Msaada

Evarm

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
1,934
1,400
Wadau naomba mnisaidie nina tatizo moja. Tatizo lenyewe ni kutokwa na damu puani. Jana nilitembea sana juani katika kutafuta riziki na niliporudi nyumbani nikafikia kufua na kusafisha nyumba na mazingira yanayonizunguka wakati naendelea na shughuli damu zikaanza kunitoka kwa wingi sana puani. Nikaweka kitambaa karibu na pua ili isinimwagikie, baadaye nikaoga na kulala tumbo juu ndo ikatulia. Ila hii hali hunitokea endapo kama nitainama muda mrefu sana au kutembea juani. Naomba ushauri wadau je hii ni hali ya kawaida au? Na je ninaweza kutumia tiba gani ili hali hii isinitokee tena?. Nawasilisha
 
Kuna sababu nyingi zinazoweza pelekea mtu akawa anatoka damu tu puani bila kuumia (google epistaxis). Unahitaji uchunguzi wa haraka sana na ENT surgeon...kwa nimeshaona wagonjwa kadhaa ambao wamewahi kutoka damu puani na ikawa haiwezekani kustop.
 
Thank you Dr. Riwa nitaenda hospitali maana yake nimekuwa nikipuuzia na huwa hainitokei mara kwa mara ila hadi kwenye hali hizo nilizotaja pale juu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom