Msaada wadau, utaratibu wa kuanzisha kampuni binafsi ya upelelezi

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,261
Salam wadau,

Kati ya vitu ambavyo ilikuwa ndoto yangu tangu utotoni ni kufanya kazi za kijasusi, ila kwa bahati mbaya au nzuri sikufanikiwa. Sasa baada ya juhudi zangu binafsi nimefanikiwa kwa kiasi fulani kupata mafunzo na mbinu kadhaa za kufanya kazi hiyo ya kijasusi.
Ila kwa bahati mbaya baada ya kushiriki na kumaliza hayo mafunzo nimeshindwa kuyatumia na hatimaye hadi sasa sijapata kuona manufaa yake baada ya kushindwa kuomba kazi kwenye taasisi zinazohusiana na kazi hizo hususani jeshi la polisi na usalama wa taifa, kwa kuwa hawana utaratibu wa kuajili watu kwa kazi hizo, ila wanachofanya ni kufundisha watu wao kwa ajili ya kazi hizo.

Sasa baada ya kutafakari hilo nimeamua kufikiria kuanzisha kampuni ambayo itajishughulisha na kufanya upelelezi kutokana na mahitaji ya muhusika, Sasa kwenye hilo ndipo ninahitaji kujua

1. Je katiba yetu inaruhusu kuanzishwa kwa taasisi binafsi itakayo jishughulisha na upepelezi

2. Kama inaruhusiwa je ni wapi pakuanzia ili nikamilishe hili, na gharama na mahitaji yake zikoje

Noambeni msaada wenu katika hili

JoJiPoJi
 
Mmh sina majibu ya maswali yako ila mawazo yako nimeyapenda.Japo hujasema uchunguzi wako utabase kwenye nini zaidi...mahusiano (kukamata wadanganyifu)...kutafuta waliopotea...kutrack wezi/majambazi au?!
 
Anzisha kampuni ya kupeleleza wanandoa hii inalipa sana jamaa wengi wamanufaika sana na hii kazi ya upelelezi.
 
Kila la kheri!
Ahsante

Mmh sina majibu ya maswali yako ila mawazo yako nimeyapenda.Japo hujasema uchunguzi wako utabase kwenye nini zaidi...mahusiano (kukamata wadanganyifu)...kutafuta waliopotea...kutrack wezi/majambazi au?!
Naona nitajihusisha sana na makosa makubwa kama ya ujambazi, utapeli, cyber crime licha sina uhakika kama kwenye hili nitakuwa na wateja

Anzisha kampuni ya kupeleleza wanandoa hii inalipa sana jamaa wengi wamanufaika sana na hii kazi ya upelelezi.
Mkuu cha msingi ni kuweza kwanza kukamilisha utaratibu wa kuanza kazi hayo mengine yatajitokeza kutokana na mahitaji
 
Mkuu wazo lako ni zuri sana. Kama mawakili binafsi na makampuni binafsi ya ulinzi yanaruhusiwa, nafikiri na wapelelezi binafsi wanaruhusiwa pia. Kama hawaruhusiwi ni muda muafaka kuliweka jambo hilo kwenye katiba mpya. Sehemu zingine tunasikia wapo wapelelezi binafsi wanaofanya kazi kwenye makampuni ya bima ili kubaini udanganyifu wa wateja wanaodai malipo bogus!
 
biashara hiyo ipo na inaruhusiwa, zipo kampuni zinazofanya hizo shughuri hapa bongo kwa mfano wacheki hawa jamaa wa TPIA

Tanzania Private Investigation Agency
If you have any enquiry, question or need an advice on any of your personal problems we will be glad to help you, our Numbers are open 24 hours a day and we work all seven days a week. Our Agent will provide a free consultation on phone. You can also write an electronic mail to the provided e-mail address below
Telephone:022 2760 724Mobile: 0713 240 856Calling from out of Tanzania dial +255 22 2760 724Mobile: +255 713 240 856 P.O.Box 61854Dar es SalaamTanzania (East Africa)E-mail: info@tzprivateinvestigationagency.comClick here to chat online with our Agent
 
Ndugu umenisaidia sana, sasa ninapo pakuanzia ila bado maoni na ushauri muhimu katika kipindi hiki
 
Mkuu utafanya kazi na nani nchi hii au nchi za dunia ya tatu? Kwa hakika utafungua ofisi yenye meza na kila kitu ila viti itakuwa ni hayo mafaili ya kesi. Kwa kazi hiyo utategemea sana ushirikiano wa jeshi la polisi na wanasiasa (kwa hali halisi ya nchi yetu) ambao ni wala mlungula wakubwa. Labda uwe kama mawakili wetu wanavyokula huku na huku.
 
Ndugu umenisaidia sana, sasa ninapo pakuanzia ila bado maoni na ushauri muhimu katika kipindi hiki
Mmmmh, kwa harakaharaka naona hii kampuni (kama ipo, maana sijaona physical au postal address yao) inashughulika na consultation tu sio investigation! Kisheria sijapata kuona au kusukia kitu kinaitwa "Pivate Investigation" ila kuna kitu kinaitwa "Private Prosecution!" Mambo ya upelelezi yako very complicated na hakuna Sheria inayoruhusu Private Investigation, especially kwa Makosa ya Jinai!
 
kweli ni watu wengi tuliokuwa tumeharibiwa akili na vitabu vya Joram Kiango na Willy Gamba pia snema za James Bond 007
 
Salam wadau,

Kati ya vitu ambavyo ilikuwa ndoto yangu tangu utotoni ni kufanya kazi za kijasusi, ila kwa bahati mbaya au nzuri sikufanikiwa. Sasa baada ya juhudi zangu binafsi nimefanikiwa kwa kiasi fulani kupata mafunzo na mbinu kadhaa za kufanya kazi hiyo ya kijasusi.
Ila kwa bahati mbaya baada ya kushiriki na kumaliza hayo mafunzo nimeshindwa kuyatumia na hatimaye hadi sasa sijapata kuona manufaa yake baada ya kushindwa kuomba kazi kwenye taasisi zinazohusiana na kazi hizo hususani jeshi la polisi na usalama wa taifa, kwa kuwa hawana utaratibu wa kuajili watu kwa kazi hizo, ila wanachofanya ni kufundisha watu wao kwa ajili ya kazi hizo.

Sasa baada ya kutafakari hilo nimeamua kufikiria kuanzisha kampuni ambayo itajishughulisha na kufanya upelelezi kutokana na mahitaji ya muhusika, Sasa kwenye hilo ndipo ninahitaji kujua

1. Je katiba yetu inaruhusu kuanzishwa kwa taasisi binafsi itakayo jishughulisha na upepelezi

2. Kama inaruhusiwa je ni wapi pakuanzia ili nikamilishe hili, na gharama na mahitaji yake zikoje

Noambeni msaada wenu katika hili

JoJiPoJi

Lengo la upelelezi/uchunguzi ni kupata ushahidi (evidence) ambao unawaza kutolewa mahakamani na kuthibitisha kutendeka kwa kosa au la. Wazungu wanasema 'The aim of investigation is to prove or disprove allegations'; hivyo mwisho wa yote utaishia kutoa ushahidi mahakamani, sasa je ni nani atakuwa mteja wako? Kwa makosa ya Jinai wapo wapelelezi ambao wapo kwa mujibu wa sheria hivyo hata akifika mahakamani inafahamika hivyo na anaheshimika kwamba ni mtaalam wa kuisaidia mahkama kufikia maamuzi ya haki. Ni wazi kuwa serikali haiwezi kuitumia kampuni yako hata kama imesajiliwa BRELA na kwingineko. Kwa mashauri ya madai, ni wazi kuwa wateja wako wanaweza kuwa wananchi wa kawaida, hata hivyo utakapofika kotini utakutana na mawakili ambao watakuchanganya vya kutosha!

Ni wazo zuri lakini nadhani biashara hii haitakulipa sana. Nakushauri ujifue zaidi kielimu japo sifahamu umeishia level gani ili ufungue kampuni ya ushauri (Consulting firm) ya masuala ya upelelezi/uchunguzi. Kampuni hiyo iwe na uwezo mkubwa wa kufundisha wapelelezi wa aina mbalimbali kuhusu mbinu za kisasa za kupambana na uhalifu na udanganyifu wa aina mbalimbali. Wateja wako sasa watakuwa ni hao Polisi, Uhamiaji, PCCB, TRA na wengineo wanaohitaji kunoa wapelelezi wao. Nadhani kwa huu mpango utakuwa umeitendea haki nafsi yako.
 
kunamtu namfahamu amemaliza degree ya sheria ruaha university college ipo iringa alifanya research inayousiana na suala hilo nakushauri nenda ruco ruco library itafute reseach ya makishe,kama nitaipata soft nitakutumia hongera wazo zuri kiongozi
 
Back
Top Bottom