Msaada wakuu kuhusu mirathi

mbwadinho

Senior Member
Jun 29, 2016
180
102
Habari zenu wakuu naomba kuuliza mimi na mdogo wangu tulipata mgao wa mirathi kila mmoja alipata nyumba 1 na nyumba nyingine 1 tulishare sasa hati zote za nyumba alichukua baba yetu mdogo kwasababu kwa kipindi hicho tulikuwa bado tunasoma vilevile tulikuwa bado wadogo sasa kwa sasa nimekuwa mtu mzima nina umri wa miaka 26 .Ajabu sasa nilipomfuata baba mdogo kwa ajili ya kuomba kukabidhiwa hati za nyumba yangu 1 anadai nisubiri kwanza bado mdogo wako anasoma chuo ingawa nilimwambia mbona kila mtu ana nyumba yake aliyokabidhiwa isipokuwa hiyo moja tuliyoshare na mdogo wangu kwann usinikabidhi hiyo moja wakati hiyo nyingine tukisubiri mdogo wangu amalize chuo .ajabu ni kwamba anakataaa anasisitiza mpaka mdogo wangu amalize chuo na chuo bado miaka 3 .Naomba msaada wenu wa hatua zipi za kisheria nifuate
 
Akikugomea unaweza kwenda mahakamani kuomba mahakama itoe amri ya kupatiwa hiyo hati. Nenda mahakamani baada ya njia za amani kushindikanika!
 
Kabla ya kwenda mahakamani washirikishe wazee na ndugu zako,hakikisha kwenye kikao unarecord kila kitu,ukishindwa wazee unaweza usisha viongozi wa kanisa au msikiti kulingana na imani yako,hakikiha mazungumzo yanarecordiwa..ukishindwa kote huko sasa utaweza kwenda mahakamani.
 
Niliwashirikisha ndugu lkn hakuna muafaka
 
Alafu suala la viongozi wa dini walisema tulifanye kifamilia kwakuwa huyo ni mzazi
 
Haya mambo ya mirathi busara isipotumika mtatengana jumla.

Kabla ya kupelekana mahakamani hakikisha njia zingine zote zimegonga mwamba.

Pengine Mzee hizo hati kachukulia mkopo bank.

Nna uzoefu na utengano uliosababisho na hii migogoro ya mirathi.
Bimkubwa alisukuma ndani ukoo mzima.
 
Sawasawa mkuu
 
Habari zenu wakuu naomba kuuliza mimi na mdogo wangu tulipata mgao wa mirathi kila mmoja alipata nyumba 1 na nyumba nyingine 1 tulishare sasa hati zote za nyumba alichukua baba yetu mdogo kwasababu kwa kipindi hicho tulikuwa bado tunasoma vilevile tulikuwa bado wadogo sasa kwa sasa nimekuwa mtu mzima nina umri wa miaka 26 .Ajabu sasa nilipomfuata baba mdogo kwa ajili ya kuomba kukabidhiwa hati za nyumba yangu 1 anadai nisubiri kwanza bado mdogo wako anasoma chuo ingawa nilimwambia mbona kila mtu ana nyumba yake aliyokabidhiwa isipokuwa hiyo moja tuliyoshare na mdogo wangu kwann usinikabidhi hiyo moja wakati hiyo nyingine tukisubiri mdogo wangu amalize chuo .ajabu ni kwamba anakataaa anasisitiza mpaka mdogo wangu amalize chuo na chuo bado miaka 3 .Naomba msaada wenu wa hatua zipi za kisheria nifuate
Unakimbilia wapi wakati ulikuwa unakula kwa Baba yako mdogo. Mbona hukudai ukiwa mdogo. Acheni uchu
 
Kwa sasa nyumba iko chini yako? I mean kama kuishi unaishi hapo au kama imepangishwa ni wewe ndio unachukua kodi?
 
Nyumba ya mtu aliyefariki ni ya mke na watoto wake, siyo ya kaka ama dada zake. Jamani - tafuteni pesa mjenge nyumba zenu, siyo kusubiri kaka zenu waondoke mlete taabu kwa wajane na watoto wao.

Baba mdogo kama anakatalia hati ameharibu mahusiano yeye mwenyewe. Kwa hiyo wewe usijali mahusiano. Kama angekuwa anajali mahusiano, asingekatalia hati. Miaka 26 wewe ni mtu mzima. Ungekuwa chini ya 18 hapo hata sheria ingesema wewe ni mtoto. Anzia kwenye ukoo/dini kama ulivyoshauriwa. Ikishindikana sheria ipo. Hata watoto wa Mengi wameamua kufuata njia hiyo.
 
Nyumba ya mtu aliyefariki ni ya mke na watoto wake, siyo ya kaka ama dada zake. Jamani - tafuteni pesa mjenge nyumba zenu, siyo kusubiri kaka zenu waondoke mlete taabu kwa wajane na watoto wao.

Baba mdogo kama anakatalia hati ameharibu mahusiano yeye mwenyewe. Kwa hiyo wewe usijali mahusiano. Kama angekuwa najali mahusiano, asingekatalia hati. Miaka 26 wewe ni mtu mzima. Ungekuwa chini ya 18 hapo hata sheria ingesema wewe ni mtoto. Anzia kwenye ukoo/dini kama ulivyoshauriwa. Ikishindikana sheria ipo. Hata watoto wa Mengi wameamua kufuata njia hiyo.
Sawa mkuu nashukuru kwa ushauri
 
Hata mdogo wako kama yupo chuo anayohaki Kudai hati hiyo . Ikishindikana sheria zipo wazi
 
Back
Top Bottom