Msafara wa Pinda wazua jambo Iringa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msafara wa Pinda wazua jambo Iringa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bobby, Jun 15, 2009.

 1. B

  Bobby JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Msafara wa Pinda wazua jambo Iringa
  • Atumia ndege mbili ikiwamo ya kukodi

  na Francis Godwin, Iringa

  ZIARA ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mkoani Iringa imezua maswali mengi kuliko majibu kwa wakazi wa Mkoa wa Iringa, baada ya ndege mbili kutua katika Uwanja wa Ndege wa Nduli huku magari zaidi ya 57 yakishiriki katika msafara huo na barabara kufungwa kwa zaidi ya saa tano kwa ajili ya kusubiri msafara wake kupita.

  Mbali ya ratiba ya ziara ya Waziri Mkuu kubadilishwa mara mbili baada ya awali viongozi na waandishi wa habari kupewa ratiba iliyowataka kukutana ofisi ya mkuu wa mkoa majira ya saa 2:30 asubuhi, ratiba hiyo ilibadilishwa na kuwa saa 1:30 kwa ajili ya kwenda Uwanja wa Ndege wa Nduli kwa mapokezi.

  Hata hivyo, moja ya mambo ambayo baadhi ya watu waliofika kumpokea kiongozi huyo walionyesha kuhoji uwanjani hapo ni wingi wa magari, licha ya waziri mkuu kuwa mstari wa mbele kupinga kwa nguvu zote matumizi mabaya ya fedha za serikali, ikiwa ni pamoja na kununua mashangingi.

  Kitendo cha msafara wake kuwa na ndege mbili, ikiwamo ndege ya serikali iliyombeba na timu yake pamoja na ndege ya kukodi kutoka nchini Kenya yenye namba za usajili 540 FLY AVITION ambayo ilitumiwa na wataalamu mbali mbali, wakiwamo waandishi wa habari na wataalamu kutoka Wizara ya Miundombinu wakiongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Omari Chambo.

  Msafara wa Pinda ambao umeonyesha kuwa ni wa kihistoria ndani ya Mkoa wa Iringa uliondoka katika Uwanja wa Ndege wa Nduli majira ya saa 4:10 asubuhi kuelekea Ikulu ndogo kabla ya kuanza safari ya kuelekea Kijiji cha Mazombe, Wilaya ya Kilolo kwa ajili ya uzinduzi wa ukarabati wa barabara yenye urefu wa kilomita 150 kutoka Iyovi hadi Iringa.

  Kwa muda wote huo kabla na wakati wa msafara wa waziri mkuu ukipita, mabasi ya abiria na magari yote yalikuwa yamezuiliwa kupita kwa muda wa zaidi ya saa tano, wakisubiri kumalizika kwa shughuli za uzinduzi wa barabara hiyo zilizokuwa zikifanyika pembezoni mwa barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam.

  Pamoja na msafara wa waziri mkuu kutoka Uwanja wa Ndege wa Nduli kuwa na magari 54, yakiwemo ya watu binafsi, wabunge na viongozi wa vyama vya kisiasa, bado idadi ya magari ilionyesha kufikia 84 katika eneo la Mazombe, kwenye uzinduzi huo, baada ya magari mengine kutangulia katika eneo la uzinduzi kabla ya msafara wa waziri mkuu kufika.  Huu mzee alipochaguliwa kwenye utambulisho wake alisema yeye ni mtoto wa mkulima. Watu wengi nikiwemo tulihisi kwamba utendaji wake ungekuwa tofauti na possibly usio na gharama kubwa. Lakini mambo yake imekuwa ni kinyume kabisa.

  Ziara zake nyingi ikiwemo ya Morogoro zinatugharimu pesa zetu nyingi taxpayers. Anyway binafsi sioni logic ya kutumia gharama zote hizo kuzindua ujenzi wa km 150 za barabara, sielewi kwenye kuifungua pesa ngapi zitatumika. Juzi boss wa huyu mzee ametangaza stimulus plan ya kibongobongo ambayo ina maswali mengi kuliko majibu.

  Ushauri wangu ni kwamba wasiishie kwenye stimulus plan tu wapunguze pia gharama zisizo za lazima kama hii misafara ya kizamani kama hii katika credit crunch tuliyonayo. Maskini ambao ndio tunaoendesha serikali kwa kodi zetu mnatuonea jamani iweni na huruma kidogo.
   
 2. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nani anagharimia gharama za safari kama hiyo?
   
 3. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Au ni maandalizi ya uchaguzi wa 2010?
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sio muda mrefu na yeye ataishia kuwa fisadi. Mtu ukianza ku enjoy raha za utajiri ni ngumu sana kupona madhara yatokanyo na njia nyingi zisizo halali zinazotumika kuusaka huo utajiri.

  Pinda achana na hayo magari na misururu isiyo na maana yoyote. Muhimu ni kuchapa kazi na kutimiza wajibu wako. Misururu yote hiyo ni ulaji wa watu.
   
 5. L

  Lyambaa Member

  #5
  Jun 15, 2009
  Joined: Dec 17, 2007
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  "Pamoja na msafara wa waziri mkuu kutoka Uwanja wa Ndege wa Nduli kuwa na magari 54, yakiwemo ya watu binafsi, wabunge na viongozi wa vyama vya kisiasa, bado idadi ya magari ilionyesha kufikia 84 katika eneo la Mazombe, kwenye uzinduzi huo, baada ya magari mengine kutangulia katika eneo la uzinduzi kabla ya msafara wa waziri mkuu kufika."

  Tatizo ni wingi wa magari ya serikali au uwingi wa magari kwa ujumla? Magari ya serikali yalikuwa mangapi? Hao wengine waliokuja kwa hiari yao,walitakiwa kuja kwa miguu?Je,hizo ndege kila moja ina uwezo wa kubeba watu wangapi? ujue kiwanja cha Iringa zinatua ndege ndogo tu. Je, huyo balozi na watu wake walikuja kwa ndege? Ipi? Kati ya hizo mbili au ilikuwepo nyingine ya tatu?

  Tujaribu kuangalia kitu kwa kina badala ya kulaumu na kushabikia juu juu. Maana hapa imechukuliwa tu hiyo idadi ya magari kwa ujumla. Aliyeleta hiyo taarifa angefafanua vizuri kuhusu hiyo idadi ya magari.
   
 6. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  U make the mistake of assuming that he is the one organizing all this! Wakati kunawatu wanataka sifa chini yake huko. THe PM does not decide the number of cars on his motorcade ama wafunge barabara for how long..Mambo ya utoto wa mkulima ni irrelevant here.
   
 7. b

  babalynn Member

  #7
  Jun 15, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata kama si yeye ali-organise hayo, je alikemea alipoona hiyo situation?
   
 8. c

  cesc Senior Member

  #8
  Jun 15, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Msitake kuumiza saaaana vichwa vyenu...serikali ipo busy na kuharakisha maendeleo kwa kila mtanzania..hiii ndio ari mpya..na kasi mpya.....
   
 9. Mike-Austin

  Mike-Austin Member

  #9
  Jun 15, 2009
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulitaka akemee kwa kufanyaje?...the key issue ni "kwa kiasi gani yamefanyika matumizi mabaya na/au yasiyo ya lazima katika msafara huu?",hoja ya idadi ya magari kuwa mengi pasipo kusema ni ya Serikali au watu binafsi unapotosha umma. Tambua PM anawapenzi wengi kuliko waliohudhuria harusi yako, so wapo wengi wenye mapenzi mema na nia njema kusifu ufunguzi wa barabara hiyo.

  No fact, no right to talk
   
 10. Offish

  Offish Senior Member

  #10
  Jun 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pinda ni walewale tu kwani kapinda siku nyingi. Anamtetea fisadi mmoja anayerudisha nyuma maendeleo ya jiji la Mwanza ndio maana akauita uwanja wa Nyamagana kichaka na kutaka kiuzwe mara moja badala ya kukijenga!
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kazi kweli kweli niwapeni dodoso?
  Viongozi wetu ni watu wa lugha gongana anacho ongea jukwaani wewe fikiria opposite yake ndo jibu lake la sivyo mtaishia kuumiza vichwa tu bila majibu.
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nani aliona msafara wa Pinda wa wiki 2 zilizo pita wakati akiwa mjini Arusha kuchangisha pesa sijui za Kanisa gani lile ? Alitoka kupumzika Ikulu akawa anaenda kula maraha pale Kibo Palace uliza alikuwa na magari mangapi mbele na nyumba yake.Pinda na misafara mirefu ni sehemu ya utendaji wake ,hajali sana maana wenzake wanakula tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
   
 13. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  katika misafara kama hii ukienda ofisi za serikali unakuta nyingi zimefungwa na hakuna wa kutoa huduma, DC, DED, DGO,DNRO, na wengine wengine wengi tu na cha kushangaza unakuta watu waetoka halmashauri moja ya wilaya na kila mtu anaenda na gari lake while they could comfortably fit in one shangingi. hapa ndipo misafara inakuwa mikubwa mnaketi kwenye traffic mpaka basi. na kwa jinsi matraffic wetu walivyo waoga sijui wanaona magari yakipita 10 min before barabara itahama?

  kwa nini wasipange mikakati na kuwa na mawasilino ya karibu? wengine wetu hakuna kulala we have to work and we dont have time to wait barabarani hata kwa nusu saa
   
 14. b

  babalynn Member

  #14
  Jun 15, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 21
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenyewe umesema No fact No right to talk, wewe harusi yangu ulijua ilikuwa na watu wangapi?
   
 15. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,281
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Jamaa amekosa safari za nje naona kaamua na yeye kufanya kama President
   
 16. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2009
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mwacheni mheshimiwa ainjoi,yeye "si mwanasiasa hata kidogo"!!!
  hahahaha...hahahaha...hahahaha..
  yeye ni mtendaji tu,hataki longolongo wala nini...
  wakati wametoka kutusomea bajeti butu kule bungeni,bajeti ambayo haina mpango wowote,wao wanaendelea kutumia expenses kibao unnecessarily...this is bulshit..how can it be?magari yote hayo ya nini?kwani nani hajui kama yeye ni PM wa bongo? anamwonyesha nani sasa, hizo si sifa za kijinga hizo? huo msafara wote unapata wapi hela ya mafuta na msosi? wasitufanye sisi wapumbavu hawa!!!wasione tumetulia kimya..tuna mind kinoma ujinga wanaoufanya katika nchi hii..
   
 17. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni kweli mwandishi wa makala ile hakufafanua vizuri. Ila kwa tulioona magari ya Serikali yalikuwa 36. Balozi alikuja kwa gari akitokea Dar. Alikuwa na gari moja tu. Ndege inayoitwa Fly 540 Aviation ambayo ilikodiwa kutoka Kenya ilibeba wataalamu kutoka Wizara ya Miundo Mbinu akiwemo Katibu Mkuu wake.
   
 18. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ili tusimuelewe vibaya ni vema PM akatoa statement kuhusu hili. Sidhani kama yeye aliruhusu msafara wa magari mengi kiasi hiki, bila shaka wasaidizi wake sio watu makini. Lakini trafiki wetu nao wana matatizo makubwa sana. Huu mtindo wa kuzuia magari kwa muda mrefu unakera sana. Kuna siku nilichelewa ndege baada ya magari kuzuiwa kwa zaidi ya one hour wakati kiongozi (sijui alikuwa huyu au mwingine) pengine alikuwa hata hajaanza kujiandaa kuondoka huko alikokuwa. Huu ni upuuzi!
   
 19. A

  August JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  na hii ndege toka kenya sio ya swahiba wetu ra kweli maana nataka kujimlisha na ile waliotumia boyz to men 1995 walipo wasilisha form za kugombea urahisi.
   
 20. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Jamani huyu Mizengo Kayanza Peter Pinda mlitaka afanyeje?? Mnajua jinsi bosi wake anavyotanua?? Kumbukeni ameshapiga mkwara MDA's zote kufanya semina na kongamano mpaka zipate kibari kutoka kwake (ofisi yake), je zimetii? Unajua kilichotokea baada ya hapo??? Mnakumbuka (kwa waliohudhuria) katika harusi ya Ridhiwani pale ubungo plaza? Kulikuwa na zaidi ya magari 120 ya serikali, sasa mjiulize kama hiyo tu ni harusi ambayo ni shughuli binafsi, vipi ufunguzi wa barabara? Achilia mbali hata kama ni barabara ya kilomita 2 na ya kiwango cha changarawe!!

  Soma signature yangu hapa chini, kisha tafakari!!
   
Loading...