Msaada: Mdogo wangu yupo darasa la 6 ila jina limetoka kwenye matokeo ya darasa la 7 ikidaiwa jina lake liliuzwa

bloodsucker

Member
Mar 10, 2018
11
7
Wakuu habari zenu? Mmeshindaje?

Sasa Wakuu kuna shida kidogo nahitaji ushauri wenu kuna mdogo wangu alikuwa anasoma Arusha shule ya msingi sasa kule kulitokea shida kidogo akaamishwa shule akaletwa Ukerewe.

Wakati anaamishwa alkuwa darasa la sita lakini shuleni alipohamia Mwalimu Mkuu akakataa kumpokea mpaka arudishwe darasa la tano, basi ikawa hivyo dogo akarudi darasa la tano.

Sasa maajabu yameibuka leo baada ya matokeo kutoka dogo bado yupo darasa la sita mwakani anamaliza darasa la saba lakini jina lake limetoka kwenye matokeo kwamba amefaulu kwa daraja B.

Baada ya hapo nikafanya kuulizia marafiki wakadai Mwalimu Mkuu aliuza jina kwa mrudiaji. Sasa nahofia hatima ya mdogo wangu mwakani atakapofika darasa la saba itakuwaje?.

Kwa wanasheria ebu mnishauri nifanye nini kwa mjibu wa sheria, maana kinachoniuma ni mtu mwingine kumiliki jina la ukoo wetu.

Wanasheria na wakuu naomba kuwasilisha
 
Katoe taarifa TAKUKURU fasta.
Takukuru wadai cheti cha mtoto aliyeuziwa jina cha kuzaliwa na kiwe cha zamani maana huyo bila shaka amezaliwa kipindi hiki ambapo vyeti hutolewa mara tu ya mtoto kuzaliwa tofaut na miaka ile... Au kadi ya clinic... Pia alete cheti cha baba yake cha kuzaliwa au kitambulisho chochote kinachotambulila na serikali hapo nadhani mambo yatakuwa mswano
 
Takukuru wadai cheti cha mtoto aliyeuziwa jina cha kuzaliwa na kiwe cha zamani maana huyo bila shaka amezaliwa kipindi hiki ambapo vyeti hutolewa mara tu ya mtoto kuzaliwa tofaut na miaka ile... Au kadi ya clinic... Pia alete cheti cha baba yake cha kuzaliwa au kitambulisho chochote kinachotambulila na serikali hapo nadhani mambo yatakuwa mswano
shhkrani sana kwa ufafanuzi
 
nimereport kwa mratibu elimu wa kata. na kwa afisa elimu wa wilaya na imeonekana kuna mchezo haram umechezwa. Jumatano hii ndo tunaenda kujua hatima ya hili suala na mwalimu mkuu atachukuliwa hatua gani
Okay sawa,ila nenda kimya kimya Takukuru bila hao uliowaambia kujua,ukiona wanazingua utakuwa na nafasi nzuri kusaidiwa
 
Dah! Pole sana mkuu! Fuatilia kwa makini bila kupanick.

Kwanza fanya kufahamu majina hayo ya mdogo wako yameingia lini kwenye register ya hiyo shule.

Pili, fanya kumfahamu kama inawezekana huyo mwenye jina la mdogo wako.

Pia, kama inawezekana, fuatilia wanafunzi wa darasa waliohitim kupata taarifa za hapa na pale. Yote haya yatakupatia nguvu za kusimama.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom