Msaada wenu tafadhali, nyumba ya wanafamilia imeteketea kwa moto

Norshad

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
5,128
12,216
Habari za asubuhi ndugu zangu wakubwa kwa wadogo.

Naamini wote tumeamka salama na wenye afya njema na hata wale wenzetu waliopo katika matatizo ya kiafya ama kiuchumi tuwaombee wapate wepesi wapite katika hiyo hali na warudi katika hali ya kawaida na waweze kuendelea katika mihangangaiko yao ya utaftaji wa kila siku.

Nije katika suala langu.

Siku ya Jumamosi kuamkia Jumapili nilipatwa na shida, nikiwa kama sehemu ya mwanafamilia, nikiwa na maana tatizo sijalipata mimi moja kwa moja bali limetokea ukweni kwangu ambapo mimi nilioa hapo na mtoto wangu anaishi hapo.

Nilipigiwa simu usiku kwamba nyumba wanayoishi huko Mombo muda huo ilikuwa ikiteketea kwa moto na hata jitihada nyingi zilifanyika katika kuokoa vitu vilivyomo ndani lakini hakuna kilichotoka zaidi ya wenyewe tu mdio walifanikiwa kutoka salama.

Sababu ya kuja huku leo hii kuomba msaada ni kwamba kama kuna yeyote ataguswa na suala hili naomba anisaidie msaada wa aina yoyote ile sababu mimi pekee nimeshindwa, nimejitahidi katika kile ambacho naweza ni kwamba uwezo wangu kama mimi umefikia mwisho ukizingatia kwa sasa siko vizuri kiuchumi, nina hali mbaya, maana huwa naamini ukweli humuweka mtu huru.

Msaada inaohitajika huko ni nguo hasa za watoto maana wapo wawili pale; mmoja ana umri wa miaka mitatu (wa kwangu) na mwingine ana umri wa miaka tisa wa shemeji yangu wa kike ambaye na yeye hayupo yupo anatafta maisha huko Oman na ndio kaondoka mwezi uliopita tu.

Pia kuna hao wazee wetu amabao nao ni watu wazima hawana kazi zaidi ya kutegemea kilimo ambapo mazao waliyokuwa wamehifadhi ndani (mahindi) yote yameungua na hata wao walitoka na nguo hizo hizo walizovaa kama watoto.

Mimi nimejitahidi kutoa kile nilichonacho lakini bado msaada wangu hautoshi kwa kweli sababu mpaka sasa nimebaki sina kitu na bado hawa watu wanahitaji zaidi msaada sababu hakuna kilichopona.

Naomba kwa yoyote atayekuswa na hili anaweza kutoa msaada wake wa aina yoyote ile nguo za watoto, za hao wazazi wetu, chakula ama hata mchango wowote ule atakaoona yafaa ili tiweze kuwasaidia watoto na kuwafariji hawa wazee wetu, maana wazazi wa aliyekuwa mke wangu ni sawa na wazazi wangu pia.

Kwa yeyote aliyeguswa anaweza kuwasiliana nami kwa namba hiyo apo: 0782566676

Jina ni Nooshard yaani mimi mwenyewe.

Mimi bado nakimbizana lakini asubuhi hii nikapata wazo la kuleta hii shida yangu huku nikiamini naweza pata msaada wowote ule, hata wa kimawazo.

Natanguliza shukrani.
 
Kwa sasa nipo Morogoro naelekea eneo la Msamvu Stand niweze kuwatumia baadhi ya vitu nimepata. Lakini kwa yeyote atakayo guswa naomba asisite kunitafuta kwa namba hiyo apo juu.
 
Anzia kwa serikali ya mtaa kisha kwa mkuu wa wilaya kuna kamati ya majanga na dharura utasaidiwa huko pia misikitini na makanisa ya eneo tukio lilipotokea huko Mombo.

Chanzo cha moto ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh mzee mimi sipo huko labda niwashauri waliopo huko wafanye hivyo, chanzo ni short ya umeme
Anzia kwa serikali ya mtaa kisha kwa mkuu wa wilaya kuna kamati ya majanga na dharura utasaidiwa huko pia misikitini na makanisa ya eneo tukio lilipotokea huko Mombo.

Chanzo cha moto ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app

065
 
Back
Top Bottom