Msaada wa ushauri na kisheria kuhusu Mafao ya kufukuzwa kazi kutoka PSSSF

Sheriff Hood

Member
May 3, 2018
82
124
Habari wakuu

Samahani naomba wenye idea na huu utaratibu wa PSSSF wanisaidie kunielewesha kama kweli hichi kitu kipo

Mimi niliwahi kuajiriwa Serikalini baada ya miaka miwili na nusu ya kudumu kwenye ajira nikafukuzwa kazi, baada ya kufukuzwa kazi nikaanza kufuatilia mafao yangu pspf (ambayo Sasa hivi ni PSSSF) nikawa nimekamilisha tafatibu zote kilichobaki ni kuingiziwa hiyo hela, lakini baadae wakaniambia hawatanilipa hiyo hela badala yake wataiingiza bodi ya mikopo kwa sababu nadaiwa. Sasa umepita zaidi ya mwaka mmoja toka waniambie hivyo na hiyo pesa bodi ya mikopo haijaingia mpaka leo.

Kutokana na scenario hiyo naanza kupatwa na wasiwasi juu ya ukweli wa uwepo wa huo utaratibu.

Naomba wadau mnaojua mnisaidie kujua Kama huo utaratibu au sheria hiyo ni kweli ipo.
 
Miaka miwili utakuwa imechanga miezi 24 ambayo ni cha mtoto sana.Sikushauri ufuatilie mafao kwani sijui kuna fao gani hapo labda la kukosa ajira lakini sijajua undani kwani inaonekana umefukuzuwa na sijui ni kwa sababu gani.

Nakushauri tafuta kazi kwingine huko mbeleni michango itakuja kuunganishwa na wewe kulipwa chako
 
Back
Top Bottom