Msaada wa Ushauri!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada wa Ushauri!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Akili Unazo!, May 29, 2009.

 1. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,809
  Likes Received: 2,513
  Trophy Points: 280
  Nina rafiki wa kaka yangu ambaye ana umri wa miaka 45 na ameoa na kubahatika kuwa na watoto wanne,wa kwanza ana miaka 18 kwasasa na wa mwisho ana mitano.Baada ya kupata hao watoto wote kwa pamoja walikubaliana kuwa idadi ya watoto walio nao inatosha hivyo wasiendelee na zoezi la uzazi tena.Hivyo wakawa wanatumia Contrception ya sindano kwa muda wa miaka minne sasa.

  Sasa katika kipindi kisichotegemea huyu ndugu mkewe mwenye miaka arobaini sasa amepata/conceive na mimba yake kwa sasa ina miezi minne.

  Kinachomtatiza huyu ndugu ni kwamba haikuwa mategemeo yake kupata mtoto mwingine kwa sasa na hayupo tayari kabisa,wakati huohuo mama yake mzazi anafurahia kwa mkwe wake kubeba mimba na kusema ni baraka kutoka kwa mwenyezi mungu.

  Ndugu huyu amechanganyikiwa na kushindwa kuamua nini cha kufanya aache mkewe azae au aitowe.Kwa maamuzi yote hayo yanamchanganya kwa sababu alikuwa amepangilia kila kitu kwa ajili ya kusomesha watoto wake hao wanne na ndo nguvu nyingi alikuwa amezikweka huko kwa kila kitu.Amuzi la pili la kutoa mimba anachanganyikiwa kwa kuwa ndani ya miaka ishirini ya ndoa yake hajawahi kusikia wanandoa kutoa mimba hivyo uamuzi kuwa mgumu zaidi,na endapo ataamua kuendeleza uamuzi wa pili mama yake mzazi atamchukuliaje endapo akisikia kuwa mkwewe hana mimba tena?

  WanaJf nawasilisha kwa ushauri na mawazo.
   
 2. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mshauri arekebishe plan zake ataweza tu kum-accomodate huyo mtoto wa tano haitakuwa taabu sana. anataka kusema maisha yake ameya-program kiasi kwamba hakuna contingencies, je kama akitokewa na matatizo mengine ya kiafya ama kisheria?
  Kisha kutoa mimba miezi minne ina risks kibao including kufa; lakini pia kuna mambo ya psychosocial kama hivyo mama mkwe keshajua!
  alikuwa wapi mimba ilipokuwa changa?
  Mwisho mwambie ni dhambi kumporomosha huyo mtoto, atakuja kuchomwa moto mpaka a-blow. na hicho kitoto kinaweza kuwa special baraka kije "kimtoe" - anaweza kuki-abort ki-obama cha baadaye, ooooh!
   
 3. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  huyu mwanamke mwenzangu alikuwa wapi mpaka mimba ikafikisha miezi yote hiyo? watoto 4 kwa maisha ya sasa kwa upande wangu wanatosha sana, basi tena azae tu! hiyo ya kusema baraka/obama wa baadae ckubalianagi nayo kabisaaaa....inalemaza! obama bila matunzo/huduma muhimu?
   
 4. P

  Preacher JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  maji yakimwagika hayazoleki - issue ya abortion ni mawazo kutoka kuzimu - killing is killing - kiume tumboni kiko hai na abortion ni kutoa uhai wa hicho kiumbe - apart from kuchomwa moto kuna curses kibao zinafuatana na mtu anayemwaga damu ya mwenzake - so afadhali azaliwe - mama mkwe afurahi - na budget ibadilike - Mungu anaweza yote - na pia ukubali kuhusu huyu mtoto otherwise ataingiliwa na spirit ya rejection - ambayo ni mbaya sana
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  If one can manage 4 children, then he/she can obviously manage 5 children. Aache visingizio vya bajeti bana...Abbortion is such inhuman!
   
 6. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Sijakuelewa hapo una maana gani.
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  May 29, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nafikiri lingekuwa jambo la busara kama wangechukua muda mwingi katika kuangalia jinsi ya kuzuia issingie than now. Kimeshakija akiache tu.
   
 8. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,809
  Likes Received: 2,513
  Trophy Points: 280

  nashukuru Mkuu nitamhabarisha lakini bado yupo reluctant kweli kukubaliana na hali hiyo.
   
 9. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  shost mwanamama alikuwa anatumia sindano.
   
 10. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2009
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  what do you mean kulemaza?
  seriously ukisha-abort you will never know who you aborted, na afterall there is no significant difference kati ya 4 na 5 kids. au?
  abortion ni bad choice, ukishaacha ikaingia - inabidi uzae tu!
   
 11. T

  Tanga Line New Member

  #11
  May 29, 2009
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa MwanajamiiOne, walitakiwa kuwa makini isiingie! sasa wakubaliane na hali halisi , hata hivyo miezi iliyobaki si mingi ati!
   
 12. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  ndio kunafanya baadhi ya wanawake wasiwe makini na kinga zao, mtu kasema hataki watoto zaidi ya wa 4 then unatakiwa uwe makini au kama vipi wangefunga kizazi kabisa,mnasema kama amewahudumia 4 basi 5 hatamshindwa, mnajuaje mfuko wake unapumuaje?...yeye mume ndio anaejua! may be ndio kila kitu hapo nyumbani kuanzia watoto na mama,na bado familia zetu kuna kuwahudumia na baadhi ya ndugu pia na uwezo wake ulikuwa hapo kwa hao watoto wa 4 ili plans zake za kimaisha zisonge....eboooo, hakuna mahali nimeshauri akafanye abortion lakini nimeuliza alikuwa wapi mpaka ikafikia miezi yote hiyo?...kwa wamama wenzangu watanielewa....mnadhani kila kitu ndani lazima aambiwe na mr?......
   
 13. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45

  Ngoja tusubiri wamama wenzako wamshauri!!!
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mume kasema watoto 4 wanamtosha,nyie mnasema kama aliweza wa 4 na wa 5 hatoshindwa kumlea, nadhani mume anajua hali halisi ya mfuko wake na plans zake nyinginezo, familia zetu ndio kama hivyo tena kuna kuhudumia na baadhi ya ndugu,inalemaza ndio, mana mwanamama alitakiwa apangilie/afatilie uzazi wa mpango kwa umakini zaidi na kama angeona inakuwa ngumu basi wangekubaliana wafunge kizazi....hakuna mahali nimesema akafanye abortion bali nimeuliza alikuwa wapi cku zote mpaka mimba ikafikia miezi 4, wamama wenzangu watakuwa wamenielewa....ndivyo hivyo mnavyotuambiaga kwamba kwasasa tusimame kwanza na uzazi ama ndio kama alivyoambiwa huyu mwenzangu kwamba hao wanatosha, sasa unadhani mr karudi nyumbani katoka kwenye kinywaji kama wa kwangu vile na kashachangamka kidogo mnaingia kwenye ulimwengu mwingine kesho uje umwambia nipo preg atakuelewa na alishakuambia iwe hivi na vile?...eboooo mambo sio marahic kihivyo.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Naona leo Nyamayao umeamka vizuri ngoja nipate kwanza Konyagi.
   
 16. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  samahani hapo juu, nimeona nimejirudia rudia lakini ina maana moja tu, kushika mambo mawili kwa wakati mmoja, kazi na JF.
   
 17. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Sasa Nyamayao, unampa ushauri gani kama mwanamke mwenzio?
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  niletee na mie....swity malezi sio mchezo eti kwanza Mungu kawajaalia watoto wazuri wa 4, kwa nini hao hao mcwape matunzo/malezi/huduma nzuri ili wawe hiyo baraka/obama wa baadae? ..mtoa mada hebu niambie kama huyu mama ni mama wa nyumbani au mfanyakazi/mfanya biznes, ...huyu baba namwelewa kabisa msimamo wake!
   
 19. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  awe makini sana na matumizi yake ya uzazi wa mpango na awe makini pia na mabadiliko ya mwili wake....na namtakia kila la kheri katika safari yake hii na mwisho wa safari mungu amjaalie ajifungue salama.
   
 20. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  amen!
   
Loading...