Msaidizi wa Kufua/ kupika na Kufanya usafi Kwangu

The bump

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
1,136
1,952
Mimi ni kijananinaeishi peke yangu, Chumba ki 1 kisicho na makorokoro mengi ndani,ni Mfanyabiashara au mjasiriamali ninaetoka nyumbani asubuhi sana na kurudi usiku sana.

Kutokana na ratiba yangu kuwa ngumu nimejikuta sipiki nyumbani maana muda nakosa, kufua nakosa muda yani muda ninaopata kufanya kitu changu ni muda wa kwenda kuoga tu ila sina muda wa kufanya kazi nyingine yyte ile.

Nyumba yangu imekua kama stooo,nimechoka kula mitaani,nimechoka kula chipsi (kijana wa kiume) Afya yangu naiona n afya ya fast foods tu,yani kama ni kuku najifananisha na Broiler.

Natafuta msaidizi atakae weza nisaidia kazi Tajwa hapo Juu lakni awe ni wa kike Umri wowote ule,awe binti,awe mama awe Bibi sina tatizo na umri wake awe tu ananifanyia hizo kazi kwa uzuri.

KUPIKA
Atakua anakuja kwangu asubuhi ananipkia chakula cha Usiku (mchana sitokuwepo) chakula kulingana na siku husika nitamuomba anipkie nini,atanipkia kisha atanihifadhia kwenye mahotpots na vyakuhifadhi kwenye friji ataniwekea,nikirudi usiku kazi yangu kupasha na kula.

Mchana atajipikia mwenyewe chakula anachotaka kulingana na kwenye Friji kuna nini,ale ashibe kisha aendeleee na mambo yake mengine sio anipkie mimi huku yeye anakaa na njaa HAPANA,nahtaji msaidizi tutae ishi kama ndugu.

Vyombo nitakavyolia atavikuta asubuhi ila kama nitakua na nguvu vyombo nitakavyolia ntakua nasuuza mwenyewe na kuviweka kabatni.

KUFUA
Nguo ni changamoo sana kwangu eneo hili ndio limenifanya nitafute mtu hasa maalum maana nimeshafuliwa nguo na watoa huduma za ufuaji hawa unaowanunulia sabuni ila ufuaji wao HAPANA KWAKWELI,nahitaji mtu ataefua nguo zangu kwa ubora na kuzifanya zing'ae wakati wote na kunipangia kabatini.

Mimi kazi yangu iwe kuzpga pasi na kuvaa Tu.

USAFI
Usafi ni wakutandika kitanda incase siku nimekurupuka nikajisahau kutandika,kudeki nyumba kufuta vumbi kwa ufupi kufanya nyumba ionekane kweli ina mtu anae deal na usafi, Makochi kuyasafisha Carpet kuliosha wakati wote liwe safi, mengine nadhani mtu mzma anaelewa nini maana ya usafi.

MAHALI PAKUISHI
Nahitaji mtu anaeishi kwake,mwenye makazi maalum hizi kazi zote ni za kuja kufanya na ukimaliza unaondoka kwako/kwenu sihitaji mtu asie na makazi maana sina mahali pakulaza mtu naishi peke yangu na sihitaji mgeni nahitaji tu Msaidizi wa kunisaida kazi tajwa hapo Juu.

MSHAHARA
Mshahara wa huyu msaidizi nitamlipa kwa mwezi na si kwa SIKU,ambao kwa mwezi nitamlipa 210,000 kama jumla ya mshahara wake wa mwezi, hii 210k nimeigawanya kwa mafungu mawili.

Nauli : 60,000Tsh
Pocket Money : 150,000Tsh

Mwisho wa mwezi nitakua nampa 150,000 lakini kutokana na kila siku atakua anakuja na kurudi kwao/kwake nitakua namuachia mezani 2000Tsh hii buku mbili n kwa ajili ya nauli yake ya kwenda na kurudi huko anapoishi,kwa hyo kila siku nitakua nampa nauli TU. Kisha itapofika mwisho wa mwezi nitakua nampa 150,000 ambayo ndio Mshahara wake kwahyo jumla kuuu iafanya mshahara wake uwe 210,000/

Nauli kila siku nimeona nifanye hivyo ila uamuzi ni wa msaidizi akiamua nauli ajitafutie mwisho wa mwezi nimpe 210k yote ni sawa,akiona kila siku nimpe nauli yake kila siku pia sawa.

SWALI
Je, utapata wapi ufunguo wakati naondoka mapema kwa maana nyingine mimi na wewe kuonana itakua mara chache sana je Funguo ya nyumba utaipata wapi? Yawezekana kuna mtu kajiuliza swali la namna hiyo.

JIBU
Kama nilivyosema awali mimi ni mpangaji sijajenga kwahyo hapo nilipopanga siishi peke yangu,kuna wapangaji wengine wenye wake zao wanashinda majumbani 24hrs, kwahyo Hao wapangaji ndio Nitakao waachia Funguo kwahyo ukija nitakuelekeza tu ufunguo uwe unaufata kwa nani na ukiondoka umuachie nani,maana utapochukua funguo n kwa mtu mwingine na utakapoacha wakati ukiondoka n kwengine kutokana na ratba yangu ya kurudi kuwa mbaya n lazima funguo utauacha mahali ambapo huyo mtu najua mida ninayorudi anakua macho kuepuka kusumbua watu wengine.

Naishi MBEZI MWISHO wengine hupaita MBEZI YA KIMARA. Kwa mawasiliano karibu PM.

ASANTENI na MUBARIKIWE, waG fyaaa (wajifyaaaa)

MREJESHO:

Asanteni kwa wote mlio onyesha nia ya kunisaidia na kuhitaji kazi bila ya kuwa na mashaka nami,asanteni sana.

asanteni pia wale wadada wathaminishaji mana wote nmewapata na kuwaona asanteni,kuna wengi sasa wanasumbua wakitaka KAZI lakini mimi siku zote ni mkweli sipendi mtu muongo muong asie straight.

Wadada wa JF waliokuja omba kazi ambao ni member wa JF jamani ni waongo waongo waongo, JF imeharibu watu sana kwenye hii kufata mkumbo,hii tabia ya kutumia FAKE ID watu wanaiendeleza hadi nnje ya JF.

Unamuuliza unakaa wapi,anakujibu nakaa bunju,kwenye story za hapa na pale akiona unaelekea kumpa kazi anakwambia anakaa mawasiliano,unajiuliza sabbu za yeye kusema uongo anapokaa ni ipi hujui,mwingine anakudanganya nakaa peke yangu Kumbe ana mtoto mdogo na Mume Juuu.

Anataka kuja fanya kazi kwako kijanja janja mume wake asijue,kwakua mimi binafsi kwenye story lazima nikubane engo flani Mtu anajaaa mzima mzima,ki ufupi wadada wote Waongo niliowaambia nitawatafuta Mnajijua Acheni hizo tabia za uongo mnapotafuta kazi.

Kuna wakweli ambao sijaonana nao ila nina namba zenu,Kaka yenu ni mjasiriamali ambae kazi kwangu haziiishi at anytime nitawatafuta kwa kazi zingine sio lazima ziwe kazi za kunisaidia nyumbani maana nyumbani tayari nimepata msaidizi moyo wangu ulieridhika nae.

Asante nyingi kwako Yna2 maana wewe ndie uliefanikisha hili Mungu akubariki sana sana.

Ushauri wa bure kwa member wa JF :
Tofautisheni maisha ya JF na maisha nnje ya JF sio kisa JF unatumia Fake ID na nnje ukawa muongo muongo hvyo hvyo,mnakosa vingi na mtajiona hamna bahati kumbe shida ni nyie wenyewe.

Ukweli na Uaminifu ulimwengu wa sasa ni jambo la muhimu sana sana msisahau hilo,hamna mtu yuko tayari kuajiri au kukaa karibu na mtu muongo muongo.

Acheni maigizo mnapokuwa ktk maisha halisi wekeni u JF JF pembeni na mtafute maisha kweli kweli, wakusikia na asikie mliozaliwa na asili ya uongo najua hili linaingilia huku na kutokea kule. shauri lenu.

Mbarikiwe

ANAHITAJIKA MWINGINE :

Kama yupo anaetafuta kazi Nahitaji mdada mwingine si kwangu ila huyu ataenda kwa rafiki yangu ni mdada,aliniona nina mdada akatamani nae apate kama wangu,kwahyo ataepatikna mwingine Karibu PM, Afahamu kuwa anaenda fanya kazi kwa mdada si kwangu. (mimi tayari ninae) Asante.
 
Kwa kijana anaetafuta pakuishi,nina shmba liko mlandizi nahtaji msimamizi sio shamba n kiwanja ila napaita shamba kwasababu wengi majirani yangu hulima kasoro mimi Tu,

NAHTAJI MTU wa kwenda kuishi huko aniangalizie tu kiwanja changu,Chakula juu Yangu,malazi Juu yangu,Afya yake Juu yangu Mshahara kwa mwezi 100,000tsh ataekuwa tayari namkaribsha PM.

kazi za kule n kufyeka fyeka tu majani na kazi za hapa na pale na kunijulisha kila kinachoendelea kwa majirani zangu.

Wajifyaaa.
 
Eeeh! Una miaka mingapi? Kabila gani au nyanda zipi? Kabila la mtu muhimu. Ndiyo maana hata hospitali au polisi utaulizwa kama id yako. Na dini pia muhimu Ili nisije pika kitimoto.
 
maelezo marefu! si ngesema unahitaji mke?

ukimpata binti alikuwa anatafuta ndoa, atakuwa anajilaza hapo mpaka unarudi unamkuta mwishi wa mambo ni kufanyana tu.. hii hali ina asilimia 70 kutokea endapo utapata binti miaka 24 - 32

All in all, nakutakia mafanikio kwenye hilo.

wasichana wa jf changamkieni fursa hiyo yani unakuwa mke alafu unalipwa 210k kwa mwezi.
 
Eeeh! Una miaka mingapi? Kabila gani au nyanda zipi? Kabila la mtu muhimu. Ndiyo maana hata hospitali au polisi utaulizwa kama id yako. Na dini pia muhimu Ili nisije pika kitimoto.
Kabila : 1 YA MAKABILA yapatikanayo SINGIDA

DINI : N wale wala kitimoto wazuri tu so sina masharti eneo hilo
 
Mnyaturu mwenzangu tunakushauri tukutafutie houseboy au Kama utaforce housegirl Basi uambatanishe na kishika UCHUMBA kwa sababu sote tunajua lazima umrombe TU binti wa watu nyau wewe
Sasa Ndege john wanihukumu mapema😂 Unajua sio kila mwanamke hufaa kudukuliwa?

siwezi dukua mwanamke wa mtu jamani,i do respect me and my self and if i do so Huyo mufanyakazi ani BAKE.
 
maelezo marefu! si ngesema unahitaji mke?

ukimpata binti alikuwa anatafuta ndoa, atakuwa anajilaza hapo mpaka unarudi unamkuta mwishi wa mambo ni kufanyana tu.. hii hali ina asilimia 70 kutokea endapo utapata binti miaka 24 - 32

All in all, nakutakia mafanikio kwenye hilo.

wasichana wa jf changamkieni fursa hiyo yani unakuwa mke alafu unalipwa 210k kwa mwezi.
Kigezo no.1 uwe na makazi yake sijali anaishi kwake au kwao muhimu asiwe tu Muwindaji

Mkuu MKE mimi hapana,unahisi kwa maelezo hayo nakosa vile vdada vya hit n run halafu nikakigeuza

mfanyakazi indirect way? yani nakinunulia smart phone ya 250k kila siku nakiambia kije kifanye kazi japo sikiiti kwa kukiambia kinakuja kufanya nini,then kinanitimizia mahtaji yangu yote?

Sihitaji wahivyo mkuu na siwezi hata kwa bahati mbaya date na mdada ataekuwa msaidizi wangu,NEVER. Nina sifa na vigezo vingi sana vya hadi mwanamke kuingia ndani kwangu Achilia mbali kupanda kitanda ninacholala.

Mimi ni moja ya wanaume wasioamini ktk mapenzi hasa kuoa au kuwa na mke,sipo kundi hilo na sihitaji i better find someone muda utapofika anizalie mtoto KWISHA habari,nitalea mwanangu . Sihitaji MKE au Mpenzi. STAKI.

i just love my self KWISHA.
 
kama kuna tasisi ya kusaidia upatikanaji wa wadada wa kazi tusaidieni mawasiliano yake

hwa wadada/wakaka wa kuokoteza vijijini nafikiri tuachane nao
mtu anakuja leo keshokutwa anaomba kuondoka kwambaq kaitwa na babu yake
akifika huko unaambiwa ukajitambulishe na urudi naye
Hao wa kampuni ndo balaa zaidi. Sisi tuliwahi kupigwa tukio na housegirl wa kampuni, baada ya kufuatilia ikaja kugundulika ni mpango wa hiyo kampuni huwa wanachonga madili na hao wadada kupiga matukio wakishaanza kazi sehemu.
 
kama kuna tasisi ya kusaidia upatikanaji wa wadada wa kazi tusaidieni mawasiliano yake

hwa wadada/wakaka wa kuokoteza vijijini nafikiri tuachane nao
mtu anakuja leo keshokutwa anaomba kuondoka kwambaq kaitwa na babu yake
akifika huko unaambiwa ukajitambulishe na urudi naye
Anaenda kuripoti kwanza alafu kazi baadae, bila kujali gharama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom