Msanii wako bora wa mwaka 2021 kwenye Bongo Flavour

Wasanii wa Usafini WOTE nahisi huu mwaka wamepiga sana Hela pia brand yao imepiga hatua

Pia KoNDE Ametuma salama kwa watanzania kwamba yupo sana na ni msanii tishio hasa kwenye suala la ushindani wa kimziki namuona mbali sana dogo

●BRAND BORA NI WCB MWAKA HUU
●HARMONIZE AMESIKIKA SANA REDIO KWA VIBAO VYAKE VIKALI HASA MWISHO MWA MWAKA

Nawasilisha
 
Ali Kiba, WcB tafadhali msinipopoe sina utimu, naona wengi wenu mmeside kwa Marioo mwaka huu 😂

Hii naifananisha na vita ya Ballon d'or 2021 vile mashabiki wa Ronaldo walivyokuwa na muhaho, mara wawe team Lewandowski mara Jorginho mwisho wa siku mshindi ni Messi
 
Heri ya chrismas na mwaka mpya!

nianze kwa kusema mimi sio shabiki wa bongo flavour napendelea sana hip hop na jazz

lakin hapa acha nitoe hii tathimin yangu kwenye bongoflavour kwa mwaka 2021 ambao tumeacha siku chache kuumaliza

kwenye muziki wetu wa bongo flavour naona jamaa marioo amefanya vema sana mwaka wote wa 2021 sana. almost ngoma zake zote alizotoa ndani ya mwaka 2021 ni kali na zimekuwa hit songs

nikiambiwa nimtaje msanii wabongo flavour aliefanya vizuri kwa mwaka 2021 basi ningesema marioo.

kwa upande wenu jf vipi?
mbali na huyo nilie mtaja, nani unaona amefanya vizurii zaidi mwaka 2021 kwenye bongo flavour?


mtu ambaye amezingua kwa mwaka huu naona ni ray vanny.. sisemi kama hajui, ila ajawa amsha amsha kwa mwaka huu.
Super MARIOOOOOOOOOOO.
1.Bia Tam
2.For You
3.Jana kaachia bonge la dude Amor X Jovial.
 
Back
Top Bottom