Msafara wa Rais Kikwete wazuia kwa muda Ubungo-rombo

Nkwesa Makambo

JF-Expert Member
Aug 26, 2011
4,763
1,314
nilikuwa barabara ya morogoro nikitokea kimara, kundi la vijana walijipanga barabarani na kuzuia msafara wa mh. Rais.
Sikuweza kujua Madai ya lile kundi, mwenye taarifa zaidi juu ya madai ya vijana atujuze...
 
Vichaa hata misikitini, makanisani, madarasani na mahekaluni wapo sembuse JF !
 
Nashindwa jina la kukupa sabu nikisema mjinga naona bado ndogo, haiwezekani uwe kimara palipo tukio halafu unakuja humu kutuuliza wakati ndo mwenye stori, ungeuliza huko uje hapa na taarifa, viupi hukuona hata mabango yao angalau ukaona kwamba ndo madai kama hayo yote hakuna kaa kimya.
 
huo mmea hapo kwenye avatar yako umeufanyia kazi nni?
wewe ndo upo karibu na tukio-lete habari au uliza hapo then tujuze sisi wengine
 
Mmnh, mbona facts zako hazijitoshelez mkuu. Wakat msafara unazuiwa wewe ulipitaje? Ulijuaje kuwa msafara umezuiwa na vijana kama hujaona? Mkuu jifunze kuleta hoja na habari zinazo pimika.
 
Hata Mimi nikiwa maeneo hayo nikielekea ubungo nilikuta kundi Hilo ambapo mheshimiwa alishuka na kubadili gari, nilichoona na mahangaiko ya wanausalama, hakukuwa na Bango lolote zaidi ya kuona mmoja wa vijana hao akiwa amshikilia kofia ngumu ya waendesha pikipiki akiwa anaipunga hewani. Sikuweza kushuka kwenye kamkoko kangu kwa uoga wa kuibiwa vipawa windo vyangi. Nami ninashauku ya kujua kilichosababisha lile kundi na walijuaje mheshimiwa atapita muda huo ?
 
WanaJF bwana cjui mkoje, mtu anawapa hint ya kilichotokea leo ambacho alikiona akipita, mnamjia juuuu.......... kuweni wastaarabu. Pole Nkwesa Makambo
 
Huenda kwa vile wanampenda sana walitaka kumpopoa kama alivyofanyiwa Mbeya. Who knows?
 
yeah nilipita eneo la tukio pikipiki ya mwongoza msafara ilianguka hivyo kulazimu msafara kusimama kwa muda na trafic police aliyepata ajali kuwekwa kwenye ambulance kuwahishwa hosipital
inasemekana rais alikuwa anaenda kimara baruti kwenye msiba wa dereva wa first lady
 
nilikuwa barabara ya morogoro nikitokea kimara, kundi la vijana walijipanga barabarani na kuzuia msafara wa mh. Rais.
Sikuweza kujua Madai ya lile kundi, mwenye taarifa zaidi juu ya madai ya vijana atujuze...
Nkwesa Makambo = mvuta bangi!! kwa wale wanaojua Kinyakyusa!
 
Mheshimiwa hakuzuiwa na vijana, ila ni kuwa muongoza msafara afisa wa polisi aliekuwa akiendesha pikipiki alipata ajali na kusababisha msafara wa Mh. kusimama na kutoa msaada kwa mhanga wa ajali, na kilichotokea ni kuwa Mh. alihakikisha majeruhia anapatiwa huduma ya kwanza na kukimbizwa hospital na gari la wagonjwa ndipo alipoendelea na safari zake Uswazi.
Upelike Nkwesa Makambo gwa mwakaleli?????
 
Back
Top Bottom