Msafara wa kikwete washambuliwa bagamoyo:

MWANAWAVITTO

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
258
220
MSAFARA wa Rais Jakaya Kikwete uliokuwa ukielekea Bagamoyo jana ulilazimika kusimama kwa muda baada ya kuzuka kwa vurugu kubwa za kurushiwa mawe katika eneo la Namanga Tegeta Manispaa ya Kinondoni jiji la Dar es salaam.Wakazi wa eneo hilo walifunga barabara kwa muda, na hivyo kuzuia msafara wa Rais Kikwete kwa kile walichodai aweze kuona namna matajiri wanavyotumia uwezo wao wa kifedha kuwanyanyasa raia wanyonge.Vurugu hizo zilisababisha mabaunsa wawili kujeruhiwa vibaya na wananchi na wamelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu zaidi.Vurugu hizo zilizodumu kwa zaidiya saa mbili, zilitokana na kitendo cha watu (mabaunsa) wanaoaminika kukodiwa na mmiliki wa kituo cha mafuta cha GAPCO aliyetajwa kwa jina Hemed Salum, kuvunja nyumba zao na mfanyabiashara huyo.Hata hivyo, msafara huo wa Rais uliweza kuendelea baada ya askari wengi kumwagwa na kuanza kuwatawanya wananchi waliokuwa na hasira.Wakiongea kwa hasira, wananchi hao walidai kuchoka na vitendo wanavyotendewa na baadhi ya wawekezaji.“Watu wenye pesa wanafanya kilawanaloliona kuwa linawafaa bila hata kujali sheria za nchi, sasa sisiwananchi tulifanya makusudi ili Rais aone mambo tunayofanyiwa na hawa wawekezaji atusaidie, lakini kinyume chake tunapewa bakora,” alisema mwananchi mmoja ambaye hakupenda kutajwa jina lake.Watu waliobomolewa nyumba zao wamesema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha mmiliki wa kituo hicho kuwavunjia nyumba zao akidai kuwa wamejenga kwenye eneo lake.“Hili eneo ni letu tunalimiki kihalali, kwani tuliachiwa urithi nababa yetu na sisi tuko watoto kumi, kila mmoja alipewa eneo lake tukajenga, na eneo la barabarani halikuwa letu hivyo aliuziwa yeye (Salum) na mtu mwingine akajenga kituo cha mafuta.“Kinyume chake ametafuta nyaraka za kugushi na kuanza kudai kuwa sisi tunaishi katika eneo lake tuondoke tumwachie, lakini hakuna mtu yeyote asiyejua kwamba eneo hili ni letu na tumeachiwa urithi na baba yetu,” alisema Fikiri Saidi mmoja wa waliobomolewa nyumba huku akitokwa na machozi.Fikiri aliongeza kwamba kabla ya tukio hilo siku mbili zilizopita, mmiliki huyo aliwafuata nyumbanikwao kwa lengo la kutaka wamuuzie eneo hilo kwa shilingi milioni 100 ili wagawane lakini walikataa, ndipo akatoa vitisho akiwambia kuwa, kwa kuwa wamekataa pesa hizo atawapa wanaozihitaji ili wabomoe na hawataambulia kitu chochote.Kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alisemapolisi wanamshikilia mmiliki huyo kwa kosa la kujichukulia hatua mkononi na kuwavunjia wakazi hao nyumba na kusababisha upotevu wa mali.Hata hivyo, Kenyela alisema polisi watafanya msako wa watu waliohusika kupopoa mawe msafara huo, huku akiwataka wakazi hao kuwa watulivu wakatiserikali ikiangalia namna ya kuwatafutia hifadhi ya muda.Watu walioathirika na tukio hilo niFikiri Saidi, Rashid Said, Farida Said na Ally Mkwandu, wengine ni Shabani Said, Kassim Said, Sijali Said Rajab Said na Waziri Rashid, ambapo inakadiriwa kuwa thamani ya nyumba na mali zilizoharibiwa inafikia zaidi ya sh milioni 300.
 

BANA BANA.... SASA ARDHI NI DIAMOND AU ZAIDI HAPA TANZANIA


Poleni sana wakazi wa Tegeta Namanga kwa tukio lilotokea jana la kuvunjiwa makazi yenu kwa uonevu mkubwa....,
ni laana kubwa kutaka kupora ardhi ya mtu.

ARDHI NI DIAMOND HAPA TANZANIA, hakuna ubishi kwa hilo...,
Tatizo linakuja Je, Govt ya CCM haitaki kukubali ya kwamba hata Watanzania wa kawaida wanaipenda hiyo DIAMOND..?, ni lazima walitambue hilo. Watanzania wote ni sawa na wana haki sawa pia.
Wao wanafikiri ni wao tuu na jamaa zao wawekezaji fake ndiyo wana hakimiliki ya kuimiliki Diamond ya Tanzania....?? aaahah ahah laaasha haiwezekani hata kidogo hilo jambo kutokea!
kila mtanzania anapenda kuimiliki na kujinafasi diamond yake kwa wakati wake, coz ni haki yake ya msingi.

Hasira za Watanzania hazitaisha kwa mambo ya ajabu yakiendelea kutokea kuhusu kaadhia ya Ardhi.

Elimu kuhusu sheria za Ardhi ni muhimu sana kwa Watanzania wote kuzijua kama umuhimu wa Matumizi ya cond........uu dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi!
Tatizo la dhuluma ya Ardhi ni janga kubwa!
Tuikubali kuporwa diamond (Ardhi) yetu kifisadi au kinyemela, ni lazima kwanza wahusika wahusishwe na kuridhia utaratibu husika.
 
Fujo hazikuhusu msafara wa rais, ilitokea tu msafara ulikuwa unapita wakati fujo zikiendelea. Acheni fitna na majungu.
 
Uongo mwingine hauna hata maana, eti namanga, tegeta ni bagamoyo. kwi kwi kwi teh teh teh !

Nani alioushambulia? kama si uongo huu ni nini?
 
Back
Top Bottom