Msaada wenu unhitajika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wenu unhitajika!

Discussion in 'JF Doctor' started by Evarm, Sep 23, 2011.

 1. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Nina rafiki yangu wa kike ambaye ana tatizo la muda mrefu sana linalomsumbua ambalo ni akikaribia siku zake za hedhi hupata pimples ambazo baada ya kumaliza hiyo hedhi humuacha na alama ambazo huwa hazitoki yaani ni za muda mrefu. Wakati mwingine hizo pimples humtokea usoni au kifuani na pia mgongoni na hizo alama hubaki katika sehemu husika na hivyo kumfanya ashindwe hata kuvaa nguo za mabega wazi kwa ajili ya makovu ya chunusi hizo. Ninashukuru Kwa yeyote ambaye ataweza kumshauri , pia madaktari tunaomba pia mtusaidie chanzo cha hizi chunusi na jinsi ya kukabiliana nazo.
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Pole sana kaka, ukikosa msaada humu jaribu kwenda madaktari wa ngozi.
   
 3. d

  drberno Member

  #3
  Sep 24, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo tatizo huwa linasababishwa kwa asilimia kubwa na kupasuka kwa 'layer' nyembamba ya ngozi (skin) inayoitwa "acid mantle".Hii huletwa na mabadiliko ya 'hormones' yanayotokea wkt wa hedhi.
  JINSI YA KUJIKINGA: aepuke kula vyakula vyny mafuta sana(hasa ya wanyama),ale mboga za majani,matunda,anywe maji ya kutosha. Pia anaweza kupaka 'vinegar'(apple cider) usoni siku 7 kabla ya siku za hedhi yake.
  TIBA(zikishakuwa zimetokea): atumie calamine lotion wkt wa usiku au white toothpaste wkt wa usk! Asijaribu kuvitumbua hii inachangia sana ktk kuacha makovu.
   
 4. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Asante sana Dr Berno kwa ushauri mzuri.
   
 5. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160


  Asante sana, nitamshauri na hilo pia
   
 6. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pole sana mkuu, kama upo Dar, nenda pale Muhimbili Hospitali kuna Madaktari bingwa wa masuala ya ngozi wanamfanyia vipimo na kumpa matibabu!
   
 7. Evarm

  Evarm JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,499
  Likes Received: 186
  Trophy Points: 160
  Thanx chatu dume.
   
 8. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #8
  Sep 24, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Tatizo la pimples ni kubwa na linaweza kuongezwa na majaribio yeyote ya kupambana nazo. Namaanisha kuwa wapo watu wanaishia kupata madhara makubwa sana ya ngozi kwa kuajribu 'matibabu' tofauti kuondokana na tatizo la pimples. Hivyo cha kwanza kumshauri huyo dada ni kuwa asijaribu kila anachoambiwa apake, kwani mara nyingi response inategemea na mtu binafsi, na vitu vingine vinaweza kukusababishia madhara magumu sana kuyatibu baadae.
  tukirudi kwenye tatizo ni kuwa mara nyingi pimples hutokea kutokana na level ya hormones fulani hasa hasa oestrogen. Hormone (pamoja na nyingine) hii hucontrol kiasi cha mafuta yanayokuwa deposited kwenye ngozi, na yanapozidi na kushindwa kutoka, pimples zinatokea. Kabla ya kujaribu njia za kupaka vitu, namshauri ajaribu njia za asili, yaani scrubbing. Hapa siongelei ile scrubbing ya kwenda kufanya sijui salon, ila scrubbing ya kufanya mwenyewe home. Kila baada ya siku moja, jioni akioga a-scrub kwa kutumia dodoki ikitegemea na ugumu wa ngozi. Asiogope maumivu hasa siku za mwanzo, ascrub kwa dakika tano kwa nguvu akitumia dodoki, maji ya uvuguvugu, na sabuni isiyo na dawa (kama jamaa). Baada ya hapo apake vaseline (natural petroleum jelly), na afanye hilo kuwa zoezi la kudumu kuwa kila baada ya siku moja, akioga lazima asugue uso na maeneo mengine yote yenye pimples kwa nguvu. Akumbuke pia kuwa Vaseline ni dawa murua ya fangazi ambalo ni tatizo kubwa kwa watu wanoishi maeneo yenye joto...
   
Loading...