Msaada wenu tena wadau..mtendaji wa kijiji kanifungia biashara yangu.nimfanyeje?

mwmbeki

Member
Apr 8, 2017
91
124
Ndugu wapendwa nawasalimu katika bwana na Mohammad
Mara nyingi napopata matatizo katika shughuli zangu napenda kuwashirikisha ili nipate pa kuanzia.
nawashkuru sana wote ambao hunipatia msaada wa mawazo na hakika unisaidia
Leo lalamiko langu ni hili hapa:
Mimi nafanya biashara mbali mbali ikiwemo na ya mapooltable.hapa jijin arusha namiliki mapooltable 3 ambayo yako sehem tofautitofauti za jiji. kwa mujibu wa sheria za nchi pooltable ni miongoni mwa michezo ya kubahatisha kama ile ya Biko,tatu mzuka,beting n.k

mchezo huu umekuja juu na unapendwa sana na watu wa rika zote wakiwemo na watoto.na umekuwa hadi na mashindano kuanzia ngazi ya kata,tarafa,wilaya,mkoa,kitaifa na kimataifa..mfano mwaka juzi kimataifa ya Africa mchezo huu ulidhaminiwa na Tanzania ambapo nchi nying za Africa zilishiriki zikiwemo Africa kusin,Lesotho,Botswana,Malawi,uganda,Kenya na nyingine nyingi fainali ilifanyikia Tanzania daresalaam kama wadhamin,manake na sisi tulishiriki ambapo mshindi wa kwanza alijinyakulia kitita cha million tano za kitanzania.

kwa mujibu wa rais wa nchi yetu mh magufuli alitoa mwongozo kuhusu mchezo huu baada ya kuona vijana wengi hawafanyi kazi waanamkia kwenye mapool table.

tarehe 15/3/2016 alipokuwa akiwaapisha wakuu wa mikoa katika viunga vya ikulu aliwaagiza hivi: "naomba ninukuhu
watakao cheza pool table kabla ya sa 10,wakamatwe wapelekwe polisi wakatoe faini ya laki 3kila mmoja.mapool table yafunguliwe sa 10 baada ya kazi siku za wikendi yafunguliwe sa 4 asubuhi ili watu wafanye kazi kwanza" mwisho wa kunukuu.

Jana tar 31/1/2018 kijana wangu wa kazi aliingiwa na tamaa ya pesa baada ya kushawishiwa na Wateja wa pooltable na kufungua sa 9 mchana,ndo mtendaji akawakuta na kuchukua kete na fimbo za kuchezea baada ya kuwakamata wachezaji na kuwapeleka polisi wakalipe faini kama raisi alivyoelekeza,na anasema alikuwa hajui kuwa kuna pooltable kwenye himaya yake,akasema hataki pooltable kwenye himaya yake ya uongozi hivyo nilihamishe nipeleke kwingine. kinyume kabsa na sheria za nchi, nimchukulie hatua zipi??
nsaidien wapendwa.
 
Duh hii kesi nzito sasa kwann wewe mtendaj hataki pooltable anyway ngoja wajuzi wa hii tasinia waje utapata ushaur nn ufanye
 
Hapo fanya kitu kimoja , kama bado ana kete na fimbo nenda ukamuombe akurudishie. Kama atakata kurudisha tafuta watu wazima wawili uende nao tena kumuomba akurudishie mali zako kama atakataa tayari utakuwa na mashahidi, then mfungulie kesi mahakama ya mwanzo kwa kushikilia mali zako kinyume cha sheri na kutaka kuhamisha biashara yako kinyume cha sheria . Maana hana mamlaka ya kufunga biashara yako wala kukuhamisha hata kama unavunja sheria chenye mamlaka hayo ni mahakama.
 
Mkuu kesi hii inatatuliwa na baraza la kata au kijiji ulichopo... Linazungumzika na kueleweka, it seems hata ushuru wa eneo la biashara ulikua haulipi, inakuaje mtendaji ashindwe kujua hapo kweli,,, ila usiogope haviusiani, embu nenda baraza la kata utatue kwanza huo mgogoro alaf ukirudi uende kwa afsa mtendaji wa kata hapo akupe kibali cha biashara ya pool table eneo ilo uwe kihalali siku nyingine hakuna atakae kuzingua tena.
 
IBURUZE MAHAKAMANI SERIKALI YA KIJIJI NA UTALIPWA MPUNGA MREFU ILA LIPA KWANZA FAINI YA POOL TABLE (JAPO HAIPO KISHERIA AMBPO MIMI NICNGELIPA)
 
IBURUZE MAHAKAMANI SERIKALI YA KIJIJI NA UTALIPWA MPUNGA MREFU ILA LIPA KWANZA FAINI YA POOL TABLE (JAPO HAIPO KISHERIA AMBPO MIMI NICNGELIPA)

Hapana mnakosea sana, jamaa hayupo kihalali ktk ilo eneo, tayari hili tu linavunja madai yake karibu yote, kama angekuepo kihalali hapo basi afsa mtendaji asingestuka kiasi icho, pili hawa watu maafsa watendaji msiwadharau sanaa, wamepewa nguvu kubwa sanaa na sheria za manispaa y mijiji/ vijiji wana uwezo wakuifungia biashara yoyote pia isipokizi vigezo vilivyowekwa na almashauri ya mji/kijiji, na kesi za namna hii zipo sanaa dar, huku wanaheshimika sanaa hawa watu, msiwadharau hawa.
 
Back
Top Bottom