Msafara wa makamu wa rais wa Tanzania wapata ajali ya gari mombo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
akiwa anatoka korogwe msafara wake umepata ajali baada ya gari la polisi lililokuwa linaongoza msafara kushindwa kukata kona kwenye milima na kutumbukia kwenye shimo. bado haijajulikana kama kuna mtu amekufa. magari yalikuwa kwenye kasi kubwa. wengi wamejeruhiwa vibaya. source itv. Mia
 
Nimeikuta mwishoni kwa TV. Mwenye habari kamili atujuze.
Source: BREAKING NEWS, ITV
 
Source radio one.
Msafara wa Dr Ghalib Bilali umepata ajali maeneo ya mombo-Korogwe baada ya gari lililokuwa likiongoza msafara kushindwa kumudu kona ya mwisho kabisa ya lushoto kuingia mombo na kuingia bondeni. Ni gari la maaskari.
Msafara umeendelea na safari kuelekea Tanga na hakuna gari lingine ilohusika na ajali zaidi ya hilo
Nawakilisha
 
Looh..pole zao...
Inawezekana watapata akili na kutengeneza mazingira mazuri ya barabara zetu!
Na mgomo wa madr mh!!!
 
vipi makamu wa rais kapona au tusahau'bora yawakute wenyewe wapungue kidogo
 
Mungu anusuru maisha ya viongozi wetu..asipotee hata mmoja...
Katika jina la YESU ninaomba...
AMEN!
 
Mungu awanusuru wote.

Ila naomba nitoe rai. msafara wa viongozi wetu hasa wa rais waachane na fikra potofu kwamba mwendo wa kasi unaimarisha 'usalama' wa kiongozi. Ukiangalia hawa watu wanavyoendesha utadhani ni mashindano ya formular 1! Kama ni usalama kinachotakiwa ni kuwa na gari-bullet/bomb proof. Ile beast ya Obama ina mwendo wa kinyonga. Hapa wanafikiri ukikimbiza ndio unaepusha hatari! hebu tujifunze.
 
Ulitakiwa useme mkuu kabisa ndiyo hana faida huyu anaweza hata kutufaa kwenye ma Uranium haya yanayochimbwa TZ maana ndiyo fani yake!..

Avt yako imenipa birudani mno! wapi huko, Makka Saudia???
 
Back
Top Bottom