Habari,
Mimi na familia yetu tunategemea kuanzisha kampuni ya biashara mbali mbali hapo mwakani kwa uweza wake Mungu, je tunaweza kutumia jina gani la biashara?
ni chaguo lako...... ila itabidi jina hilo liwe halijasajiliwa tayari.... ila chochote kile ni ruksa..... Ila nashauri Jina lihusiane na biashara yenu, liwe proffessional na sio refu sana liwe liwe a bit cool..... mfano (Ebay;Mtv Mwanahawa & Sons, Wataalamu; etc) na sio the likes of (Wachakachuaji; xytvsbris company;Yahoo; Amazon hata kulitamka inakuwa shida...... What I mean ni kwamba jina lako liwe linahusiana na biashara yako....
Nakubaliana na Cronique na VoR, unapofikiri jina la biashara hakikisha linaendana na biashara unayofanya, cha kuzingatia ni jina liwe fupi na rahisi kwa wateja kuweka kumbukumbu. Kwa vile baishara ni ya kifamilia inaweza kuwa busara kama mutaweza kuingiza jina la ukoo mfano Tesha Suppliers, KataviS, Michuzi Enterprises and so on.
Vitu vengine vya kuzingatia ni soko lako linalenga wapi? kimataifa, kimkoa ama kitaifa? Endapo ni kimataifa jaribu kufanya research ili kuepuka kukopia Domain name ya biashara za watu.
Jina lisiwe lenye matusi, mfano nyinyi ni akina To*mba lakini jina kama T*mba Care Ltd halitofaa kwenye hii biashara.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.