Msaada wageuka shubiri baada ya kupaki kiumbe cha ajabu maeneo ya fukwe

Pilot_In_Command

JF-Expert Member
Nov 10, 2013
2,507
3,406
Kabla ya Tukio

Nilikuwa nimetoka safarini.. Uchovu na kulimiss jiji la Dar ilibid nipitilize katka moja ya Beach maarufu hapa Dar.. Ilikuwa mida ya saa 11 jioni.. Siku ya jumatano.. Watu hawakuwa wengi, hasahasa wazungu na wengne walikuwa wanafanya Mazoezi..

Kutokana na tabia yangu ya kuingiza gari mpaka ufukweni kuliniletea shda kdog wakati nataka kuondoka.. Gari iligoma kuwaka na ukizingatia imetoka safari ndefu.. Injini ilipata jotokali so sikuweza kugusa kitu nikisubiri ipoe huku napata mziki na miogo ya ufukweni.. Nilikuwa mwenyewe tu.. Sikupata wasiwasi kutokana na ile gari inakatatizo fulani katk mfumo wake wa umeme so nilijipa moyo nitagusa hapa nitagusa pale itawaka!


MUDA UNAZIDI KUYOYOMA.. Saa 2 usiku inaenda saa 3.

Hapa nikaanza ufundi mdogo mdogo.. Kila nikitekenya gari haiwaki.. Kusukuma Nissan Patrol katk mchanga wa bahari sio kitu chepesi! Nilijitahdi sana ikbd ninyooshe mikono.. Simu inakarbia kukata moto ..."niliitumia kama tochi kwa muda mrefu".. Muda unazd kwenda.. Mpaka kufika saa 4 usiku natoka jasho sina cha kufanya.. Na watu wanazidi kupungua.. Wauza miogo nao wanafungasha virago.. Nikajisemea.."leo kazi ninayo"

baada ya muda kupita.. Nikapiga moto direct.. Kumbe fuse ilikuwa imekufa mzgo ukawaka.. Nikawa naelekea baharini kunawa niondoke..

SAA 5.. Kasheshe lilipoanza..

Niliporud nilikuta gari inawaka kama kawaida nikaingia na kuanza safari.. Wakati nageuza nilimuona mdada kakaa ktk benchi peke yake.. Sikujali.. Niliendelea na kugeuza gari nikatoka ufukweni mpak katika lami..

Nilitembea mita chache nikamkuta yuleyule dada anatembea pembeni kwa mwendo wa kuchechemea (sikuwaza amefikaje huku wakati nimemuacha ufukweni tena nikiwa na gari yeye akiwa hana dalili za kuondoka)

niliminya breki.. Nikaweka chuma pembeni.. Alipita gari na kuendelea tu kutembea.. Ah nikamfata na kupiga honi alisimama na nikamuonesha ishara ya ingia..

Msichana mrembo tu na mavazi yake ya rangi nyekundu na nyeupe kwa mbaali.. Nilimuongelesha lakn alijibu kwa kutikisa kichwa na kunikazia macho.. Ah sikuwaza nilitak nimsogeze mpaka barabara kuu..

Kwa kuwa alikaa siti ya nyuma.. Nilipata shda sana kugeuka geuka .. Baada ya muda niliona hali isiyoyakawaida..

Gari niliiona ikiwa nzito.. Nilifika ktk kituo cha mafuta nikaweka wese.. Mhudumu akaniambia "naona chuma imeshba mzgo!" ah sikumjibu nilitia gia nikasepa.. Kasheshe linakuja namuuliza unashuka wapi? "zilitoka sauti nne kwa mpigo zikisema tushushe hapa hapa..tena kwa ukali wa hali ya juu!

Dah ndg zangu nilikuwa ktk spd ya 130/kph.. Ilibid niyumbe kdg.. Nikaiweka gari sawa nikapak pembeni.. SIKUMBUKI KILICHOENDELEA..

Asubuh mida ya saa 3 asbh nagongewa dirishani na mlinzi.. Namuuliza kuna nini kimetokea? Akanijibu "tangia saa 7 niliona watu kama nane wakishuka humu wote wakiwa wamevaa nguo zisizoeleweka za kuwakawaka.. Akanambia nilidhan wametelekeza gari.. Akanirudishia swali.. Kwan wale wakina nan? Sikumjibu gari ilikuw inawaka bado na cha kushangaza sina jeraha lolote.. Ingawa nilipata Usingizi mzto mno..

TUWE MAKINI usiku..
 
Driving mirror.. Usiku haisaidii maana giza ingawa taa za barabarani ziliingiza mwanga mule.. Ugumu pia alipopanda alikaa nyuma ya siti yangu yaan alijibana upande wa kulia.. Ndo hapo nikawa nawas wasi wa kugeuka geuka.
 
Coco beach iyo noma saana usiku kunakuwaga na vikao mule pembezoni mwa bahari.

Kuna muuza miogo mmoja alinihadithia alikua kafunga biashara yake kama kawaida akaondoka kufika njiani akagundua kuna kitu kasahau ile kurudi akakuta kuna watu wengi sana wanakula na kunywa maeneo yao pale wanapopika mihogo
 
Mr Nyambiza..

Sijajua kwa coco beach.. Huwenda na huko kuna shda pia..

Mie nilikuwa maeneo ya 'Open beach' kule.. Kuna minazi kadhaa pemben kuna kibanda cha miogo
 
Mwanaka.. Shukuru Mungu sana... DUNIA ni pana bado najifunza mengne siyajui yaliyojificha zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom