Msaada wa utofauti wa maneno mawili ya (English) RICH AND WEALTH

akatanyukuile

JF-Expert Member
Sep 13, 2019
315
500
Kama inavosomeka hapo juu kwenye pitapita zangu za kusaka maarifa ya kidunia nimekutana na maneno hayo mawili yakionesha utofauti mkubwa.

Katika utofauti wa hayo maneno walienda mbali zaid na kuonesha yakua rich mwisho wake ni umasikini na wealth mwishowake ni good life.

Sasa nikajiuliza unaweza kua wealth bila kua rich? Wataalamu wa Economics tusaidizane kidogo asante na karibuni
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
8,329
2,000
Kwa uelewa wangu, naweza kutumia ukwasi na utajiri kutafsiri rich na wealth.
Ukwasi unaweza kuwa na kiasi kikubwa cha pesa mkononi, ambayo usipokuwa muangalifu, inaweza kupukutika na ukajikuta katika umasikini.
Utajiri, licha ya kuwa na pesa, pia unakuwa na mali zinazozalisha kipato na kukufanya kwa hali yoyote Ile usiwe na uwezekano wa kufilisika, na utajiri au wealth unaweza kurithiwa kutoka kizazi hadi kizazi hata kama kizazi kijacho kisipotoka jasho, kitafaidika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom