Msaada wenu kwa mnaosoma Clinical Medicine na wazoefu

Peter Majaliwa

Senior Member
Jun 16, 2017
161
30
Niko Chuo cha Muyoge, nasoma kozi ya Clinical Medicine ninapitia wakati mgumu sana katika maisha yangu ambapo imenifanya niingie kwenye mgogoro wa nafsi maana mazingira ya chuo nilichopo na ufundishaji hayaridhishi.

Mgogoro wangu wa nafsi nataka nihamie chuo kingine ambapo moyo wangu utaridhika na kuweza kujituma kufikia malengo yangu nasio niendelee kujazwa maneno yasiyokuwa na ukweli wowote yanayotolewa na wanafunzi na uongozi wa chuo hiki nilichopo.

Kozi hii nilipenda kuisoma mwenyewe sijalazimishwa na mtu. Nilitaka nihamie Mlimba Morogoro ili niweze kufikia malengo.

Nisadieni ushauri vinginevyo nitafeli maana kozi hii bila kujituma na kuiweka moyoni sitafikia malengo.

Naombeni sana sana munisadie wanajamvi. Kila kukicha mawazo, kuchekwa na kulia.

Nisadieni niweze kufarijika na kuanza kufikia mafanikio 2020 kwa kufanya vyvema katika hili. Mimi nipo mwaka wa kwanza, semester one.
 
Unalia Uko semister one
Mambo yakichangamka si utakimbia
Kwanza Changamoto zipi unapitia na Unahitajii msaada Gani mkuu
 
nielekeze napataje nafasi make Niko private
Hiyo ni Ngumu mkuu
Ila Unaandika Barua Inakua na anuani nne ya chuo unachotoka ,Anuani yako na Chuo unachotaka Kuhamia (Hii ni Baada Ya Kuconfirm Kama Kuna nafasi) na anuani ya Wizara Kama sikoseii ...Baada Ya Hapo Unagongewa Muhuri chuo unachotoka Then unaenda Chuo unachotaka Kuhamia unagongewa Muhuri tena then Barua Unaituma Nacte unasubiri Majibu Hii ni mpaka Umalize semister One Bila Sup
 
Nahitaji ushauri wako nihamie ? Make naona hapa Hanna nichokifanya ilanapoteza tu pesa mkuu yaani hiki chuo kinazidiwa kwa mandhari na shule ya msingi niliyosoma naona na ahishwa
 
Poleee Kijana,, ila nadhani kwenda mlimba ni kukwepa majivu na kukanyaga moto,, kaa utambue hakuna mafanikio mepesi, hasa kozi za medicine, kozi ukifanikiwa kumaliza una 50percent ya kufanikiwa, so kama unataka kuhama ni vyema ukatafuta nafasi serikalini,, ila ukienda private tena utakua ni mwanzo wa kuhama hama na unaweza usimalize course..
 
Mkuu kwahyo ni pambane hapa hapa hapa nikipata supp nazishughulikia kisha naenda serikalini
 
If possible,, coz kwenda serikalini lazima utapoteza at least one semister mpaka one year kutokana na connection zako huko uendako, na katika maisha usikubali mazingira yakuendeshe wewe, inabidi uyaendeshe, means ukitaka supplementary itakuja na usipotaka haiwezi kuja, hii course inakatisha sana tamaa na kama una roho ndogo kuiacha ni kawaida
 
[/QUOTE
Ni kweli inanikatisha sana tamaa nifanyeje na naipenda sana
 
Onyesha uanaume na tofauti na wengine walioogopa,, jambo lolote linaloonekana gumu huwa lina mafiniko makubwa mbeleni
 
nielekeze napataje nafasi make Niko private
Ilikuwaje mpaka ukaamua kwenda chuo kama hyo ambayo hata jina halieleweki.. Kuna vyuo kedekede vya serikali kama
Mtwara COTC
Lindi COTC
Iringa COTC
Masasi COTC
Mafinga COTC
Hv vyote viko chini ya wizara ya afya.. Nakushauri uombe hapa LINDI au Mtwara.. Hutojuta
 
Kuna gharama zozote labda zinahitajika kupata nafasi?
 
Back
Top Bottom