BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 4,041
- 10,463
Ni hali ambayo sio Mimi tu inanitokea bali wengi wetu. Ni jinsi ya kufanya maamuzi tuseme unajikuta una chaguzi mbili kwa mfano upo kwenye mawazo ya kujenga Nyumba au kununua gari unaweza kuwaza kununua gari ila baada ya muda ukajiona ulifanya maamuzi ya kipuuzi ni heri ujenge nyumba lakini ukikaa tena baada ya muda flani mawazo yanabadilika unawaza kununua gari na hii hali inakuwa aina mwisho unaweza kufanya kimoja wapo na bado ukaendelea kujilaumu kwa nini umefanya kitu flani badala ya kitu kingine. Wataalamu wa elimu ya akili naombeni msaada jinsi ya kukabiliana na hii hali maana madhara yake ni kujikuta ufanyi chochote kwenye muda unaostahili.