Msabaha katendewa haki?

mtizedi

JF-Expert Member
Jan 31, 2008
360
1
Hivi Ibrahimu msabaha katendewa haki kwa asilimia zote?
Maana amelalamika kuwa mfumo wa utendaji kazi wa serikali kwa ujumla wake ndio umemponza na ameomba uangaliwe upya siku za usoni
 
Haki imetendeka maana 80% ya sakata la Richmond ilikuwa facilitated wakati yeye ndio waziri wa nishati na madini!

Ivi huyu Msabaha kama anaonewa ni kwa nini hakusema kabla na subiri mpaka awe kafara?? Does it need him to have PHD ili awe na uwezo wa kuona matatizo ambayo angeyapata in future kwa kutenda hayo anayosema mfumo ulimuelekeza???

Msabaha anatapatapa tu he's playing BLAME GAME, na hata katika ripoti nafikiri kuna recommendation juu ya utendaji na kama watafanya kulingana na tume basi tutegemee mambo mazuri katika utendaji!!!

Haki imetendeka na naiomba hii haki iende PCCB, kwa AG, Katibu Mkuu wizara ya fedha na wengine wote ambao wako implicated... warudishe hela za walipa kodi!!

maisha magumu Tanzania ati!!!
 
Alikuwa wapi kwa muda wa miaka miwili asiyaseme hayo, au ameonyesha wapi kuwa alikwisha lalamikia hilo lakini halikusikilizwa? Tatizo ni kutokuelewa kuwa uwaziri si kupokea tu amri kutoka kwa waziri mkuu au rais. Serikali huendeshwa kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na zinazoendelea kuwekwa kila siku bungeni. Kama alihisi au aliona kuna mfumo ambao kiutendaji utafikia kunja sheria basi ilibidi achukuwe hatua za mapema kutokuruhusu uvunjaji wa sheria. Mengine ni hekaya...
 
tatizo la kufanya kazi kwa mambo ya YES kwa mkuu wako just kwa sababu unataka kulinda kazi yako huku maslahi ya nchi nyuma....alijua kabisa ile ni fraud ila kulinda kibarua chake akakubali kushiriki,imefika time sasa watu wafanye kazi kwa haki bila kuogopa mtu la sivyo nao hawatufai tuu,hasara imetokea chini ya uangalizi wake sasa anataka kutuambia nini? aende zake huko
 
tatizo la kufanya kazi kwa mambo ya YES kwa mkuu wako just kwa sababu unataka kulinda kazi yako huku maslahi ya nchi nyuma....alijua kabisa ile ni fraud ila kulinda kibarua chake akakubali kushiriki,imefika time sasa watu wafanye kazi kwa haki bila kuogopa mtu la sivyo nao hawatufai tuu,hasara imetokea chini ya uangalizi wake sasa anataka kutuambia nini? aende zake huko

Koba
Spot on! Aliapishwa kulinda na kutetea katiba ya nchi. Kama Msabaha aliona analazimishwa kufanya kazi nje ya maadili, alikuwa na nafasi ya kumweleza Raisi au kujiuzulu. Hakufanya hivyo! Sasa Bangusilo analia nini. Hastahili huruma!
 
ndio maana ninasema watu kama dr. Idrisa wa tanesco ni watu makini sana.
alipoona mambo hayaendi kama inavyopaswa aliamua kujiuzulu hadi rais alipokataa kujiuzulu kwake na kwa heshima ya rais akaamua kurudi kazini.
nadhani msabaha alitakiwa atende kama huyu
 
Back
Top Bottom