Lussadam
JF-Expert Member
- Oct 13, 2007
- 1,294
- 835
Kwani kuna Bahati Nasibu yoyote umeshiriki huko UK???? Kama hujacheza Bahati Nasibu yeyote huwezi kushinda. Yaani ni sawasawa na mti wa Maparachini uzae MananasiHeshima kwenu Wana-jukwaa
Natumai hamjambo wote Wakuu..
Niende kwenye maada moja kwa moja,,.
Takribani wiki moja imepita toka nipokee ujumbe wa simu ukinijulisha kuwa nimeshinda bahati nasibu katika kampuni ya vinywaji huko UK,, hivyo natakiwa kutuma taarifa za umri na mawasiliano yangu..
Baada ya tafakari niliamua kutuma na hawakusita kunijibu na kunitumia fomu ambayo nlipaswa kuijaza taarifa kama marital status, umri, kazi, utaifa na kuituma Bank ya huko huko UK.
Niliwatumia taarifa hizo nao wakajibu kuwa wanahitaji taarifa zifuatazo
1. Kitambulisho cha Utaifa au Leseni ya udereva au Hati ya usafiri
2. Cheti cha ushindi kutoka kampuni tajwa
3. Fund Release Order kutoka Financial Services Authority ya UK.
Niliwajulisha kampuni husika na baadae wakatuma Cheti tajwa na kuniomba kama npo UK basi nizione Mamlaka na kama nipo nje ya UK basi niwasiliane na Wakili ambae wamenipa mawasiliano..
Wakuu Je hapa sio kutaka kupigwa??
Msaada wa kimawazo Wamajukwaa..
Natanguliza shukrani