Msaidizi wa Benard Membe, Allan Kiluvya adaiwa kutekwa na watu ‘wasiojulikana’

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Wakuu,

Taarifa nilizozipata punde zinaonyesha ndugu Allan Kiluvya ametekwa jana usiku maeneo ya Mbezi.

Allan anadaiwa kuchukuliwa na watu takribani 7 waliokuwa na silaha.

Benard Membe ambaye alikuwa Mbunge wa Mtama, ni mwanasiasa aliyefikia viwango vya juu nchini Tanzania, alikuwa Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika serikali ya awamu ya nne, iliyoongozwa na Jakaya Mrisho Kikwete.

Membe aligombea Urais kwa tiketi ya CCM 2015 na kuchujwa katika vikao vya ndani ambapo hatimaye Magufuli kupewa ridhaa. Toka wakati huo, amekuwa kimya na kutojishughulisha na masuala ya kisiasa.

Soma zaidi...

Msaidizi wa Membe adaiwa kutekwa

JUMAPILI , 7TH JUL , 2019

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Allan Kiluvya ambaye anatajwa kuwa ni msaidizi wa Waziri mstaafu wa Mambo ya Nje ya wa Serikali ya awamu nne, anatajwa kupotea baada ya kuchukuliwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.


Tukio hilo limetokea usiku wa jana alipokuwa na baadhi ya marafiki zake katika eneo la Mbezi jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa mtu wake wa karibu ambaye amefahamika kwa jina moja tu la Magret, amesema mara ya mwisho yeye na Allan walikuwa pamoja wakitokea eneo la starehe, kabla ya kutokea kwa watu hao 7, wakiwa kwenye gari aina ya Land Cruiser ambayo ndiyo ilimchukua na kuondoka naye.

Aidha Magret ameeleza kuwa wameshatoa taarifa za awali kwa Jeshi la Polisi kwa ajili kuanza kwa uchunguzi wa kupatikana kwa Allan Kiluvya.

EATV/EARadio Digital imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mussa Taibu kwa ajili ya kuzungumzia tukio hilo, ambapo amesema, "tumepata taarifa za tukio hilo kutoka kwa ndugu wa Allan, na sisi tunaendelea kulifuatilia kujua ni kwa namna gani alichukuliwa lakini siwezi kusema ametekwa kwa sababu bado hatujathibitisha".

Juhudi za kumtafuta Bernard Membe bado zinaendelea.

Msikilize Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinonfoni akizungumzia tukio hilo.

====

UPDATES: 09 JUL 2019

Hatimaye amepatikana. Zaidi soma;

 
Ila wanafurahia kuwa wale kumbe na wao yamewafika nasi tuwatetee na kuoaza sauti zetu bila kuangalia maana ndio Nazi yetu
 
Back
Top Bottom