Msaada wa wazo la biashara

Tractor

Member
May 23, 2019
55
125
Wakuu naomba kupata wazo la kufanya biashara zaidi ya moja wakati nikiwa kwenye kaduka kangu.
Nilianza udalali wa magari na viwanja ila nilkkosa network, pia ninayo Gari ndogo raumu ila nakuja nayo Kwenye duka langu narudi, siyo mbali na nyumbani, sasa shida inakuja ni kuwa kipato Ninachokipata ni kidogo.

Niliwaza kusambaza mayai ila bado niliona gharama kusambaza kwa gari. Mimi nipo Dar wakuu, naombeni sana sana ndugu zangu nisaidieni wazo, nitashukuru sana kama mtanisaidia.
 

dingihimself

JF-Expert Member
Jan 9, 2016
9,232
2,000
Duuh ok..!
Why madereva huwa wanalalamika na uswahili mwingi kwenye masuala ya hesabu ya week?
Huo si uhuni tu, kwa maboss wao na unakuta wengine wanabanwa sana

Nina rafiki yangu alipiga uber kwa boss mmoja ndani ya mwaka akamuachia yule jamaa gari yake, alikua ka make tsh 6,000,000 akatafuta ist kwa bei hiyo anapiga nayo kazi sasa.
 

6Was9

JF-Expert Member
Mar 2, 2021
1,594
2,000
Huo si uhuni tu, kwa maboss wao na unakuta wengine wanabanwa sana

Nina rafiki yangu alipiga uber kwa boss mmoja ndani ya mwaka akamuachia yule jamaa gari yake, alikua ka make tsh 6,000,000 akatafuta ist kwa bei hiyo anapiga nayo kazi sasa.
Nimekupata vyema mkuu.. !
Hata mimi hilo suala la hawa jamaa kupenda kulalamika ni uhuni, kuna dogo nilimuachia biashara fulani aifanye kwa hesabu ya week .. siku akiuza sana anatumbuwa hela siku moja tu itokee mambo yameenda vibaya atalalamika mwezi mzima biashara ngumu.

Kwa ufupi they don't care about you or your business.. anapambana kivyake na yeye achomoke hapo haijalishi hata kama anakuumiza!
 

Reginald L. Ishala

JF-Expert Member
Jun 18, 2011
3,823
2,000
4.Kodi/nunua mashamba Kanda Ya Ziwa au Nyanda za Juu Kusini,

Kisha limisha mpunga, maharagwe, ngano, dengu, tangawizi, Vitunguu maji na swaumu, viazi mbatata, na mihogo myekundu. Hutojuta.

AU: Subiri muda wa mavuno uanze, Langua nafaka tajwa hapo juu halafu uza kwa kilo au subiri yaadimike toa stoo upige bingo mara 3-4.
 

Reginald L. Ishala

JF-Expert Member
Jun 18, 2011
3,823
2,000
5.Nenda Kanda Ya Ziwa, Chukua kibali na leseni ya uchomaji/uuzaji mkaa.

Gharama ya kibali na leseni ni 60K/270K Jumla ni kama 330K.

Labda unaanza na gunia 10X15=150K Ukijumlisha na 330K=480K na usafiri ni 1 sack per 5000X10=50K, kwa hiyo utaanza na mtaji wa sh 600K by estimation.

UKIUZA GUNIA 1 BEI YA JUMLA NI SH 50K au 52K au 56K, Tunafanya hivi:-

Ndoo 1 ya lita 20 [debe 1 la mkaa] inauzwa sh 7.5K pengine 8K, Sasa gunia dogo ni debe 6X8=48K, La kati linabeba debe 7X7.5K=52.5K au 7X8K=56K wakati wewe ulinunua gunia 1 moja kwa 15K au 20K kama limepanda.

HATA: Ukiuza kwa ndoo ya lita 10 yaani nusu debe kwa sh 4-5K bado unakula vichwa kwa faida shazi.

Hata ukiuzwa makopo ya GOLD STAR au COLOR PAINT kwa buku kila kopo la mkaa, Bado faida ni shazi.

NOTE: Kama hunywi "pombe" wala hupendi sana "sketi" basi utapiga ankara ya kutakata.
 

Reginald L. Ishala

JF-Expert Member
Jun 18, 2011
3,823
2,000
6.Kata kibali cha kuchezesha PS "PLAYSTATIONS" ile michezo ya ma games ya ngumi na mpira.

Weka ofisi hizo maeneo ya uswahilini na mjini kati uone utakavyokula bingo.
 

Reginald L. Ishala

JF-Expert Member
Jun 18, 2011
3,823
2,000
7.Fungua kijiwe cha tangawizi, chai, maziwa, mayai, maji, soda, chipsi, Weka tangawizi kikombe sh 200.

Maziwa ambayo hayajafanyiwa fanya kikombe sh 300.

Chai kikombe sh 100. Tumia viungo tu kama mchaichai, hiliki, mdalasini na viungo vya Kiarabu tu wala usitie majani ya kiwandani.

Weka maandazi, chapati, karanga zote, Mihogo ya kukaangwa/kupikwa na mibichi na kashata na ufuta.

Weka TV, King'amuzi cha Azam, Deki, na Flash ya movies au CD na mpira.

NOTE: Weka kibao nje au pembeni kikionyesha menu za vinywaji, kapile na vyakula ulonavyo sanjari na ratiba ya mpira wa siku hiyo au movies za siku hiyo bure kwa wateja.

Umekula bingo mkuu.
 

Reginald L. Ishala

JF-Expert Member
Jun 18, 2011
3,823
2,000
8.Fungua huduma ya water supply, Nenda idara ya maji jisajili na ulipie wakuvutie bomba.

Ukiwa nyumbani, Uza maji kindoo kidogo (lita 10) ni sh 50 na ndoo kubwa [ya lita 20] ni sh 100 kule Lake Zone sijui bei ya Dar.

Chongesha toroli 5 kodisha toroli 4 kila moja kwa siku ni sh 1000.

Halafu toroli 1 ilobakia ni yako usiikodishe, Nenda nyumba kwa nyumba uwaombe uwe unawasambazia maji kwa toroli wanakulipa au weka kijana kama unaona soo.

NOTE: Bei ya kutengeneza toroli moja kwa nondo na bomba ni sh 70K, Kwa matano ni 5X70K=350K gharama ya kuchomelea matoroli matano.

Gharama ya kuvuta bomba la maji kule Lake Zone kama haijapanda ni sh 150K ila hapo haujaweka vifaa vingine unaweza kuazima. Baadhi ya vifaa ni kama pipe wrench, tape, praizi/katapraizi, koki, mpira, connector, ulaji wa fundi, n.k.
 

Master Kutu

Member
Jun 8, 2021
77
150
Wakuu naomba kupata wazo la kufanya biashara zaidi ya moja wakati nikiwa kwenye kaduka kangu.
Nilianza udalali wa magari na viwanja ila nilkkosa network, pia ninayo v
Gari ndogo raumu ila nakuja nayo
Kwenye duka langu narudi, siyo mbali na nyumbani, sasa shida inakuja ni kuwa kipato Ninachokipata ni kidogo, niliwaza kusambaza mayai ila bado niliona gharama kusambaza kwa gari.
Mimi nipo dar wakuu, naombeni sana sana ndugu zangu nisaidieni wazo, nitashukuru sana kama mtanisaidia.
Kuna Ideas nyingi na nzuri kwa mtaji mdogo ila faida kubwa,sasa unahitaji wazo linalo lenga biashara gani?

1.Commodity Business

2.Expect Business
 

Master Kutu

Member
Jun 8, 2021
77
150
Mkuu naomba utupe idea zote mbili itapebdeza nawasilisha
Hapo mkuu ni muhimu muhusika ajue ana taka afanye biashara gani kati ya hizo mbili maana tunapo sema

Commodity Business

Ni kwenda kuchukua bidhaa kwa wauzaji wa jumla afu wewe unaenda kuuza ili upate faida.

Expert Business (Entrepreneurship)

Kwanza una angalia jamii unayo ishi ina changamoto gani inayo wasumbua na hakuna solution iliyopatina ama kama ipo haija fika kwa watu wengi.

Wewe una enda kutafuta suluhisho la hiyo changamoto then una address tatizo lao ili uweze kuwa uzia suluhisho ulilo nalo.

Sasa hapo before huja pewa Idea ninge penda nijue una lenga biashara gani na pia kama kuna jambo unalijua naweza kukupa changamoto yake ili uweze kuuza solution katika jamii ya Watanzania then utengeneze pesa kwa mtaji mdogo na nguvu kidogo tu but maarifa zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom