Msaada: Wadudu wamekula mbao za dari, paa linataka kudondoka. Mtaalamu wa dawa anisaidie ushauri

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
4,494
2,000
Eneo nililopo lina mchwa sana. Mchwa ambao unaweza kuangamiza paa la nyumba ndani ya miaka chini ya kumi. Najitaji kutibu mbao za kujengea, kwani huku hakuna watu wanaouza mbao zilizotibiwa.
Naomba msaada wako wa mawazo juu ya aina za dawa, matumizi yake, na bei. Mawazo yako ni muhimu sana.
 

HGYTXK

Senior Member
Oct 3, 2011
194
170
Upo maeneo gani?,huku Mtwara tunatumia sana mafuta yanayotokana na maganda ya korosho kutibu hilo tatizo,unazipaka mbao kabla haujazitumia na hakuna mdudu atakayeziharibu. Kwa kawaida lita moja ya hayo mafuta uuzwa kati ya elfu 3 hadi elfu 5 kulingana na msimu wa upatikanaji wake. Kama upo Dsm ulizia kama kuna kiwanda chochote cha kubangua korosho kisha waulizie kama kuna wanaochoma hayo maganda kwa ajili ya mafuta.
 

kivyako

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
14,342
2,000
Nami kuna wadudu flan wanakula mbao za dari hatari japo nilinunua ambazo ziko treated, unacheki unga unamwagika tu na wanasikika wanapokuwa wanatafuna ndani kwa ndani, mpaka kero, mwenye ushauri tafadhali.
 

komamgo

JF-Expert Member
Sep 14, 2012
1,653
2,000
Hili tatizo lilisha tatuliwa kwa kuezekea kenchi za chuma basi!!!!!!
Asikudanganye mtu .Huna jinsi ezua paa na weka chuma.
Gharama za chuma ni 100,000/-kwa kenchi katika span ya 40ft. Kwa kenchi moja.
Zinduka ndugu.
 

The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,409
2,000
Hili tatizo lilisha tatuliwa kwa kuezekea kenchi za chuma basi!!!!!!
Asikudanganye mtu .Huna jinsi ezua paa na weka chuma.
Gharama za chuma ni 100,000/-kwa kenchi katika span ya 40ft. Kwa kenchi moja.
Zinduka ndugu.

Sasa ndugu yangu usifikiri kila mtu anauwezo huo, anajipiga anapoweza kwanza uweke kenji ya chuma kwani huo ni Ukumbi wa mikutano?
Kenji ya chuma kwa nyumba ya kuishi mbona naona haijakaa poa na wengine hebu tusaidieni hii KENJI YA CHUMA KWA LEAVING.HOUSE
 

Mungu Mweusi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
1,472
2,000
Mtafute mtaalamu wa dawa za usingizi nearest Hosp.awafunze adabu awapige kaputi ya Mwaka mzima
 

Enzymes

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
4,340
2,000
mimi ni fundi, ilikuwa rahisi kama ningekuwepo wakati wa kupaka hiyo dizeli, sio kupaka tu. kuna jinsi ya kufanya, mi nilijifunza kwenye kampuni ya wayugoslavia (partizansk put ya morogoro) wanatumia dizeli safi, mbao haichafuki na ina dumu
Fundi tusaidie siye wa huku mikoani namna gani tupake? (Msaada tafadhali)

Je kati ya Oil chafu, Disel safi na hiyo dragnet kwa uzoefu wako, unaona ipi inafaa zaidi?
 

Swat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,200
2,000
Ni Mbao za aina gani umetumia?kama ni Jamii ya crevilia au Mbao zenye Sukari ni bora kubadili Mbao zote za paa Kabila halijashuka.mimi nafanya kazi za carpentry,nimewahi kukutana na tatizo Kama Hilo almanusra nifunge Kiwanda sababu ilinichukua Mwaka mazima kufanya repair za bidhaa mbalimbali zilizokuwa zikirudishwa na wateja walionunua kwangu kwa kipindi cha miaka mitatu kabla na kukumbwa na tatizo hilo,nilijaribu dawa mbalimbali bila mafanikio mpaka nilipoamua kubadili mbao nilizotumia ndio ilikuwa suluhisho.Tabia ya huyo mdudu ni kwamba anakula mbao mpaka inapoisha ndio mwisho wa maisha yake,na ilivyo ni kama anajitengeneza tokana na mbao kama alivyo mdudu wa kokwa la embe,hivyo suluhu ya uhakika ni kubadili aina ya mbao ulizotumia,pole sana.
Aksanteni kwa ushauri.
Nami nyumba yangu moja ina tatizo hilo!
 

Chabo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
986
1,000
Hata mm nina tatizo hili..huwa najiuliza hawa wadudu wanaingiaje kwenye mbao..maana ukifanikiwa kumtoa kwenye mbao ni mkubwa kama funza lkn huwezi kuona alipopitia!!!!
 

Kichoi

JF-Expert Member
Apr 13, 2014
212
195
Hili Tatizo hata mimi limenikumba. Nasikitika kusema kuwa wauzaji wa hizi mbao wanasema ni Treated lkn kiuhalisia haziko treated, wanatutapeli hela zetu kwa kutuuzia mbao ambazo zimechovya kwenye dawa lkn hazija chemshwa na dawa.
Mti kwa kawaida una Starch au wanga ambao ndio kivutio kikubwa cha wadudu. Tunapo chemsha mbao tunaondoa hiyo starch na kufanya ubao/mbao kukosa starch ambayo ni chakula cha wadudu.
Hiyo Diesel na Oil chafu inaeeza kuzuia lkn ipamkwe mapema kabla ya mbao/ Kenchi kupigwa. Diesel na Oil Chafu inasaidia kukata supply ya oxygen endapo mdududu atataka kushambulia au akiwa ndani.
 

Chabo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
986
1,000
Nashukuru kwa ushauri wako mkuu...hata mm nawalaumu sana hawa wauzaji wa mbao treated(feki).ni bora zisingekuwepo kbs ili watu tujihami na oil au deasel maana naona inasaidia sana kiliko hizi treated uchwara.ok nimeona umezugumzia mdudu kukosa oxygen akiwa ndani ya mbao..je!kama mbao imekwisha anza kuliwa na wadudu kuna uwezekano wa kuwadhibiti wasiendelee kula kwa kupaka hiyo oil au deasel ???
 

Dengue

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
1,811
2,000
Hili Tatizo hata mimi limenikumba. Nasikitika kusema kuwa wauzaji wa hizi mbao wanasema ni Treated lkn kiuhalisia haziko treated, wanatutapeli hela zetu kwa kutuuzia mbao ambazo zimechovya kwenye dawa lkn hazija chemshwa na dawa.
Mti kwa kawaida una Starch au wanga ambao ndio kivutio kikubwa cha wadudu. Tunapo chemsha mbao tunaondoa hiyo starch na kufanya ubao/mbao kukosa starch ambayo ni chakula cha wadudu.
Hiyo Diesel na Oil chafu inaeeza kuzuia lkn ipamkwe mapema kabla ya mbao/ Kenchi kupigwa. Diesel na Oil Chafu inasaidia kukata supply ya oxygen endapo mdududu atataka kushambulia au akiwa ndani.

Hawa wauza mbao ambao sio waaminifu ni majipu. Inabidi wakaguliwe mara kwa mara na kuwe na nfumo wa kutambua mbao ambayo imekuwa treated.
 

kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,975
2,000
Kweli kuna haja ya kuwa na namna yakutambua mbao ambayo imetibiwa vizuri ili kuweza kukwepa hizi hasara.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom