Msaada wadau kuhusu namna yakupatikana GPA

Vella

Senior Member
Nov 16, 2016
165
250
Ndugu habarini za asubuhi, naomba kueleweshwa kwa wale waliokwisha kuhitimu chuo kikuu, eti G.P.A ya mwisho wanachukua ile ya semister ya mwisho ya mwaka wako wa mwisho au wanachukua jumla ya ufaulu (G.P.A) ulizopata tangu first year nakuzijumlisha kisha wakagawa kwa idadi ili wapate mean av. Ya G.P.A ya jumla kwa miaka yote 3?
 

expedition

JF-Expert Member
Jul 16, 2016
690
1,000
Hapana.
Huwa tunachukua credit za somo husika tunazidisha na point za grade ulopata then unatafuta total kwa masomo yote alafu unagawanya kwa jumla ya credit zote.
Mfano A=5 B+=4 B=3 na C=2
first year
DS labda ina credit 2 na ulipata A so inakuwa ni 2×5 = 10
Communication 3 na una B+ 3×4 = 12
ICT 4 na una A 4x5 =20
second year
ecology 5 na una A so n 5x5=25
GIS 4 na una C = 4×3=12
Quantitative 5 na una B 5×3=15
third year
Research 5 na una B+ 5×4=20

then unachukua 10+12+20+12+15+20=89
gawanya kwa 2+3+4+5+4+5+5=28
so ni 89/28 =3.17 ila baadhi ya vyuo huchukua kiwango kimoja tu cha desimali ambapo itakuwa ni 3.1 huwa hatu estimate eti iwe 3.2.
hiyo ni njia ndefu japo unaweza chukua jumla ya credit ulizopata 1st year ukajumlisha na za 2nd year na 3rd year ata mwaka wa nne kama upo then ukagawa kwa jumla ya credit hours kwa masomo yote usije tafuta wasitani wa GPA zako kwani baadhi ya masomo huwa na credit nyingi na mengine ni chache unaweza kuta first year una GPA ya 5 kumbe masomo yana credit ndogo sana alafu second year una 2.7 alafu credit zake ziko juu sana so lazima iyo 5.0 ya first year imezwe kwenye second year
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom