapa tu!lakini kutapatapa kwake at least kunasaidia kukosoa chama chake!ila na yeye ni walewale nakuambia asingehamishwa kutoka Dar kwenda kuwa katibu wa UV-CCM Tanga wala asingemtetea Nape!Na sasa anasema hayo kutokana na hasira ya kurudishwa tena Dar kuwa katibu msaidizi wa Nchimbi
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Waitara bwana kaa macho CCM wako tayari kubakia hata 2 Nchi Nzima ili mradi wawe na mapesa an madaraka .Musoma huwa inamashujaa miaka yote na hasa Tarime na Wazanaki.Ukiondoa wapuuzi wachache kama Wasira na Msekwa anayetoka Mwanza.Waitara umeanza kurudisha heshima ya Mkurya na uendelee kutetea yale wangwe amekuwa akiyaamini .

  Nina funga novena kukuombea maisha marefu na ujasiri zaidi .
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Sina haja ya kumjua mtu anayesema kweli kuhusu chama cha mafisadi ili kuyakubali anayosema ama kuyakataa. Huyo Kikwete na Makamba hawayaoni au hawayajui mabaya yanayotokea ndani ya chama chao? Mbona hatuwasikii kuyakemea? Wako radhi kumshusha cheo au hata kumfukuza yeyote anayesema kweli ndani ya chama hicho ili waendelee kuwakumbatia wanafiki na mafisadi na kuendeleza uovu wao.
   
 11. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #11
  Oct 2, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  NAKUONEA Huruma Mwita Mwikwabe japo kwa upande mwingine nalazimika kukupongeza.Ila nachokusikitikia tu ni kwamba uliingia nyumba usiyoijua ukafanikiwa kupenya hadi karibu na chumbani kabisa,lakini kabla hujagusa kitasa cha chumbani ukarudishwa sebuleni na hatimaye uani.Kuna kajimsemo fulani kanasema "you can not kill the butterflies unless you kno their ways".Sasa huko UVCCM ndio kwenyewe.MWIKWABE kama kweli wewe ni jasiri na upo tayari kucheza muziki wa ccm tunakupa hongera sana ila sasa jiandae na MAKUBWA yanayokuja mbele yako,mbaya zaidi mbaya wako ana majeshi(waziri wa ulinzi),uzoefu,pesa(chenge.lowassa.rostam) na pia wana dola(ridhwani.com).Umeshajua ukubwa wa silaha zao?kama utaendelea kubaki humo ndani fahamu kabisa hutofika hata hatua tatu mbele,labda tu uamue kutoka kabisa.Lakini mwita navyokufahamu kuanzia pale DARUSO sina imani sana na unayoyasema,sina imani sana kama una nia ya dhati au ulikuwa unataka umaarufu tu,bado nina mashaka kama umebatizwa na kuwa TRULY ANTI-FISADISM

  uSHAURI WANGU LEO KWAKO NI HUU TU "AMUA LEO KUWA WA MOTO AU WA BARIDI PERIOD"
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hana lolote huyu Mwita, ni opportunist anayetangatanga.
   
 13. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kijana bado sana. Hajui nini cha kusema hadharani, matokeo yake utapoteza grassroot support. Unaowataka sapoti yao ndani ya chama wanaweza kuwa ni wasambaza chai na hawakusoma kama wewe mwenzetu.

  Na viongozi wenzio ndani ya chama utakaotaka sapoti yao kwenye power struggle dhidi yako na huyo emerging kingunge wa CCM, Bw. Nchimbi, ndio hivyo tena umeshawatangaza wana elimu ya darasa na nne. Nani atakutetea ?

  Rudi shule kamalizie madarasa ya public relations, practical politics na uungwana.
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Oct 2, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,406
  Trophy Points: 280
  Na wewe "investigation" ya Dr. Masau vipi, hujamaliza tu?
   
 15. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #15
  Oct 2, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Murrah! Uh! Amang'ana murra!

  Hii kule Arusha tunaita "kupandisha mori". Kwa bahati mbaya huwa inaishia kama hasira za mkizi (malizia...). Hapa kina Nchimbi na wenzie watajisifu kweli kuwa lengo lao limefanikiwa: hawakumtaka kwenye kundi lao.

  Kufa kikondoo au kufa kama chui vyote ni vifo tu, lakini kile cha kudhalilisha kinaumiza zaidi, kwa hiyo hongera murra kwa msimamo, bado unazo nafasi tele katika nyanja nyingine, utafanikiwa tu murra, si lazima ufanyie kazi siasa ama CCM. Nakusihi uendelee na harakati halisi za mapambano ya kuikomboa na kuijenga nchi.
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Oct 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Afadhali huyu opportunist anayetangatanga lakini anasema kweli kuliko mafisadi na wanafiki wanaoiangamiza Tanzania. Wadanganyika wengine hata akitokea mtu anayesema uozo uliojaaa ndani ya CCM bado tutaka kumzodoa na kumponda bila kujali kama anayoyasema yana ukweli au la. Mbona hatuwasikii akina Kikwete, Msekwa na Makamba wakisema uozo uliojaa ndani ya CCM. Hebu kuweni wakweli wa nafisi zenu!! give credit where credit is due siyo kuponda tu bila kutathmini yale anayoyasema Waitara.
   
 17. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #17
  Oct 2, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Watu weweeeeeee! Thats why I love Nyani. Do you wanna me to tell this Kuhani guy to also go back to school so as to study how to do the Dr Masau "Investigation" na kuja na majibu ya kiungwana?

  Asha
   
 18. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  yaani niwe namfungilia mlango akifika ofisini, kumuandalia chai na kupeleka maji kwenye vikao, hilo haliwezekani,`` Kweli bwana waitaraaa hii haijakaa vizuriii, Graduate Aaandae chai?

  Lakini kuna nyumba zinachomwa moto huko Bhumera, wao wapo hapa mjini wamegeuka kukamata magari utafikiri ni trafiki,`` Hii unanikumbusha marehemu Wangwe alivyokuwa akichachamaa Bungeni

  Waitara alisema licha ya CCM kupoteza mwelekeo wa kampeni hizo, kinakabiliwa na changamoto ya kujibu hoja zinazohusiana na kashfa ya ufisadi inayowakabili wanachama wake waandamizi.
  Piga ua garagaza, Kamwe hawana jibu muafaka kwa hilo la ufisadi

  Ushauri wa bure ni kuwa usije hama chama chao, wee komaa nao ndani ya chama chao cha mafisadi mpaka wakufukuze na baada ya hapo ukiingia upinzani nakuhakikishia ubungeTarime ni wako kwani unafanana sana na Wangwe
   
 19. H

  Hamad Yussuf Member

  #19
  Oct 2, 2008
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nampongeza Kijana Waitara kwa kuthubutu, inawezekana kama binadamu kuna mambo yaliyotokea kwenye CCM yamemkera, kama mwenyewe alivyojieleza la msingi nakubaliana naye kwa msimamo wake wa kutetea watu wa Tarime waachiwe wenyewe waamue hatma ya nani awe mbunge wao, badala ya kushinikizwa na mafisadi kwa kuwatumia polisi vibaya, yapo ya msingi sana aliyoyaeleza katika maelezo yake ambayo kama watu makini tunapaswa kuyazingatia, inawezekana aliyoyaeleza yakawaudhi wengine lakini ndio haki na ukweli daima huwa hivyo, wasioipenda haki na kweli daima wanakuwa wanaichukia ikiwekwa hadharani, ninayo imani kwabwa kwa wana JF kwamba ni watu makini wasioshabikia na ambao wenye kuchambua na kujenga hoja za kuisaidia nchi yetu, ninayo matumaini kwamba daima tutaendelea kusimamia kwenye ukweli .
   
 20. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #20
  Oct 2, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  Kithuku you have said all .Mabandiko yako yameanza kunivuta sana na hasa ukisimamia haki bila ya unazi , sawa na shy alivyo anza kuona kwamba huwezi kwenda mbinguni hadi ufe , na ndiyo maana tunautafuta uzima ama ahera tungali hai .Safi sana wakuu .Tuendelee
   
Loading...