Msaidizi wa Membe, Allan Kiluvya azungumza baada ya kurejeshwa na watu wasiojulikana

Vitendo hivi vya utekaji mpaka wananchi tuanze kuchukua hatua wenyewe ndiyo vitakoma, bila hivyo vitaendelea
Inabidi sasa tunapoyaona mambo kama haya ni kuwavamia na kuwapiga. Au tunatakiwa kuandamana nchi nzima kukataa utekaji. Na njia nyingine ni kuwataja hawa watekaji halafu tuwavamie kwenye makazi yao
 
Anasema alikuwa wapi?? Kwa nani?
Mkuu ukipata mrejesho wowote wa hili swali unitag.....inaonekana huko wanakopelekwa waliotekwa kuna viapo wanapeana hakuna aliyewahi kutekwa akasema alikuwa wapi na ilikuwaje :oops::oops:
 
Wale Marafiki wa Allan mbona Hawaji kumshukuru Membe kwa kupatikana kwa rafiki yao Kama yy alivyofanya?
 
Kuna kitu nyuma ya akili yangu kinaniambia kuwa "Huyu anayedaiwa kuwa msaidizi wa Membe bila shaka atakuwa ni wakala wa #TISS..
Walimchukua wenyewe ili akawape ushirikiano.." Si bure!
 
Sawa Pole Allen,ila tunakuacha kwanza upumzike halafu ili vitendo hivi visirudie ni vizuri sana ukawa wazi bila kuogopa,
kutueleza kwa uwazi kilichotokea tangu mwanzo hadi mwisho.

Nasema hivyo kwa sababu mambo haya yakishaenda huko ulikosema hamnaga mrejesho kwa wale waliopiga kelele.

Vinginevyo wataendelea kusema hii ni video ya kutengeneza kama wanavyosema siku zote.

Wapasukie wazi au wanasemaga waanike kweupe hadharani mchana liwalo na liwe potelea mbali,Naishi leo kesho yangu nayo itafika tu.
 
Msaidizi wa MEMBE 'Allan' anachokizungumza baada ya KUREJESHWA na WATU wasiojulikana.

Akizungumza kwa namna alivyoachwa njia panda ya Segerea amesema “Nilishushwa sehemu ambayo niliona ni sehemu salama kwa sababu nilieweza kupata usafiri wa kurudi kwangu.”

Ameeleza kuwa “Wao wenyewe(Wanaodaiwa kuwa Watekaji) waliuliza ni wapi tukikushusha unaweza kufika salama? Nikawauliza kwani tupo wapi? Wakasema tupo Gongo la Mboto. Nikasema mimi nakaa Kinyerezi mkinishusha njia panda ya Segerea nitakuwa salama.”

Aidha, kwa sababu suala hilo lipo Polisi amesema kuwa hawezi kuelezea ni nini kilitokea huko alikokuwa bali tusubiri tamko au ripoti ya Polisi. “Kwa kuwa mimi ni Mkweli sana na najua Polisi watasema kile nilichosema.”

Lakini pia alipohojiwa kama ataendela kuwa Msaidizi wa Membe, Allan amesema kuwa anatumaini ataendelea kuwa Msaidizi wa Waziri huyo wa zamani kwani amekuwa msaidizi wake tangu mwaka 2012 akiwa Mwanafunzi wa Chuo hadi sasa

Awali, alianza kutoa shukurani zake kwa Wanahabari kwa namna ya walivyojitolea kuhakikisha sauti za familia yake, Wanasiasa na Watanzania wote zinasikika. Pia amemshukuru Membe, IGP Sirro na Polisi wote wa Kituo cha Kawe

Mtekaji ametekwa na alie muajiri... Kwaheri
 
Swali ni kwa nini viongozi wakubwa wa nchi hawakemei vitendo hivi?, ina maana wanafahamu malengo yake
Watakemea nini na wakati wao ndio wahusika wakuu wa utekaji wenyewe ?, mmesahau Makonda alivyo ratibu kutekwa kwa Roma, unategemea kama mkuu wa mkoa angekuwa na nini cha kukemea hapo ?. serikali hii inakuwa nyuma ya matukio yote ya utekaji yanayotokea hapa nchini, Familia ya Allan wametuambia waliiitambua gari na hata dereva aliyekuwa anaendesha gari hiyo, kuna nini kingine ambacho polisi wanakihitaji kushughulikia swala hili ?
 
nadharia ni nyingi sana,sababu tu mtekwaji kaamua kukaa kimya,wamemtaka nini mpaka aogope kusema?

labda sasa utuambie hayo yote yana uhusiano gani na huyu msaidizi,kwanini wasiteke mtoto au mke wa membe,kama lengo ni harakati za membe?
Mkorinto usitake watekwaji wajibu sawa na kichwa chako. Mbona hawakumteka mke wa Mbowe au wa Zitto ?!. Badala yake wasaidizi wao wamekuwa wahanga.

Sijui unabisha nini ?! Kwa Zakaria au Mo ungesemaJe ?!. Fikiri nje ya box
 
Mkorinto usitake watekwaji wajibu sawa na kichwa chako. Mbona hawakumteka mke wa Mbowe au wa Zitto ?!. Badala yake wasaidizi wao wamekuwa wahanga.

Sijui unabisha nini ?! Kwa Zakaria au Mo ungesemaJe ?!. Fikiri nje ya box
ndio maana hata wanaosema aliiba mke wa mtu wanasikilizwa pia,si jukumu lako wala mimi kumsemea mtekwaji.
 
Back
Top Bottom