Msaada wakuu, nimetumiwa SMS kuwa nimeshinda bahati nasibu huko UK, je nataka kutapeliwa?

Lussadam

JF-Expert Member
Oct 13, 2007
1,207
2,000
Heshima kwenu Wana-jukwaa

Natumai hamjambo wote Wakuu..

Niende kwenye maada moja kwa moja,,.
Takribani wiki moja imepita toka nipokee ujumbe wa simu ukinijulisha kuwa nimeshinda bahati nasibu katika kampuni ya vinywaji huko UK,, hivyo natakiwa kutuma taarifa za umri na mawasiliano yangu..

Baada ya tafakari niliamua kutuma na hawakusita kunijibu na kunitumia fomu ambayo nlipaswa kuijaza taarifa kama marital status, umri, kazi, utaifa na kuituma Bank ya huko huko UK.

Niliwatumia taarifa hizo nao wakajibu kuwa wanahitaji taarifa zifuatazo

1. Kitambulisho cha Utaifa au Leseni ya udereva au Hati ya usafiri
2. Cheti cha ushindi kutoka kampuni tajwa
3. Fund Release Order kutoka Financial Services Authority ya UK.

Niliwajulisha kampuni husika na baadae wakatuma Cheti tajwa na kuniomba kama npo UK basi nizione Mamlaka na kama nipo nje ya UK basi niwasiliane na Wakili ambae wamenipa mawasiliano..

Wakuu Je hapa sio kutaka kupigwa??
Msaada wa kimawazo Wamajukwaa..
Natanguliza shukrani
Kwani kuna Bahati Nasibu yoyote umeshiriki huko UK???? Kama hujacheza Bahati Nasibu yeyote huwezi kushinda. Yaani ni sawasawa na mti wa Maparachini uzae Mananasi
 

makatheboy

Senior Member
Sep 5, 2016
157
500
Bado hawajakukosa. Hizo data ulizozitumia wanaweza kuzitumia kukupiga, kwa mfano:
1. Kupata password zako za miamala ya pesa na kadhalika. Wata click kwenye Forgot your password? Hizo data ulizowapatia zitawawezesha ku reset password mpya na kupiga hela yako yote iliyoko benki na iliyoko kwenye mitandao ya e-money hususani tigopesa.

2. Data ulizowapa zitawawezesha kutengeneza vitambulisho vitakavyotumiwa na wasafirisha unga, magaidi (terrorists), wahamiaji haramu, money laundry, nk wakitumia identity yako. Ni watu hatari.

3. Na kadhalika. Hivyo hauko salama. Mbinu hizi za wahalifu wa mitandaoni (cyber criminals) ni wa siku nyingi na jamaa hawa wengi wao wako nchi za Afrika magharibi. Kwa hatua uliyofikia wasiliana na polisi wa mtandaoni (cyber police) wanaweza kukusaidia. Pole sana kijana. Ndiyo mambo ya mitandao. Kuna mijizi hadi majambazi humu mtandaoni. Be very careful in this digital era.
Credited Mkuu..
Japo saana wapo money oriented though na mengine pia yawezekana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom