Msafara Wa Mamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msafara Wa Mamba

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Nov 13, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Miaka 15 ya mfumo wa vyama vingi Tanzania. Mengi tumeyaona, lakini yaliyotokea juzi na jana kule Dodoma yamenipa funzo kubwa kwamba upinzani Tanzania umejaa waganga njaa na wanafiki wanaoweza kuonesha usaliti wao mchana kweupe.

  Nilistuka sana niliposikia kuwa kumeundwa kitu kinachoitwa 'minority opposition'. Hata wakati wa upigaji kura matokeo yalionesha pasipo na shaka kuwa siyo CCM peke yake wanaokichukia Chadema, bali hata vyama vingine vya upinzani.

  Hivi kosa la Chadema ni nini? Mbona silioni?

  Au kwa kuwa safari hii kimevuna wabunge hata kusiko kuwa na Wachaga?

  Kwamba wazazi wangu CCM damu amekipigia kura Chadema(na wameapa hawatapigia kura CCM tena)?

  Kwamba kwa nini Chadema kimeanza kupigiwa kura hata na wasukuma badala ya kupigiwa kura na wachaga kama ilivyokuwa zamani?

  Kwamba Chadema kimewaamsha Watanzania kwa kuwaondolea fikra pandikizi za CCM?

  Kwamba Chadema kimesheheni(na kitaendeleakusheheni) wanachama na wafuasi wasomi wa vyuo vikuu?

  Kuna maswali mengi ninayojiuliza kuhusu chuki kwa chama hiki makini.

  Somo moja nililopata baa da ya harakati za jana na juzi:

  Vyama vya upinzani Tanzania havina tofauti na Msafara wa mamba ambamo Kenge na Mijusi huwa hawakosi.

  Viva Chadema. Stand on Your Feet.

  Tuko Nyuma Yenu.

  Change is Inevitable. It's just a matter of time.
   
 2. n

  ngoko JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Mkuu mtu akionesha juhudi za kweli kukunyang'anya ulichonacho mkononi wakati unakitaka hakika utamzulia mengi, ndicho kinachotokea.
   
 3. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pipoooooooooooooos pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...