MSAADA: WATAALAMU WA SHERIA ZA USAFIRI WA ANGA NA MIKATABA NISAIDIE.

Chilli

JF-Expert Member
Jul 17, 2011
1,655
743
Habari ndugu Wasomi wa humu.

Naandika nikiwa jimbo mojawapo la nchi ya China. Ninaomba msaada wa kisheria. Nilikata tiketi na kampuni Emirates mwezi wa tisa mwaka huu ya kuja hapa jimbo nilipo na kurudi Dar es salaam (Round Trip). Na katika makubaliano yetu ilikuwa wao kunichukua Dar es salaam mpaka hapa nilipo (ambapo walitekeleza saa ya kuja) lakini vilevile ilitakiwa wanichukue mji huu niliopo na kunirudisha mpaka Dar es salaam mwakani nikiwa narudi nyumbani.

Lakini wiki kama tatu zilizopita nilipokea ujumbe wa e-mail toka kwa kampuni ya Emirates kwamba mwakani itabidi tukapandie mji mkuu wa China Beijing kwani safari za kuja hapa nilipo zimesitishwa. Na kwamba wao hawatanisafirisha mimi wala abiria wengine kutoka mji huu mpaka Beijing. Hivyo tutajitegemea. Nimewaandikia kuwaelezea kwamba wanigharamikie lakini hawajanijibu.

Kutoka jimbo hili nilipo mpaka Beijing ni umbali mrefu na gharama kwa ndege ni Yuan zisizopungua 1200 ambazo ni sawa na kama Tsh 396,000 na kwa Treni ni kama Yuan 500 ambazo ni sawa na Tsh 165,000.

Je, kwa wanaofahamu sheria za masuala ya usafiri wa anga na sheria za mikataba, ninaweza wafungulia hawa watu kesi ya namna gani? Je, naifungualia wapi? Is it material??

Asanteni sana.
 
Back
Top Bottom