Msaada wana JF,kuhusu makazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wana JF,kuhusu makazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Original Pastor, Nov 1, 2009.

 1. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mimi nimebahatika kutembelea nchi ya Congo Kinshasa, Sudan, Ethiopia Cha kushangaza nimeona maajabu sana katika nchi hizi kwani nilianza na Sudan yaani ni Kuwapongeza 100% kwani mji wao umepangwa vizuri hakuja sehemu gari haifiki kwani wao huruhusiwi kujenga mpaka kibali kitoke kwa kamishna wao wa ardhi. Kwani hata kujenga duka au baa lazima kitoke kibali na Serikali ijue kuwa kunawekwa nini na kama hakina faida kwa Wananchi hakiwezi kukubaliwa.

  kwa mfano kuhusu duka huwezi kuweka kila mtaa duka mpaka upate kibali wajue kweli hapo panahitaji duka la zivyo utaenda sokoni kuuza bidhaa zako.

  Pia open Space zipo nyingi kila mtaa kuna kuwa na kiwanja , shule ,hospital kituo cha Polisi na mahitaji muhimu ya Wananchi. Yaani Serikali ya huku inachofanya inapita juu na Helcopter inapiga picha kisha inachora Ramani na ukienda kuomba unaambiwa upewa kiwanja chako, na hakuna uchochoro ni mitaa na mtu akipewa kiwanja sharti la kwanza anatakiwa aweke fansi yoyote ile ilimradi tu hakuna mtu kukuingia sio fensi ya michongoma hapana nifensi ya matofali, makuti na mbao tena unaweka vyema hakuna mtu kuingia,ukienda Ethiopia Nchi iliyo milimani ambayo kila mtaa unajina lake yaani utafurahi walivyopanga mitaa hata Congo ila sijazunguka sana nilienda Rwanda hapo utafurahi mwenyewe hakuna mtu anayetupa uchafu eti fulani ataokota mji msafi umepangwa vizuri na ukumbuke miaka saba tu walikuwa Vitani.

  sasa twende kwetu Nauliza swali hivi Wizara ya Ardhi inafanya nini? kwani miaka ya 80's mabonde yote ya Keko, Mbagala, Kigogo, Buguruni, Kagera Magomeni,na sehemu zingine kulikuwa hakuna nyumba na Serikali ilikuwepo na cha kushangaza leo hii watu wamejenga mpaka hakuna njia ya magari je Nauliza Hakuna Wizara inayohusika na hili?

  Au inaachiwa jamii pekee ijipange? kwa KWa nchi nyingine kama mji utakutaka kubomoa kwa sababu huna kibali basi utabomoa je kwa Tanzania inakuwaje? kwani Serikali si ya Kulaumiwa moja kwa moja ni wananchi wenyewe wangelalamika Serikali ingefumbuka macho.Kwani ukifika Kariakoo utashangaa mwenyewe wale wanakwenda kufanya vile kwasababu hakuna Masoko mitaani ndo maana wanajikusanya na kufanya biashara chini kungekuwa na mipango madhubuti wangeishia huko huko mtaani.

  Nilipata kutembelea mkoa mmoja wa Iringa nilishangaa kuona yaleyale ya Makazi Holela kuna sehemu jina sikumbuki ila nimita 100 kutoka katika Stande kuu ya Mabasi Iringa wamejenga kiholela sasa utasema ni wale wale waliokuwa wanaishi kule mabondeni( makazi holela wa Dar es salaam ndio wamehamia huku nini kwani nyumba zimejengwa shangalabagala.

  Sasa tukiacha na Mkoa huo mimi ni Mtanzania nina machungu sana na nchi yangu kwanini Serikali isipime maeneo nilienda Ardhi kuomba kupimiwa eneo langu jibu nililojibiwa na afisa mmoja wa ardhi nilitoa chozi maana sikutegemea kuwa msomi kama yule angeniambia maneno haya na nukuu " wewe wenzio wanajenga tu wewe unataka kupimiwa kiwanja ili kikusaidie nini? kama unataka kupimiwa kiwanja hapa lazima utoe pesa za upimaji hela ya mpimaji na uniwekee mafuta kwenye gari" sasa nikajiuliza inamaana Serikali haina mafuta hapana, ina maana Serikali halipi mshahara hapana Je hii yote inatokana na nini?

  Sasa mimi ni mtanzania nina machungu na nchi yangu nataka tuijenge vyema ipendeze kama nchi nyinge ambazo zina Vita wakati wote lakini Sera zao zimekaa vizuri Afisa ardhi anapima viwanja bila kukuomba rushwa yoyote sisi watanzania tumejaliwa kuwa na wasomi wengi wa sauala ya Ardhi lakini sasa sijui ni ninini? wanakuwa hawatoi ushauri kwa Serikali.Swali la msingi ni nani wa kulaumiwa Serikali au Wananchi wanaojenga kiholela. maana hata mimi baada ya kujibiwa vile nikarudi kujenga bila hata ya kupimiwa je nitalaumiwa? Yaani tunashindwa kujenga daraja pale Kigamboni? wakati kuna nchi madaraja wanayo saba tena makubwa.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hoja yako ni sawia ndugu kiongozi.

  Tatizo letu ambalo tunalizungumzia huku kwetu, kila siku, ni tatizo la uongozi dhaifu usio na maono ya mbele. Kufikia maendeleo ARDHI ni mojawapo ya nyenzo muhimu kabisa. Ili tuendelee hatuhitaji tu ardhi bali tunahitaji kupanga vyema jinsi gani ya kuitumia ardhi hiyo, ikiwemo na suala zima la upangaji miji.

  Binafsi sielewi kiongozi anawezaje kunadi kuleta maendeleo bila ya kuwa na roadmap ya miji na vijiji. Hili binafsi sijawahi sikia popote walipoendelea bila ya kupangilia miji yao. Ni Tz pekee ambapo nchi zote zinazotuzunguka zinatuonea gere na ardhi yetu lukuki lakini bado tunaishi ktk slums, na bado zinaongezeka siku hadi siku!

  Nashindwa kuendelea kutype maana nitaishia kutukana.
   
 3. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Haya yote kutokana na uzembe, umangimeza, ufisadi na uvivu na kukosekana mifumo imara ya kusimamia mambo na badala yake kutegemea utashi wa mtu binafsi aliyepewa nafasi. Tatizo hili ni kutokea awamu ya kwanza mpaka sasa ambazo zote kwa bahati mbaya zimetokana na chama cha mapinduzi. Tunahitajiaka tubadilike, tubadili mfumo, tuweke mifumo yauwajibikaji na tuisimaimie.
   
Loading...