Msaada wa ushauri, kuhusu udahiri wa vyuo vikuu kwa waliodisko

mzalendo namba moja

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
390
476
Mambo vip wanajukwaa?
Kwa wazoefu naomba Msaada, nina mdogo wangu alidahiliwa kwenda chuo kikuu cha Dodoma mwaka 2013 kwa points 3.0 yaani D na E, kwa wakat ule wanafunzi walidahiliwa kwa hizo point tofauti na hizi za sasa (4.0).

Mwaka 2015 akiwa mwaka wa pili aliugua na akaondoka chuo bila taarifa akakaa muda mrefu bila kufuafa taratibu za kuahirisha masomo, matokeo aliporudi chuoni, pamoja na evidence za ugonjwa alizokuwa nazo mkokoni lakini ikashindikana kurudishwa kwenye system (alidisco)

Kwa mwenye uzoefu msaada tafadhari, baada ya muda wa discontinuation, what follows ili arudi chuo?
 
Huyo mdogo wako ni muhuni!anaishi ki mbinu mbinu! Akaanze diploma tu! kama kweri aliumwa alitoa taarifa hata kwa uongozi wa wanafunzi hata kwa njia ya sim japo wamtee? Alishindwa hata kumwambia rafiki yake akachukue leave form amjazie then asambaze..au ndo yale yale ya haki bila wajibu?
 
Mwaka 2015 akiwa mwaka wa pili aliugua na akaondoka chuo bila taarifa akakaa muda mrefu bila kufuafa taratibu za kuahirisha masomo, matokeo aliporudi chuoni, pamoja na evidence za ugonjwa alizokuwa nazo mkokoni lakini ikashindikana kurudishwa kwenye system (alidisco)

Hivi aliondokaje chuoni bila kufuata taratibu? Nina hakika alijua kuna taratibu. Na sioni kama chuo kitamsikiliza mtu ambaye amevunja taratibu za chuo. Sasa kwa kuwa alijaribu kurudi chuo, ni sababu zipi zilifanya ashindwe kurudishwa kwenye system na walimpa ushauri gani?

Sasa bahati mbaya vigezo vya kudahiliwa vimebadilika, ushauri wangu ni ajaribu bahati yake kupitia njia ya Diploma au sivyo atazidi kupoteza muda.
 
Back
Top Bottom