Msaada wa ushauri kuhusu masomo ya baishara

Terace

Member
Jun 13, 2017
75
98
Habari zenu ndugu.

Ninaye kijana wangu ambaye anaelekea kuhitimu masomo ya sekondary na amekuwa akichukua masomo ya biashara kulingana na uwezo wake... japo kama mzazi nilipenda achukua masomo ya Sayansi ila yeye akapenda biashara kwa hiyo nikamsupport.

Sasa kwa mliopitia masomo ya biashara O-level, ninaomba ushauri wenu njia ipi ni sahihi kulingana na ulimwengu wa sasa;

1.
Kwanza nasikia kuna option ya kwenda Chuo ukasome diploma then degree au uendelee na mfumo wa F.6
Hapo ipi ni bora zaidi?

2.
Sitaki kijana aegemee kwenye masomo yanayomwandaa kuajiliwa...bali napenda aende upande unaomwandaa kujiajili either kwa kufanya biashara zake mwenyewe.

So hapo ni combination zipi achukue maana naskia huwa kuna commerce, economy, marketing e.t.c na kwa O-level nadhani ni general sana book keeping & Commerce.

Kiukweli mie sijui sana huko mgawanyiko ulivo ndo maana nikaomba ushauri kwenu. Uwezo wa kumsupport atapokuwa anamaliza naamini Mungu atanisaidia nimpe hata Capital ya above 40M

Sitaki asome kuka kuajiliwa...bali kuanzisha, kuendesha na kusimamia biashara zake ama za family ambazo zitakuwepo.

Asanteni
 
Back
Top Bottom