Msaidizi wa Membe, Allan Kiluvya azungumza baada ya kurejeshwa na watu wasiojulikana

au wataliundia zengwe kwa Membe..lol..ila mbona amerudi baada ya Rafiki zake kutangaza kumpa masaa 24 Membe kumtoa huyu msaidizi…..mie sitaki kuumiza kichwa siku hizi...nataka nijikite kule MMU sitaki kufa na pressure na mada za siasani
Kwahiyo kumsingizia membe ndio itawasaidia ,unataka kusema wote waliotekwa kuanzia Saanane,Azory, Kanguye walitekwa na membe .Halafu mbona waliowapa wasiojulikana Massa 24 watawataja ndio wakamwachia ? Membe anahusikaje hapo we Lumumba .
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sometimes I miss the old Rebeca 83.

au wataliundia zengwe kwa Membe..lol..ila mbona amerudi baada ya Rafiki zake kutangaza kumpa masaa 24 Membe kumtoa huyu msaidizi…..mie sitaki kuumiza kichwa siku hizi...nataka nijikite kule MMU sitaki kufa na pressure na mada za siasani
 
Msaidizi wa MEMBE 'Allan' anachokizungumza baada ya KUREJESHWA na WATU wasiojulikana.

Akizungumza kwa namna alivyoachwa njia panda ya Segerea amesema “Nilishushwa sehemu ambayo niliona ni sehemu salama kwa sababu nilieweza kupata usafiri wa kurudi kwangu.”

Ameeleza kuwa “Wao wenyewe(Wanaodaiwa kuwa Watekaji) waliuliza ni wapi tukikushusha unaweza kufika salama? Nikawauliza kwani tupo wapi? Wakasema tupo Gongo la Mboto. Nikasema mimi nakaa Kinyerezi mkinishusha njia panda ya Segerea nitakuwa salama.”

Aidha, kwa sababu suala hilo lipo Polisi amesema kuwa hawezi kuelezea ni nini kilitokea huko alikokuwa bali tusubiri tamko au ripoti ya Polisi. “Kwa kuwa mimi ni Mkweli sana na najua Polisi watasema kile nilichosema.”

Lakini pia alipohojiwa kama ataendela kuwa Msaidizi wa Membe, Allan amesema kuwa anatumaini ataendelea kuwa Msaidizi wa Waziri huyo wa zamani kwani amekuwa msaidizi wake tangu mwaka 2012 akiwa Mwanafunzi wa Chuo hadi sasa

Awali, alianza kutoa shukurani zake kwa Wanahabari kwa namna ya walivyojitolea kuhakikisha sauti za familia yake, Wanasiasa na Watanzania wote zinasikika. Pia amemshukuru Membe, IGP Sirro na Polisi wote wa Kituo cha Kawe

Watekaji wa Siku hizi ni Wazuri hadi nimewapenda kwani wanakuuliza wakushushie wapi tena Kistaarabu tu na wanakushusha hapo hapo huku wakiwa hawajakudhuru popote. Natamani nami Waniteke ili wakiniuliza wanishushie wapi niwaambie wakiniacha ndani ya Ikulu ya Tanzania tena Sebuleni kabisa watakuwa wamenisaidia.
 
Nikawauliza kwani tupo wapi? Wakasema "tupo Gongo la Mboto. Nikasema mimi nakaa Kinyerezi mkinishusha njia panda ya Segerea nitakuwa salama.”


Mungu yupo
Ina maana walimshusha usiku sana ili wasionekane?
Au walimziba usoni asiweze kuona nje ya hilo gari?
Ingependeza angeuambia umma ili kujifunza jambo kwakuwa kujifunza hakuna kikomo maana hata watekaji wenyewe wanajifunza kila kukicha
 
Back
Top Bottom