Msaada wana jf, wana ccm wenzangu nisaidieni humu!!

Boeing

Senior Member
Apr 16, 2017
151
421
1. Mwaka 2000 nilikuwa miongoni mwa walioomba kuteuliwa na chama changu kugombea ubunge jimbo mojawapo hapa tz. Mojawapo ya kigezo kilichotushindanisha wengi tuliogombea nafasi ile ni Elimu, hoja iliyoletwa na mpinzani wangu ndani ya chama. By that time nilikuwa sijamaliza masomo yangu hivyo nilipigwa chini akapita
mwenzangu.

2. Sasa hivi mnasema sifa kuu ni kujua kusoma na kuandika. Mbn hatueleweki?

3. Kwa upande mwingine najiuliza hivi kwa dunia ya sasa kweli tunahitaji engine ya watu wanaojua tu kusoma na kuandika? Inawezekana kipengele hicho kiliwekwa wakati elimu ikiwa duni hivyo wenye kujua na kusoma walionekana the most successful, hiyo sifa ni applicable hata sasa?

4. Miongoni mwa graduates waliotapakaa nchi nzima hakuna wenye sifa ya kuwa wakuu wa wilaya, mikoa au kuwa mawaziri!? Au hakuna makada wa chama waliosoma?

5. Ni kwa nini tusione kuna haja ya kuheshimu taaluma, wakapewa nafasi ya kuamua hatma ya tz? Hatuoni tunakosea kama nchi kudharau wataalam?

6. Ni kwa nini raisi ambaye ana ujasiri wa kuchukua maamuzi abaogopa kuwagusa hawa wanasiasa ambao tunaamini ndiko kwenye uozo wa vyeti feki??

NAOMBENI MAJIBU AU USHAURI NI KWA NN INAKUWA HIVI
 
Katiba inaelekeza kwa ujumla.

Lakini Chama na chenyewe kina taratibu zake ikiwa ni pamoja na Elimu ya Mhusika.

Hayo ya CCM mimi siyajui.
 
Wahenga wetu hawakuwa na maneno mengi; na kwahiyo bila shaka wangesema maneno manne tu: Punda afe, mzigo ufike!!

Hata ikibidi kuwapiga chini madaktari wote wa Muhimbili kama gharama ya kumlinda Mwana Mfalme..., potelea mbali; ni ama punda afe, mzigo ufike and no alternative!!

Pasipo budi, tunaweza hata kubadilisha sheria za nchi hii ili hatimae suala la kufoji vyeti lichukulie ni ubunifu na maarifa.. kwamba ni struggle za maisha! Ni ama punda afe, mzigo ufike!

Bado una maswali?!
 
Back
Top Bottom