Msaidieni huyu ndugu kujibu hilo swali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaidieni huyu ndugu kujibu hilo swali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by boss80, May 14, 2011.

 1. boss80

  boss80 Member

  #1
  May 14, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wadau hebu tusaidiane katika hili, mimi ni mkazi wa mji mdogo waTunduma mkoani Mbeya.

  Hivi karibuni nilihudhuria mkutano wa Chadema mjini hapa na nimeishi hapa kwa muda zaidi ya mika 30.

  Tokea mfumo wa vyama vingi vya siasa umeanza, na mikutano yote ya kijamii sikuwahi kushuhudia kusanyiko kubwa la watu kama hili la hivi karibuni katika mkutano wa Chadema mjiji hapa.

  Nina mengi maswali ya kujiuliza, lakini kubwa ni hili. Kwa nini watu hujaa sana katika mikutano ya Chadema?

  Kwani ni ukweli kuwa wapo watu ambao hutembea kwa miguu zaidi ya kilometa 5 kufuata mkutano.

  Imetokea pia hapa Tunduma, inanikanganya sana.

  Kwenu wadau.

  Source: Mjengwa blog
   
 2. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 868
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  mkuu usijali ndo movement imeanza,soon tutakua kama Tunisia tukianza kuwapopoa mafisadi barabarani,CDM is the key to changes and development,viba CDM
   
 3. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Umeuliza swali zuri na swali hilo litazaa majibu ya aina tofauti tofauti kutegemeana na utashi wa kisiasa wa mtu na mtazamo wa mambo.

  Inawezekana hiyo ni ishara ya kupendwa na kuungwa mkono kwa chama hicho. Vile vile inawezekana kwamba watu wamekata tamaa na sasa wanatafuta sehemu ambayo watakusanyika na kumaliza hasira zao kwa kutoa matamko mbalimbali.

  Uko pia uwezekano kwamba watu hawana shughuli za kufanya na hiyo ndiyo outing yao na fursa ya kuwaona viongozi waliowasikia kwa muda mrefu kupitia vyombo vya habari.

  Tusipuuze pia uwezo wa ushawishi wa viongozi hao na kwamba mahudhurio hayo ni matokeo ya ushawishi wao.


  Lililo wazi ni kwamba watu wana manung'uniko dhidi ya serikali na hatimaye chama tawala. Wamekata tamaa na sasa wanadhani hao wanaotembea kote nchini pengine ndiyo wakombozi wao.

  Lakini kusema kwamba yatatokea yaliyotokea Tunisia au Misri ni kukosa uelewa wa jinsi siasa za dunia zinavyokwenda.

  Mazingira ya huko na huku ni tofauti na possibility ya kuwa na replication hiyo ni ndogo au hakuna kabisa. Hoja zetu na za kwao ni tofauti na hivyo hivyo mfumo wa uongozi na uendeshaji wa nchi.

  Sisi tuna tatizo la msingi la ugumu wa maisha na kupanda kwa gharama za maisha. Tatizo hili halipo Libya lakini kuna uasi unaendelea.

  Institutions of democracy huko Arab world hazikuwepo na ndiyo sasa kuna harakati ya kujaribu kuzileta. Wakubwa wao kule wamejigeuza watawala wa milele na kazi yao ni kurithisha dola kwa familia zao.


  Lakini bado nina-share na wewe hiyo concern yako kwamba ufuasi wa CDM umekua kwa kasi sana katika miezi ya hivi karibuni na kwa hakika kuna haja ya kufanya utafiti wa kina juu ya hii changing fortune kwa chama tawala.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  May 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145


  Time-bomb!. wakubwa walipuuza kulitegua sasa liMElipuka. In practicle terms, hakuna mzazi yeyote anayetamani mtoto wake akiwa mkubwa awe machinga, auze viberiti, asukume mkokoteni, aokote chupa!.Hakuna. Au hakuna mjamzito anayefurahia kujufungulia sakafuni huku akiambiwa alete nyembe, maji, gloves. Hakuna mwenye saluni (za kike na kiume) anafurahia kupiga miayo kwa sababu umeme umekatika. Hakuna mtu anashangilia kuona bei za bidhaa zinapanda kwa kasi kila kukicha. Mbaya zaidi, wengi wanachukizwa sana tena sana kuona watu waliopiga kambi majimboni, wengine wakapiga magoti kuomba kura lakini mara walipopata nafasi ya kuingia bungeni wakaamua waziwazi kuwasaliti na kusimamia maslahi ya wachache.

  Sasa wananchi wameamua kuhudhuria mabunge yao huku mtaani maana la Dodoma limekuwa la watu 'maalumu kwa kazi maalum'. Ila Mama Makinda anatakiwa achugue ama aendeshe bunge la wawakilishi wa wananchi kwa manufaa ya wananchi AU wananchi wataendesha mabunge yao wenyewe 'kama ambavyo wataona inafaa'. HAKUNA MULTIPLE CHOICE KWENYE HILI.
   
 5. M

  MndemeF Member

  #5
  May 14, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wananchi sasa wamepata muamko wa kisiasa tofauti na zamani zile. Wengi wamekatishwa na tamaa ya serikali ya sasa kwani inajali wachache na wengi wanaachwa katika mataa. Yaanu sasa wanatafuta chama ambacho wanadhni kitakuwa ndio mkombozi wao. Na kwa ukweli kwa sasa hakuna chama kingine zaidi ya chadema.
   
 6. k

  kakini Senior Member

  #6
  May 14, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  mbona unaandika utumbo na mavi yako hapa????
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  May 14, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu you are the one of the few greater thinker we have here. Thank you for your usefull contribution.
   
 8. s

  seniorita JF-Expert Member

  #8
  May 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yes I share your sentiments, well thought and well said....
   
 9. s

  seniorita JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ndugu kutukana si ustaarabu hata kidogo, tena unamtukan amtu ambaye ametoa hoja yake vizuri na wewe badala ya kujibu hoja by hoja unatukana matusi.....sasa kama ya mwnezako uaita utumbo na mavi, je matusi yako yataku-label wewe kuwa ni nani na jibu lako tuliite ndio ice cream na soda? Please think before you write...mods please watch out for this person, matusi yanatukera bwana na anachafua JF...hafai kuwa hapa
   
 10. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,468
  Trophy Points: 280
  Wamesikia mabadiliko yako chadema pekee,hivyo basi wanakuja kupruvu kutokana na hoja zao.
   
 11. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watanzania hawa wamekata tamaa ya maisha sasa lile dude walilokuwa wakilitegemea limewa let down sana kwahiyo wametafuta mbadala wa kuwaondolea matatizo yao na kurudisha matumaini yaliyopotea na si kimgine sasa ni CDM ambao wanaonekana kuwa na sera nzuri ambazo zitzwasaidia watanzania hawa. hiyo ndiyo sababu kubwa ya kuungwa mkono kwa CDM na watu mbalimbali wa rika, kabila na dini tufauti tufati.
   
 12. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Watoto waliolelewa kwenye mazingira magumu utawajua tu! Ilikuwa lazima uingie humu kama huna hoja? Tunayaweza na sisi tukitaka lakini huu siyo wakati wake.
   
 13. f

  frankkarashani Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nape mkubwa wee!!!
   
 14. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Broda,
  Huyo unayemtukana kakosea wapi?
  Kwa kutumia akili kidogo tu, huyo unayemtukana ni analyst mzuri sana wa chanzo cha mikusanyiko hiyo, sielewi unambeza kwa kusimamia nini!
  Sielewi kama ni ushabiki wa kiwango gani, au ni kukosa uelewa kabisa, ndipo mtu anaanua kujipostia maneno yoyote yasiyo na hekima kiasi hiki!

  Waheshimu wenzio jukwaani, na wewe utaheshimiwa!
   
 15. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  what u write is what u are........ itabidi urudishwe milembwe
   
 16. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #16
  May 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Tunduma ina jambo na Chadema, ambalo limeingia kwenye vitabu vya historia.
  Wakati wa uchaguzi, hapa Tunduma ndio panasadikika palikamatwa mabox ya kura za rais, ZIKITOKEA Afrika Kusini, ambazo tayari zilikuwa zimeshamchagua JK...
  Japokuwa jambo hili lilifunikwa funikwa na kuwa 'sealed' kwa kauli kwamba Dr Slaa ni MZUSHI, MWONGO, na MROPOKAJI, lakini naamini wanaTunduma ndio wanaojua hasa ninini kilichoendelea kuhusiana na kadhia ile ya mabox, na hivyo huenda hiyo ndiyo driving force inayosukuma mioyo yao kutenda hayo wanayotenda!

  Lakini pia ikumbukwe kuwa hapo Tunduma kulitokea vurugu mwaka 2009, ambapo polisi walifyatua risasi na kuwaua baadhi ya raia pale, ambapo wengine walikuwa hata hawahusiki na matukio hayo!
  Hii ilipanda chuki kubwa sana kati ya serikali ya ccm na wananchi...na matunda yake yanaonekana!
  Ni mawazo tu, na inawezekana isiwe lolote kati ya hayo!
   
Loading...