Natania
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 262
- 217
Habari zenu!
Tafadhali naomba msaada wa ushauri. Nina ndugu yangu (wa kike - miaka 50) ambaye ni mwathirika wa UKIMWI (miaka kama minne sasa toka apime). Shida ni kuwa huwa hataki kunywa dawa. Akiacha kunywa dawa hali yake inakuwa mbaya sana.
In fact huwa anachanganyikiwa kabisa. Tumempeleka hospitali ya wagonjwa wa akili Mirembe -Dodoma karibu mara mbili. Akiwa huko Hospitali ana-recover haraka sababu anakunywa dawa (ARV na zile nyingine za kutibu psychosis) kwa lazima - shida ni kuwa akirudishwa nyumbani (na huwa anarudishwa mapema kabla hata haja-recover vizuri) anakuwa hataki tena kunywa dawa, mkilazimisha anaishia kutoroka!
Kwa sasa amekuwa kama mtu aliyechanganyikiwa - haamini tena kuwa anaumwa ukimwi bali anaamini amerogwa, mara anaamini ni hali ya hewa na anazungumza mambo ambayo hasa unajua amechanganyikiwa.
Kwa wale wanaojua namna nzuri ya kuwasaidia wagonjwa wa aina hii (mbali na kuwapeleka hospitali za rufaa za mikoa ama mirembe) naomba ushauri tafadhali. Kama kuna Hospitali private ambayo ina-specialists (kwa mikoa ya Dar, Moro, ama Dom) wa hali kama hii ya ndugu yangu tafadhali naomba contact zao!
Tafadhali kama una-ushauri mwingine usisite ku-shirikiana nami.
Natanguliza shukrani.