Msafara wa Waziri Wassira wapigwa mawe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msafara wa Waziri Wassira wapigwa mawe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 2, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,886
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Waziri Wassira apigwa mawe

  • Magari ya viongozi waliofuatana naye yapasuliwa vioo


  na Berensi Alikadi, Bunda
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu


  JESHI la Polisi wilayani hapa, linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kuupopoa kwa mawe msafara wa viongozi wa wilaya, akiwamo Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira.

  Tukio hilo lililosababisha magari kadhaa kupasuliwa vioo, lilitokea juzi wakati msafara wa viongozi hao ukitokea katika sherehe za kuuaga mwaka 2008 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2009, huku gari la Waziri Wassira likinusurika baada ya kupita kwa kasi eneo hilo.

  Tukio hilo lilitokea juzi, majira ya saa sita usiku wakati viongozi hao wakirudi majumbani mwao, wakitokea katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bunda, kulikofanyika sherehe hizo, zilizokuwa zimeandaliwa na mkuu wa wilaya na kuhudhuriwa na Waziri Wassira, ambaye alikuwa mgeni rasmi.

  Viongozi hao walikumbana na zahama hiyo mara baada ya kufika eneo la Nyasura, ambapo walikutana na kundi kubwa la vijana waliokuwa wakisherehekea kuupokea mwaka mpya.

  Kama vile waliamrishwa na mtu, baada ya kuona msafara huo, vijana hao kwa nyakati tofauti kila mmoja alitafuta jiwe na kuanza kuyatupia magari hayo, huku wakiuita msafara huo kuwa ni wa mafisadi.

  Magari yaliyopondwa mawe na kuvunjiwa vioo ni la Mamlaka ya Maji mjini hapa, lenye namba DFP 1949, aina ya Toyota Land Cruiser na SM 2986 Toyota Land Cruiser, ambalo lilikuwa limewabeba viongozi wa mji huu, kwa ajili ya kuwarudisha makwao.

  Magari mengine ni pamoja la Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, SM 4225, la Katibu Tawala, STJ 2884, ambalo lilipasuliwa kioo wakati likiwa limetoka kumsindikiza Waziri Wassira nyumbani kwake.

  Gari jingine lililokumbana na mkasa huo ni lenye namba za usajili T 694 ADJ, linalomilikiwa na Hospitali Teule ya DDH.

  Aidha, vijana hao licha ya kulirushia mawe gari la Waziri Wassira, hawakuweza kulisababishia uharibifu, kwani lilipita kasi katika eneo hilo, ambapo nyuma yake, lilikuwa likifuatiwa na gari la wanahabari.

  Wengine waliopigwa mawe na kundi hilo la vijana ni pamoja na muuguzi wilayani hapa, Nelson Malisa, ambaye alikuwa akiendesha pikipiki aina ya Toyo na Mwenyekiti wa Mtaa wa Migungani, Simon Mwita, ambaye amejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya DDH .

  Kwa mujibu wa polisi, watuhumiwa hao watawafikisha mahakamani muda wowote kujibu tuhuma zinazowakabili.
   
 2. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  As Obama puts it: ”We should be able to disagree without being disagreeable”. I think that the people of Bunda have lost their marbles. It is despicable that drunken mobs among them wonder through our streets, and in their drunken bliss, stone those they do not agree with.

  In Tanzania, we oppose our political rivals with words, not with stones. It is my ardent hope that the Police will speedly prosecute everyone who was involved in this sordid mess.

   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Huu utamaduni unaashria kitu mbaya kwa Taifa letu. Sasa watu wakipata silaha za moto je?. Inabidi tuulaani kwa nguvu zote hii tabia na njia pekee ya kuonesha hasira zetu kwao ni kutowapigia kura si kuwapopoa mawe. Pia tume za uchaguzi kutenda haki katika chaguzi ili matokeo ya uchaguzi yawakilishe maoni ya wananchi katika kuwachague viongozi wanaodhani wanawafaa.
   
 4. M

  Mbunge Senior Member

  #4
  Jan 2, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KATIKA hali inayoonesha hatari kubwa ya vijana kukosa ajira hapa nchini Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa S.M.Wassira juzi alifunga mwaka kwa kukoswa koswa na mawe ingawa wasaidizi wake kadhaa walijikuta wakidondokewa na vioo vya madirisha ya magari yao baada ya kupopolewa na mawe ya vijana waliochoka ufisadi huku ahadi nyingi lakini ajira sifuri!


  Inaaminika bwana huyu ni rafiki wa karibu wa waziri mkuu mmoja wa zamani na mrfanyabiashara mmoja mwenye asili ya Afghanistani!
   
 5. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2009
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pamoja na kuporomoka maadili ya vijana wetu, hayo magari hapo juu ni mali ya uma na hayatakiwi kuendeshwa hovyo hovyo. Sina shida na gari la waziri lakini hao wengine wangeweza kutumia basi ndogo ili kupunguza matumizi. Wafanye hivyo mkesha wa mwaka mpya ujao.
   
 6. M

  Masatu JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hakuna chochote ni stunts tu kama kweli wana hasira wazielekeze kwenye sanduku la kura sio kuharibu mali za umma. Sasa wamevunja magari ya serikali na kusababisha hasara kwa ambayo in one way or another walipaji ni wao kupitia kodi zao!

  Huu ni ujinga wa hali ya juu na unatakiwa kukemewa na kila mpenda nchi.
   
 7. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2009
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na hao ambao hawapigiwi kura kama wakurugenzi wa halmashauri wafanyweje wanapotumia magari ya serekali usiku na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa?
   
 8. E

  Eric Ongara Verified User

  #8
  Jan 2, 2009
  Joined: Sep 19, 2006
  Messages: 165
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Taifa limefika pabaya! Ni vizuri tukaangalia chanzo cha haya? imekuaje tumefika hapa? Mbona watu wamekataa tamaa na mfumo na taratbu za kisheria? hii inaashiria nini?

  Tatizo la wananchi kukosa subira na kujichukulia sheria mkononi linadhidi kukuua. tunalishuhudia kila siku watuhumia wa uwizi wakichomwa moto hadharani na umma ni kama umehalalisha vitendo hivi, leo wamevuka mstari wameingia katika siasa, tutafikia hatua watuhumiwa wa ufisadi watachomwa moto hadharani, watu hatasubiri kisutu tena, huko ndiko tunakoelekea kama hatujirekebisha haraka.

  Siungi mkono utamaduni huu mbaya na wa hatari sana, ni lazima turejee katika utawala wa sheria na haki ili kurejesha matumaini, pia serekali iongoze kasi ya kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi hususani suala la ajira kwa vijana lasivyo taifa litawaka moto.
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hili ni fundisho kwa Wassira ili aache kuongea ovyo na kuunga mkono mafisadi.
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ni vizuri kukaa na kutafakari kwa kina nini hasa chanzo cha tabia hii inayojijenga kwa kasi sana ndani ya jamii yetu ya kuwapopoa mawe viongozi wa serikali!! Kuwakamata na kuwafunga hawa vijana hakutatusaidia, serikali inabidi ihakikishe kuwa ufisadi unatokomezwa ili vijana waweze kupata ajira. Ukichunguza kwa makini wanaopopolewa ni wale wanaohusishwa na ufisadi; kama huyu Wassira yeye ni mtu wa karibu na mafisadi wakuu wa nchi wakina Lowassa, Diallo, Chenge , Lowassa, Rostam na huyo muaFGHANISTAN wake. Do not dismiss hawa wananchi kama ni walevi wanajua wanachokifanya na wanawafahamu nani mafisadi katika jamii yao. Si mnakumbuka Wassira alivyokuwa anayapigai kelele na mayowe magazeti kuwa yasiandike mambo ya EPA!!
   
 11. M

  Masatu JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hao wasiopigiwa kura wanateuliwa na waliopigiwa kura. Hivyo tukichagua viongozi wazuri na watateua watendaji wazuri
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwalimu Moshi,
  The people of Bunda have not lost their marbles. They have lost their patience. You can promise some people some of the time but when you fail to deliver do not expect to be showered with flowers. CCM is facing a very hard time in Mara maybe except only in Mukono's constituency. I hope the opposition is listening.
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mkuu ni bora wawapopoe tu mawe maana kwenye sanduku la kura nako wanafanya ufisadi tena si ndo wao wenye dora wanweza kupindisha matokeo watakavyo lakini nguvu ya umma ndo yenye nguvu ipo siku watashindwa hata pa kukimbilia hawa mafedhuri.
   
 14. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Huna haja ya kujuiuliza kwa nini viongozi wanapopolewa mawe, ni kwa sababu ya uongo kila msafara wanaingiza hela halafu unaleta longo longo zako za ahadi za kipuuzi watu wameshachoka sana na ujinga wao.

  Nafikiri tujiandae na vita inakuja kwenye uchaguzi ujao.
   
 15. share

  share JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,295
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  Siungi mkono uhalifu wa vijana, lakini pia viongozi wetu wanavuna walichopanda kwa jamii. Hawa vijana hawakuwa barabarani kusubiri msafara wa waziri. Walikuwa wanasheherekea mwaka mpya kivyao. Ghafla msafara wa waziri unapita na wao wanaanza kutafuta mawe kuwapiga wakidai ni mafisadi. Kumbe hata kama wasipowapiga mawe, bado chuki ya raia kwa viongozi wao imejengeka ndani ya mioyo ya raia. Kupiga mawe ni matokeo tu ya uadui wa ndani uliojengwa na viongozi wenyewe kwa raia kutokana na matendo yao. Tumefikaje hapa ndilo swali la kujiiuliza. Mkuu Hostede ametoa hoja nzuri - ni chaguzi za kiujanjaujanja zinazowapa ushindi watu wasiostahili. Maoni ya watu yakifuatwa ipasavyo kwenye sanduku la kura, na serikali ikajitahidi kukemea vitendo vya rushwa ili tuwapate viongozi chaguo la wananchi, watakaojituma kwa wananchi, sidhani kama wananchi watakuwa vichaa kutafuta mawe kuwapiga viongozi wao. Wananchi wanawapiga mafisadi siyo viongozi wao. Viongozi wanapeperushiwa bendera, kanga, vitenge na matawi ya miti, siyo mawe. Hao wanaopigwa mawe ni maboss walijivua uongozi. Maboss walishajivua uongozi, badala yake wamejifanya watawala, kuwaibia wananchi, na hata kutokuwa na lugha nzuri kwa wananchi maana wananchi hawakuwachagua. Fedha zao zilinunua kura, hivyo wanaheshimu fedha zao siyo wananchi. Wasipojirekebisha tutasikia mahali pengine wamepigwa mawe (siyo Mbeya na Bunda peke yao).
   
 16. share

  share JF-Expert Member

  #16
  Jan 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,295
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  So what? Kwani Benz pale ikulu zimeharibika au kupopolewa kwa mawe hata walipa kodi tulazimike kubeba gharama kubwa ya kununua BMW mpya? Kwani mashangingi ya serikali ni mabovu mpaka tulazimike kubanwa kodi zetu tununue mashangingi mapya kila baada ya miaka 2? Umesikia Mabenzi ya BOT yaliokuwa grounded! Fedha ngapi za kodi zinaibwa kwenye halmashauri zetu? Makongamano mangapi yanapoteza fedha za kodi bila sababu nzito? nk. nk. nk. Wewe umeona kodi ya kununua vioo tu ndiyo inakupeleka kuita "Huu ni ujinga wa hali ya juu"?! Wananchi wamechoka na mabosi (watawala). Wanataka viongozi. Kupiga mawe ni dalili tosha ya kuonyesha jinsi walivyochoka. Kumbuka walianza kwa kuzomea (unakumbuka mawaziri walivyozomewa wakipita kuinadi bajeti?). Sasa wanaonyesha hisia zao tena kwa ngazi ya juu kidogo - kupiga mawe. Hali isipobadilika, nina wasiwasi wanaweza kuonyesha hisia zao hata kwa kurusha baruti za kienyeji. Cha maana watawala wabadilike wawe viongozi ili wapate heshima ya wananchi. Kama hawana uwezo wa uongozi, wasitumie fedha kupata uongozi - wataaibika kwa kupopolewa na mawe. Viongozi bora wapatikane kihalali kwenye chaguzi halali. Tume ya uchaguzi iwe makini. Hatutaki mambo ya kenya yatokee Tanzania.
   
 17. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Inaelekea mengi ya hayo magari yalikuwa yanafanya safari ambazo ni kinyume kabisa na kazi zilizokusudiwa.

  Ukiachia waziri, hao wengine hawakutakiwa kuwa kwenye hayo magari muda huo.
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Inaanza kuwa kama ile PICHA kali sana mwaka jana ya THAILAND. Walinifurahisha hawa Wathai pale walipopita na Mgari wa Kinyesi na KUMWAGA mbele ya geti la PM ambaye alikuwa kajifungia ndani. Wao nao shida yao ni hiyohiyo kuwa MAFISADI kwenye uchaguzi wanaiba kura au kuhonga. Sasa dawa ni kum-mwagia ....... loo, sijui heri upopolewe mawe au UWEKEWE hiyo perfume.
   
 19. M

  Mundu JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ahadi zisizotekelezeka za CCM ndizo zilizowadanganya wapiga kura hususan vijana na hatimaye wakakichagua chama na rais wa CCM.

  Sasa vijana wamesubiri maisha Bora hakuna, ajira hakuna lakini kila kukicha viongozi wanafanya masherehe ya kupongezana kama hayo ya kufunga mwaka. Ni heri wangekuwa wametoka kufungua zahanati ya kijiji au kituo cha Polisi... ingekuwa ni kwa faida ya Umma. Sherehe ya funga mwaka kwa hela za Serikali na miundombinu ya Serikali huku wananchi wanalala hoi si ni kuwatia hasira bure?

  Wanapopata nafasi ya kuwapopoa wawapopoe na kuwazomea pia, kwani miaka hii mitano wameshachelewa... lakini akili kumukichwa... Uchaguzi wa 2010.. kura zao wasikipe chama cha mafisadi.
   
 20. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #20
  Jan 2, 2009
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaani msafara wa viongozi umepigwa mawe, watu wamekamatwa ASAP na wako polisi na wanafikishwa mahakamani na JF kila mtu anacomment.

  Vibaka wanapotuhumiwa kuiba na kupigwa mawe na kuchomwa moto, kila kitu shwari na polisi hawakamati mtu na JF hamna hata topic inayoanzishwa in most cases.

  Nadhani SISI WATANZANIA NI VICHAA NA KWA KWELI NO WONDER TUKO MASKINI NA NCHI INAZIDI KUDIDIMIA.
   
Loading...