Msaada: Wanaoijua Mgambo JKT Tanga ikoje mazingira yake?

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,374
73,975
Mwenye kuifahamu Mgambo anisaidie mazingira yakoje> Panafaa kwenda? au ni mateso? Haya makambi yanatofautiana ingawa kote ni mitulinga ya Jeshi.
 
Mkuu..,
Kambi ya Mgambo JKT ipo Waliya ya Handeni, Kijiji kinaitwa Kabuku, eneo ambalo ni njiani kabla ya kufika Segera.
Mandhari yake si mabaya sana kwakuwa inapakana na Vijiji vya Jirani, na ni wastani wa Km 7 kutoka njia kuu ya DSM-Segera na panafikika wakati wote!
 
Mwenye kuifahamu Mgambo anisaidie mazingira yakoje> Panafaa kwenda? au ni mateso? Haya makambi yanatofautiana ingawa kote ni mitulinga ya Jeshi.

Wewe nenda JKT, mtaala wa JKT ni ule ule wether ukienda Mafinga, Mgambo, Bulombora au wapi! Hakuna cha kusema kambi fulani ina nafuu au kali kuliko kambi nyingine. Labda kama unazungumzia hali ya hewa! Kama unataka baridi kali nenda Mafinga!
 
Mwenye kuifahamu Mgambo anisaidie mazingira yakoje> Panafaa kwenda? au ni mateso? Haya makambi yanatofautiana ingawa kote ni mitulinga ya Jeshi.
Mjiandae kuvuna mahindi huko mgambo, kuna mashamba yanaitwa mashamba dunia. Utavuna mpaka ukome, ndo kazi zilizopo huko.
Labda utakachoinjoi ni kula machungwa tu.
Ile ni kambi ya uzalishaji, hivyo utakua umeepuka mazoezi ya kijeshi kwa kiasi fulani. But pako vizuri japo nilitoka huko zamani sana.
 
Thanks a lot. Wewe umenipa taarifa ninazozitaka. Ubarikiwe.
 
Mjiandae kuvuna mahindi huko mgambo, kuna mashamba yanaitwa mashamba dunia. Utavuna mpaka ukome, ndo kazi zilizopo huko.
Labda utakachoinjoi ni kula machungwa tu.
Ile ni kambi ya uzalishaji, hivyo utakua umeepuka mazoezi ya kijeshi kwa kiasi fulani. But pako vizuri japo nilitoka huko zamani sana
Machungwa ndo yalikua chakula tukidoji kazi.Hahahaaaa mujibu wa sheria hatari
 
Yes nasikia kuna mashamba makubwa ya mahindi. Kuna mwenzako kanijibu hapa. Lakini Tanga kuna ukame sijui kama wamelima.
yeah hakuna kikubwa zaidi ya kilimo nadhani taratibu nyingine ni za kawaida jeshini binafsi sikuona ugumu huenda kwa kua nilikua naumwa kila wiki hahahaa
 
Yes nasikia kuna mashamba makubwa ya mahindi. Kuna mwenzako kanijibu hapa. Lakini Tanga kuna ukame sijui kama wamelima.
Hakuna cha ukame wala nini, kulima ni kama kawa. Kipindi naondoka hapo tulikuwa tumeshaandaa ekari elf 2 kwa ajili ya mahindi na lengo ilikuwa tuandae ekari elf 4 .

Mpaka tunaondoka serikali ilikuwa imepanga kuwalipa fidia wanakijiji wa pale jirani ili wachukue ardhi yao iwe ya kambi. Lengo ilikuwa ni kuongeza mashamba zaidi.

Lakin sijui kama mambo yatakuwa yamebadilika maana nimeondoka huko operation ya kwanza kabisa mwaka 2013. Na ndo tulikuwa wa kwanza kama mnakumbuka vizuri.
 
sikumbuki maana sifuatilii mambo hayo. Wanangu hakuna aliyekwenda jkt hivyo sifuatilii. Last one ndiyo amechaguliwa kwenda hapo.
 
Kwani kule jeshini wanaruhusu kuumwa???
Magonjwa si yapo tu kokote,,ila hata ukiumwa hakuna mapumziko ya maana ila sie muda mwingi tulikua tunajiuguza ki uongo uongo mtu unaenda hosptal unadanganya kichwa sijui nini wakipima hauna lolote hadi joto kawaida ni vile tulikua tunafurahia kale ka muda ka kukaa hosptal wakati mazoezi/kazi zinaendelea.Aisee jeshi ni wito haswaa miezi mitatu niliona miaka kumi.HONGERENI WANAJESHI WETU
 
Hakuna cha ukame wala nini, kulima ni kama kawa. Kipindi naondoka hapo tulikuwa tumeshaandaa ekari elf 2 kwa ajili ya mahindi na lengo ilikuwa tuandae ekari elf 4 .

Mpaka tunaondoka serikali ilikuwa imepanga kuwalipa fidia wanakijiji wa pale jirani ili wachukue ardhi yao iwe ya kambi. Lengo ilikuwa ni kuongeza mashamba zaidi.

Lakin sijui kama mambo yatakuwa yamebadilika maana nimeondoka huko operation ya kwanza kabisa mwaka 2013. Na ndo tulikuwa wa kwanza kama mnakumbuka vizuri.
Hahahaaaa mwaka wangu pia
 
Back
Top Bottom