Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa wapata ajali Meatu

Online Pastor

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,948
1,515
Msafara wa Ndugu Kheri James Denice wapata ajali wilayani Meatu baada ya gari ya polisi kuchomoka tairi hivyo kuziba njia na magari ya nyuma kupandiana barabarani.

More updates:
Majeruhi wamefikia watatu wamepelekwa hospitali ya Mwandoya kwa huduma ya afya na gari ya basi ya Rombo imepata ajali baada ya kuigonga gari ya madiwani kwa nyuma.

Ajali imetokea mpakani mwa wilaya za Meatu na Itilima katika kijiji cha Kisesa.
Wakuu wa wilaya za Meatu na Itilima wapo eneo la ajali kutoa msaada stahiki.

Msafara umeendelea baada ya majeruhi kufikishwa Mwandoya.

Shukrani zimwendee dereva wa basi la Rombo kwa kuchepusha gari nje ya barabara ili kulikwepa gari la polisi

Pia tunaishukuru Kamati ya Ulinzi ya Wilaya ya Meatu kwa uharaka wake wa kulishughurikia tukio hili

Madiwani waliojeruhiwa ni kata za Imalaseko, Mwasengera,Tindabuligi na Ngoboko

Sad News:
Mhe Diwani wa Tindabuligi Mhe Mahega ameiaga dunia muda huu.
Rest in Peace
 
Leta taarifa iliyokamilika,kama idadi ya majeruhi,marehemu na uharibifu wowote kama upo
 
Mpaka sasa kuna majeruhi wako watatu,na wote wakiwa ni madiwani wa wilaya ya meatu na wameshakimbiizwa hospitali ya Mwandoya
 
Hii chuki inazidi kuwa kubwa na inaendelea kukua kila uchao. Umoja wetu unazidi kupotea kutokana na dhulma na visasi kwa wananchi. Mkuu wa kaya ana kazi nzito ya kurudisha upendo na amani miongoni mwa watanzania.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom