Msaada

Gizzo

Member
May 8, 2008
6
0
Naomba mchango wenu wa mawazo wanajamii
kuna mdada anajirengesha kwangu ila mimi sina mpango nae
sasa jana usiku katuma sms ktk simu yangu akilalamika kwamba namtesa
ksababu najua ananipenda ndio maana namletea mapozi sasa kibaya zaidi wife ndio mtu wa kwanza kuiona sms ameniwashia moto akinituhumu kwamba nammega yule demu nimejaribu kumuelewesha hanielewi kabisa na ameshaenda kushitaki kwa wazee wangu kwamba mimi sio muaminifu ktk ndoa so jpili natakiwa ktk kikao na wazee.je waunwana mnanishaurije?
 
Acha tabia yako ya kumega nje,
kama anajilengesha number yako alipataje? na huwa unamjibuje msg zake? inaonekana una mawasiliano mazuri na huyo dada. Ngoja wazee wakakupe ushauri zaidi maana ya ndoa.
 
sasa kama unaenda kwenye kikao kuukumiwa unataka ushauri wa nini?
hivi kweli umeona lakini bado unakuwa na mwasaliano ya kugawiana simu na vimada, mshkaji hiyo ni noma sana,
umesharikoroga inabidi ulinywe
 
Naomba mchango wenu wa mawazo wanajamii
kuna mdada anajirengesha kwangu ila mimi sina mpango nae
sasa jana usiku katuma sms ktk simu yangu akilalamika kwamba namtesa
ksababu najua ananipenda ndio maana namletea mapozi sasa kibaya zaidi wife ndio mtu wa kwanza kuiona sms ameniwashia moto akinituhumu kwamba nammega yule demu nimejaribu kumuelewesha hanielewi kabisa na ameshaenda kushitaki kwa wazee wangu kwamba mimi sio muaminifu ktk ndoa so jpili natakiwa ktk kikao na wazee.je waunwana mnanishaurije?
...Kwa hapo kwenye red unajionaje we mwenyewe kwa maoni yako???....Then naweza kukushauri cha kufanya..
 
Mimi ni muaminifu 100% ndio maana hata wife cm yangu yuko huru nayo siifichi wala nini nashangaa huyo binti amepataje namba kiukweli waungwana
sijawahi kummega huyo binti
 
Ushauri gani unataka sisi tukupe,tena nahisi unamsingizia huyo dada kuwa anajilengesha kwako,aliipataje namba yako kama sio wewe mwenyewe ulimpa? we sema hivi una mazoea na huyo binti,haiwezekani tu from no where mtu aanze tu kutuma msg,siku ambayo msg imeonekana ni kwamba arobaini yako ilikuwa imefika.Umelikoroga linywe,mnapenda sana kusema wadada wanajilengesha kwenu wakati ni uongo,mnawatongoza wenyewe mnagawa namba za simu wenyewe yakiwafika ooo alijilengesha.
 
Mimi ni muaminifu 100% ndio maana hata wife cm yangu yuko huru nayo siifichi wala nini nashangaa huyo binti amepataje namba kiukweli waungwana
sijawahi kummega huyo binti


Tutaamini vipi haya unayotwambia? unataka kusema kuwa hukumpa huyo binti namba?,we kuwa wazi tu eleza kwa uwazi issue ilivyo ili watu wakupe ushauri.
 
huo ndio ukweli wangu sina haja ya kuficha kitu sasa kama naficha au naongopa kuna haja gani ya mimi kuomba ushauri?
 
huo ndio ukweli wangu sina haja ya kuficha kitu sasa kama naficha au naongopa kuna haja gani ya mimi kuomba ushauri?
Usijali kaka,Mungu ndiye huwa anajua mambo ya sirini kwani Mungu anaangalia moyo na sie wanadamu tunaangalia sura.Wewe cha kufanya nadhani uwe mpole tu kwa sababu ishatokea.Nenda kwenye kikao kama walivyokuita na endelea kuusimamia ukweli kama unavyodai.Usife moyo, hayo ni majaribu tu yatapita zaidi Mungu Mungu akuepushe na mabalaa yanayoinyemelea ndoa yako.Tafuta njia ya kumdhibitishia mkeo kuwa wewe ni mwaminifu na hayo mawasiliano na huyo dada yakate kwa njia yoyote ile.
 
Pole kaka,mkeo anatakiwa awe na imani na wewe, kwa message hiyo wala nisingekushitaki kokote. Mwanaume yeyote mwenye akili hawezi kumega nje akaruhusu kupigiwa simu wakati yeye anatumia cm na mkewe.

Hata message inaonyesha kwamba humtaki na unaleta pozi.
 
pole sana kaka mpendwa mie nimesoma hii post yake nahisi kama vile unasema ukweli tu
kwanza wadada siku hizi wanapenda sana waume za watu
nachokuomba jaribu tu kumwelewesha mkeo kwa upole zaidi mwambie hujammega huyo dada zaidi yeye ndo anakufata kama kuna kikao cha familia nenda tu na konfidensi zote na useme kweli kama hausiki na hila sakata

Kuna mtu amesema namba yako ya simu kaipataje? kupata namba ya mtu ni rahisi sana kwa dunia ya sasa ya utandawazi na kama mko karibu kikazi ,majirani na kadharika
FL1
 
Mimi ni muaminifu 100% ndio maana hata wife cm yangu yuko huru nayo siifichi wala nini nashangaa huyo binti amepataje namba kiukweli waungwana
sijawahi kummega huyo binti
weye kicheche tu....kwanini mnaoa wakti mnapenda totozi mbichi mbichi? acha hizo...
 
Huyu jamaa si kicheche wala nini mimi si mmegaji lkn mara nyingi huwa watu wanakosea kupiga simu, au sms zinakuja kwangu ziwe za wanaume huwa shwari ila km ni ya mwanamke hapo amani inapotea kabsaa, nadhani huo ni wasi wasi tu wa mapenzi km alivyoimba Stara Thomas, hata km mwanaume/mwanamke katuma sms kama hiyo na mtumaji anaonekana kulalamika kwamba mshikaji hamjali inaonekana wazi kabisa jamaa hana time naye, ila huyo dada anatafuta nafasi hapo, siku hizi jamani wadada wanapenda sana waume za watu mno, so kupata namba ni kitu kidogo sana, cha muhimu huyu mwanamke wala asingefika mpaka huko kwenye kikao, angefanya uchunguzi wake mdogo tuu angebaini nini kinaendelea hapo
 
ni tabu sana mwanamke kuweza kujiamini kumtumia msg mume wa mtu kama hujamuonesha udhaifu fulani. kama sio hivyo basi inawezekana kafanya maksudi ili kukutia kisirani na mke wako.
ushauri: kama ni kweli huna makosa wala mawasiliano na huyo mwanamke basi hudhuria kikao na elezea uaminifu wako kwa mke wako na kula kiapo kwa imani yako ili kuwatoa khofu zaidi, pia tumia kigezo cha kwamba unamruhusu mke wako kusoma meseji zako kwakuwa unajiamini. waelezee uwezekano wa huyo mwanamke kuipata namba yako bila ya kupitia kwako.

pole kaka na matatizo, nakutakia ufumbuzi mwema wa matatizo yako.

quiet
 
...shikilia msimamo huo huo!
-Deny, Deny, Deny!!!-
...ukikiri kosa umekwisha!
 
Ukiweza kujibu ni vipi huyo dame aliipata namba yako ya simu na jibu lako likawaridhisha wakubwa kwenye kikao basi huna case ya kujibu vinginevyo jiandae kwa wakati mgumu kwenye kikao.


[ame]http://www.youtube.com/watch?v=xK082mbeBZ0[/ame]
 
Back
Top Bottom