Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,888
Makamba na Tambwe na wapambe wao majuzi walipata adha na adhabu toka kwa wananchi wa Singida kwa kuitwa waongo na kumwagiwa mchanga wakati wanaondoka toka maeneo ya mikutano yao. Hivi karibuni Tambwe na Makamba na CCM nzima wamekuwa wakihaha kila kona ya Nchi kujaribu kuzima sumu iliyo mwagwa kwa wananchi juu ya kuibiwa mali zao .
Walikuwa wakiondoka ambapo wananchi walisema mnatudanganya maisha ni magumu na hatuwataki wakaanza kuwamwagia mchanga ndipo FFU walipofika na kuokoa jahazi hilo. Katika kutapata kwa CCM wamekuwa wakifanya mabadiliko kwa kuwahamisha makatibu wao wa Chama ambao ni wasemaji sana na kuwapeleka maeneo ambayo CCM ina wakati mgumu ikiwamo Pwani ambako Katibu wao Sofia Kishindo kahamishiwa hapo toka Mbarari. Pwanim imekuwa moto baada ya wazazi na vijana kuhoji uhalali wa wao kukosa Elimu na kuuza vitu vidogo vidgo na kuishia katika kuwa madereva na utingo wa magari .
CCM inahaha baada ya kugundua kwamba sasa watu wamechoka na wanaelewa vya kutosha .