Msaada wakuu Sabufa (radio) SeaPiano haitoi sauti

Wgr30

JF-Expert Member
Jan 22, 2017
1,770
2,374
Ni matumaini yangu kuwa mko salama,

Wakuu radio (sabufa) aina ya SeaPiano imepata shida haitoi sauti na hata upande wa Fm radio haingei wala haiendi kila ukibadili inaandika Bluetooth ila kuwaka inawaka kawaida sauti unaisikia kwa mbali sana haingozeki wala nini.

Tatizo limeanza mchana saa16pm.

Msaada wenu ndugu!
 
na hapo ndio mwisho wa sabufa.

ukilipeleka kwa fundi utaambiwa mara AC ya joto imekufa,mara capacitor ya speed imekatika,sijui njia ya speaker imemiss nk.

cha msingi nunua jingine tu,kama umechoka sana tafuta hela ununue kinachoeleweka.
 
Japo mm sio mjuvi sana ila hua napenda sana kijifunza kupitia nyuzi za wataalamu walio humu.

1. Control itakua imeharibika yaani ile ya mode ya kuhamishia bluetooth, radio na USB.

2. Ic ya base itakua imeharibika peleka kwa fundi aliyokarbu nawe ili akapime kama ni nzima.

3. Au sehemu ya pawa itakua na shida.
 
na hapo ndio mwisho wa sabufa.

ukilipeleka kwa fundi utaambiwa mara AC ya joto imekufa,mara capacitor ya speed imekatika,sijui njia ya speaker imemiss nk.

cha msingi nunua jingine tu,kama umechoka sana tafuta hela ununue kinachoeleweka.
Acha bana nawewe! Anunue jingine wakati kitu kina spare mitaani na kinatengenezeka kabisa..!?

Hii ni sawa na mtu alete tatizo aseme simu yake touch imekufa hai sensi afu umwambie hiyo ndo basi tena aweke kwenye droo anunue nyingine wakati touch screens zipo madukani huko zimezagaa...
 
ana nafasi ya kukusikiliza wewe au mimi pia,ila ninachojua,akifata ushauri wako siku si nyingi ataukumbuka wa kwangu.

sabufa ikizingua imezingua,niamini mimi.
 
Mimi ki aborder changu cha elfu 60 hakina hata muda tangu ninunue halafu eti tangu juzi ghafla tu spika ndogo hazipigi(twita) wakati pini nzima tu...

Kilianza upande (wa tundu moja) ndo lilikuwa halifanyi kazi mara ikawa yote tu ukichomeka waya ni kama hujachomeka kwahiyo inapiga spika ya redio tu huwezi kusikia mziki labda usogeze sikio karibu kabisa na redio

Maelezo ya ziada ni kwamba tangu ninunue nimekuwa nikigongesha sana mziki kwa Bluetooth. Picha hizo ya kwanza ndo redio na spika zake ya pili inaonesha upande wa kuchomeka nyaya (pini) na ya tatu ni spika kubwa ya redio ambayo ndiyo inayodunda peke yake kwa sasa

Naomba msaada wa mawazo hata mimi
JPEG_20210107_123933_785774813.jpg
JPEG_20210107_124008_-1896134744.jpg
JPEG_20210107_124129_1317707788.jpg
 
Chukua lile speaker kubwa lenye kimonitor lipige kofi juu mambo yote yatakaa sawa. Ukute ni mende tu kagusa waya wa FM. Za kuambiwa changanya na zako
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom