Msaada wa ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa ushauri

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Jalalasam, May 21, 2010.

 1. J

  Jalalasam New Member

  #1
  May 21, 2010
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba ushauri,kama mtu hakufanya vizuri form four akipata Div four,sasa amesoma kozi ndogo ndogo mpaka kufikia level ya Adv Dip,je hiki cheti cha form four kinatia aibu,je kwenye kuomba kazi nikitumie au kuna haja ya kurudia mitihani ya form four?

  Naomba tafadhali ushauri na sio kupondea.

  Asante
   
 2. E

  Exav Member

  #2
  May 21, 2010
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mkuu Jalalasam,

  Sioni kama una sababu ya kuwa na wasiwasi. Kwa kuwa ulifanya hizo kozi ndogondogo, bila shaka ulipata vyeti vyake, hivyo uombapo kazi tumia vyeti hivyo hivyo including hicho unachohisi kinatia aibu. Kama una nia ya kurudia mitihani ili kusafisha cheti chako, nakuunga mkono - fanya hivyo. Lakini usisite kuomba kazi kwa kutumia vyeti ulivyo navyo kwa sasa.

  Kila la kheri!
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Best fuata tu job advert inasemaje ila nathani kwa ajira nenda na vyeti vyako vya kozi wakihitaji cheti cha four wape!
   
 4. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2010
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Mara nyingi waajiri wanaangalia vyeti vyako vya juu au vya hivi karibuni. Hivyo kama una Adv Dip huna haja ya kupeleka cheti chako cha form 4 na wala usifikirie kufanya mitihani wa form 4 tena. Daima mbele nyuma mwiko!! Na kama watakihitaji, sioni kama itakunyima kazi!!
   
 5. J

  Jalalasam New Member

  #5
  May 25, 2010
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru wote kwa ushauri mzuri mlionipatia na ahidi kuufanyia kazi
   
 6. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2010
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Kama umri unakuruhusu na ndio kwaanza unaingia kwenye ajira, nakushauri kurudia mitihani taratibu ili kukifanya kiwe kizuri ambacho hutakionea shida kukitoa. Huko mbele uendako kwenye elimu utatakiwa uwe umefaulu masomo kadhaa kwa cheti hicho na ndipo hapo itakapokuwa taabu, lakini kama utakuwa umesawazisha kwa sasa utajikuta unapeta tu kila hatua unasonga mbele. Nakuhakikishia baadae, hutaweza kusonga mbele kielimu na cheti hicho kwa baadhi ya vyuo vyetu vikubwa, mimi mmoja wa waliokwama kwa sababu hiyo na sasa nimejichimbia kwenye kufuga wanyama maana umri umekwenda japo elimu haina mwisho, naona taabu after all the years kuanza kurudia masomo. Kila la kheri!
   
Loading...