Msafara wa rais magari 23 pikipiki 2 je hii ni sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msafara wa rais magari 23 pikipiki 2 je hii ni sawa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ntemi Kazwile, Apr 2, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wadau nimeshitushwa na utitiri wa magari kwenye msafara wa rais (umenipita mitaa ya Kibamba) bila shaka unaelekea Msoga kwa mapumziko ya week end.

  Hizi zote ni kodi za watanzania masikini zinazoteketezwa, na huyu ndiye rais anayetaka tumwamini kutuletea katiba itakayo kidhi matakwa ya taifa hili kwa miaka 50 ijayo!

  Na ile ambulance ya Group 5 bado ipo, sijui serikali hawajui zinapouzwa ambulance? Au Mhimbili hakuna ambulance???
   
 2. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha ajabu hapo. Huyo ni Rais wa Nchi kumbuka si mwenyekiti wa kijiji. Tembea uone mbona huyu ana nafuu. Je hukuona gari zimefungwa MG juu na askari wamevalia kivita wakisafisha njia ya mkuu wa nchi? Je hukuona Helkopta zikipishana angani kuongoza msafara?

  Mbona ubadhirifu ni mwingi tu nchi hii? hata hao tunaosema ndio wapinga ufusadi mbona misafara yao ni mikubwa tu?

  Kweli kunya anye kuku!!

  Itifaki ikizingatiwa msafara huo ni mdogo kwa mkuu wa nchi!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sikubaliani na wewe, Yes Marais wa Marekani wana misafara mikubwa na sophiscated zaidi lakini uchumi wa Marekani ni mara milioni ya uchumi wetu ukitaka kujilinganisha na Wamarekani umekwisha! Hizi Vougue na VX zote za nini????
   
 4. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Msafara wenye magari mengi zaidi kwa africa ni wa kiongozi wa libya. Msafara unaokwenda kasi zaidi kwa africa ni wa rais wa kenya. Ulinzi (magari mengi) pia una determine jinsi rais asivyopendwa (ana maadui wengi)
   
 5. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2011
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Guys, has any of u seen convoy ya UK prime minister? Piki piki 2, land rover freelander, Rover ya primemister, freelander na mwisho piki piki 2. Now hii ni nchi inayofadhili maskin Njaa Kaya na nchi yake.
   
 6. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Kwenye suala la usalama wa Rais tusiquestion wala kutaka structure yake!
   
 7. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  NIMEKUTANA NA HUO MSAFARA WA MALANDCRUISER NA MAAMBULANCE NA MAPIKIPIKI ,NIMEKUTANA NAO JANGWANI MIDA YA SAA TATU NA NUSU HIVI KWELI JK NI FISADI

  KILICHONISHANGAZA MIMI NI KUWA KUNA MAGARI KAMA MANNE LANDCRUISER NYEUSI KUBWA GX V8 HAZINA WATU YUKO DEREVA PEKE YAKE,HII INA MAANA MSAFARA WA JK UNA MAGARI MENGI KULIKO WATU MMH'''

  nchi yetu uchumi wao
   
 8. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huu hapa wa Marekani...magari kumi tu

  [​IMG]
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Wala sikubishii...........

  [​IMG]
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  wapi hao? na huwa na msafara wa magari mangapi na kwenye shughuli ipi?...
  ni ajabu kweli mtu kama wewe kutetea rais kuwa na msafara wa magari zadi ya 20...wakati angeweza kutumia magari yasiyo zidi 5...
  inaoneka wewe huwa unatembea sana..lakini naomba nikuulize msafara wa raiswa kenya huwa magari magapi? maana baadhi ya mawaziri walishawahi kuja na coaster hapa Arusha...
   
 11. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ahsante mkuu unajua tena sisi wa ng'waluzwilo hatujafika huko kwao kuona misafara yao
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimetafuta kidude cha thanks sikioni...Thanks
   
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wingi wa magari katika msafara ndio unaoleta usalama? Ni dhahiri kuwa kama kukitokea jambo fulani, wingi huo wa magari ndio utakuwa chanzo cha kupunguza usalama. Na hizi barabara zetu zilivyo, itakuwa ni kasheshe!
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huu hapa wa Malkia...magari sita tu

  [​IMG]
   
 15. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Sijaona alipofananisha na Merekani, naona wewe ndio unafananisha na Merekani na kumtia maneno yako kinywani mwake. Wacha kuchakachuwa.
   
 16. m

  mao tse tung Member

  #16
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ambulensi ni muhimu kwani kunakajamaa huwa kana kaugonjwa kale ka kuanguka anguka. na leo si unajua UDASA wanakongamano? hivyo kakisikia hoja zinavyojengeka hapa na kuwasilishwa haka kajamaa ni lazima kiamguke. sema sikuhizi inakuwa siri wanaficha kakianguka tu, kanaingizwa ndani ya ambulance.
   
 17. shanature

  shanature JF-Expert Member

  #17
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 718
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  hahaha mh!
   
 18. K

  Kisaa kyafo Member

  #18
  Apr 2, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli bwanamageuko ume├Ângea na una akili,msafara wa gari 23 kwani una tatizo gani,apo pia protoko aijafuatwa kikamilifu zinatakiwa ziwe gari si chini ya 25
   
 19. m

  mlagha Member

  #19
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani Mhe Rais si kaama mwenyekiti wa TLP ama NCCR ambao hawahitaji escort. Rais wa nchi hawezi kukaa kwenye magari yote. Ila ana wasaidizi wake na vyombo vya ulinzi na usalama. Inaonekana wewe hujaona msafara wa obama na marais wengine
   
 20. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndo maana wengine hawaelewi kwanini tz ni nchi maskini. Wingi wa VX V8 barabarani ili hali yule askari aliyeshikilia bunduki kwenye msafari mawazo kibao - mtoto wake kafaulu kwenda st Kayumba na walimu hakuna, mke wake mja mzito yupo mwananyamala na dk amegoma kumfanyia operation kisa hakuna umeme au glovs hakuna; na yeye mwenyewe solidier mshiko wake hajalipwa sababu sei-kali haina fezwa; mnyororo ni mrefu.
  Je hapo pana usalama ama mfano wa usalama.
  Tafakari
   
Loading...