Msaada wenu ni muhimu kwangu

queenkami

JF-Expert Member
Feb 8, 2010
1,599
1,025
.wapendwa hope wote mko fine!
1.naombeni mnisaidie kwa anayejua kodi ya mwezi kwa sehemu inayotosha kufanya mgahawa kariakoo au posta.
2.nataka kununua shamba morogoro lkn sijui ni jinsi gani watu wanafanya wanapotaka kutafuta shamba lakununua na sina mwenyeji huko wakunisaidia kutafuta na pia ningependa kununua kwa kutumia njia za kiserikali,hivyo naomba kwa anayejua juu ya haya maswala anipe japo mwanga.
thanx in advance.
 
ila unaita sana qeen, umeolewa??? unaweza pia kupata mchumba hapa jamvini!!!!!

any way, all the best
 
ila unaita sana qeen, umeolewa??? unaweza pia kupata mchumba hapa jamvini!!!!!

any way, all the best

vipo vitu vingine vingi tu vya maana naweza kupata hapa jamvini lkn mchumba kutoka hapa sio my wish!!!asante kwa wazo lako lkn,nipe msaada nilioomba basi kama unajua lolote.
 
vipo vitu vingine vingi tu vya maana naweza kupata hapa jamvini lkn mchumba kutoka hapa sio my wish!!!asante kwa wazo lako lkn,nipe msaada nilioomba basi kama unajua lolote.

halafu mbona hujasema thanks pamoja na kukusifia dada? huo si utamaduni wa kiafrika!

haya bwana watakuja hapa wenye madili yao watakumegea wenzio tuko mbali, ila mchumba very important na hapa kuna wazuri tena wote ma-great thinker wa kuaminika!!!!!!!

usipuuzie
 
lol kweli wewe Akili kichwa ni noma
Dada hapa utapata msaada na hapajaaribika neno mie siko maeneo hayo ulotaja
 
inategemea lakini ni kuanzia laki saba kwa mwezi na kuendele.
la shamba, mwingine aseme.
 
inategemea lakini ni kuanzia laki saba kwa mwezi na kuendele.
la shamba, mwingine aseme.
Thanx Nanu!inategemea na nini?hivi huwa wanataka ya mwaka au hata miezi 6 unaweza kulipa?
 
1. Kwa biashara nadhani kinachotoa uelekeo wa kodi ni eneo husika, jengo na accessibility yake, ila nyingi kwa maeneo hayo uliyotaja ni kati ya laki 6 mpaka 1.5m kwa mwezi na wengi wao huchukua kodi ya mwaka na kuendelea kulingana na biashara unayotaka kufanya!

2. Kuhusu taratibu za ununuzi wa shamba Morogoro, mi si mkazi wa huko ila nilishawahi kufanya taratibu hizo, unakwenda eneo husika unalotaka kumiliki shamba lako hilo, unauona uongozi wa kijiji ukiwa na barua ya maombi kwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji ambayo inaeleza kwa ufupi nia yako ya kuhitaji shamba hilo na kiasi cha hekari unazohitaji, then kuna gharama chache ambazo hulipwa kwa baraza la ardhi la kijiji na baadae maombi yako yakioshapitishwa kuna bei ya serikali kulingana na eneo husika ambayo ni kiasi kidogo sana kwa mfano hekari 10 waweza kulipa kiasi cha laki 2 mpaka 3, na baada ya hapo utapewa barua za serikali ya kijiji za kuthibitisha umiliki ambazo utahitaji kuzipeleka ngazi ya wilaya kwa ajili ya upimaji na kuwekewa mipaka ya shamba lako na baadae kupata hati ya umiliki. Natumai umepata mwanga kiasi.
 
nawashukuru wote mlionipa mwanga.ila mbona wanafamilia mmenichunia hadi nahisi kutengwa kwa kutopewa ushirikiano wenu jamani bandugu.
 
nawashukuru wote mlionipa mwanga.ila mbona wanafamilia mmenichunia hadi nahisi kutengwa kwa kutopewa ushirikiano wenu jamani bandugu.

Kisusi Mohamed amekueleza kinabaubaga juu ya maswali yako! Kazi kwako!
 
kuhusu shamba morogoro kwa mjini ninayo mawili pale mikese ekari 30 ( nimelima mahindi kidogo mwaka huu) pamoja na kule mgolole kwa masista( kama ekari 17) ...vilevile malinyi nina ekari zisizopungua 80 ,kati ya hizo 50 nalima mwenyewe mpunga ....je unataka ukubwa gani ??? naweza kukuuzia au kukukodisha
 
kuhusu shamba morogoro kwa mjini ninayo mawili pale mikese ekari 30 ( nimelima mahindi kidogo mwaka huu) pamoja na kule mgolole kwa masista( kama ekari 17) ...vilevile malinyi nina ekari zisizopungua 80 ,kati ya hizo 50 nalima mwenyewe mpunga ....je unataka ukubwa gani ??? naweza kukuuzia au kukukodisha

hongera una maeneo mengi!mie nataka lakununua sitaki kukodi ila nidokezee kwanza bei utakayoniuzia kwa ekari moja ndio nitajua ninauwezo wa kununua la ukubwa gani.
 
Mie ni mzoefu katika eneo lote la kariakoo, hasa kuhusu Masuala ya Biashara.
Unawe kupata eneo la biashara ya mgahawa kwa bei kati ya 150,000 mpaka 1,500,000/= kwa mwezi.Zaidi inategemea na eneo yaani mtaa mfano, mt wa kongo,Aggrey,Swahili,Nyamwezi, Sikukuu,Mchikichi, Msimbazi,Tandamti vyumba vina bei inayokaribiana,ila pia inategemea na aina ya Nyumba na ukubwa wa eneo.
Lakini vema ukaweka wazi aina ya mgahawa unaopenda kuanzisha,je unataka eneo la sq mita ngapi?.Lazima pia ujue aina ya wateja unaowahitaji.NB kumbuka kodi huwa ni kwa mwaka mzima, ila unaweza kupata hata kwa miezi sita.
Karibu sana Kariakoo.
 
Posta au kariakoo unataka kwa NHC walishika wahindi au kwa mutu binafsi??? kwa walioshika wahindi ni 1M mpaka laki 9 kwa mwezi kwani hawa wanashika kisha wanapangisha watu hapo usihoji nchi imeuzwa. na kwa watu binafsi ni 2M mpaka 1M sasa sijui unatakaje?
Morogoro viwanja vinapatikana Manispaa hapa Morogoro unakwenda kuandikisha jina Milioni 3 mpaka 4 ila usitoe zaidi ya hapo manispaa wanakupa full documents waweza kukope mukopo sehemu yoyote ila ni hayo tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom