Msaada wa Ushauri juu ya Magumu anayopitia Mtanzania maeneo ya Tandika

maruudaniel

JF-Expert Member
Dec 19, 2020
342
500
Ninaandika hapa nikiwa huzuni juu Madhila anayopitia huyu Kijana
Niende moja kwa moja katika Mada husika.

Huyu kijana najuana naye tangu miaka ya 2000 katika maeneo ninayoishi ambayo ni pembeni ya Kota za shirika la nyumba lakini hizo Kota waliuziwa waliokuwa wafanyakazi wa shirika husika.

Katika hizi kota kuna maeneo ya wazi na sehemu kubwa la eneo hili la wazi watu walikuwa wakimwaga takataka.

Pembezoni kuna kituo cha kupandia daladala na kushukia.
Hapa Standi kukawa kuna mahali vijana wanakutania wao wanaita maskani yaani kuna vibenchi walivijenga kwa ajili ya kukaa kwa ujumla ni vijana wastarabu.

Wengi wa vijana ni kuzaliwa hapa kota na wengine wa maeneo ya pembezoni pa hili eneo la kota.

Katika wale vijana kuna kijana mmoja alijenga Banda la mbao akafungua Grosary na huyu kijana sio mzaliwa wa kota wala maeneo ya pembezoni mwa Tandika yaani mtu kutoka Mkoani.

Grosary ikawa ni maarufu sana na wateja wakawa wanatoka sehemu mbalimbali pale anapotajiwa jina la grosary na hii grosary ilifikia mahali ikawa ina kesha yaani usiku kucha biashara inafanyika ya vinywaji na vyakula.Jina hiyo Grosary ni (CHINI YA MUTI TAKE AWAY)

Grosary ikakuwa kukawa mpaka Choo cha temporary ambacho kipo mpaka leo ambapo eneo limekuwa na mabanda mengi ya biashara tofautitofauti kwa ujumla mzuko watu wanaojipatia kipato wameongezeka hapo.

Na hawa wafanyabiasha wote pamoja na wateja wao,Abiria, Wapita njia ,Bodaboda na watu wanaoshinda hapa Choo kinachotumika ndio hicho.
Huyu baada ya kuona kuna frusa katika eneo husika aliongeza mabanda mengine matatu ya mbao na kuyapangisha kwa watu wengine.

Huyu kijana anaishi vizuri na watu wa kota na pembezoni mwa kota.Lakini ni kijana aliyepitia mengi magumu ya uonevu japokuwa sio mtu mwepesi kukubali kwani mtu mwenyekupenda kujua mambo na kuyafanyia kazi kwani kwa aliyopitia ni mengi sana kisa tuu sio mzawa wa kuzaliwa watu wa kota hawana shida naye ila tatizo ni hawa wa pembezoni ambao aliwakaribisha mwenyewe kutokana biashara yake na wengi wao marafiki zake.

Niache aliyoyapitia huko zamani twende kwa sasa hivi ambayo yamenifanya niandike hili andiko fupi juu yenu watoa ushauri.

Wiki iliyopita alinifuata nyumbani na kunieleza haya-
Kati Banda moja lililokuwa halina Mpangaji kwa kipindi kisichopungua mwaka,siku moja ktk hilo banda alimpata mtu wa kumpangisha lakini katika hilo banda pana choo na hicho kilikuwa kimejaa na baada kupewa fedha kesho yake aliongea na vijana walioko ktk hilo eneo ili wakizibue ni Choo cha Matairi ya magari. Walielewana na vijana kuanza kazi kuchimba na yeye akiwa pembembeni amekaa na watu wengine huku wakipiga stori.

Gafla alitokea Mtu akiwa anaongea na simu ili apofika pale niliona vijana wanaanza lining'onezana kama vile kuna jambo sio zuri limetokea pale.
Baada kumaliza kuongea na simu aliuliza mnachimba Choo akajibiwa na kijana mmoja kati ya wale wachimbaji hapana tunatapisha.

Aliyetoa kazi aliposikia anasema alisimama na kusogeleana na huyu mara akauliza vibali akamjibu hatuna vibali akamwomba samahani kwani akamwambia amezoea ikitokea kimejaa huwa ana tapisha akaomba msamaha.

Mara baada ya muda kidogo alikuja Mwenyekiti wa Mtaa naye akauliza vibali akamwelezea na kuomba msamaha baada ya muda mwenyekiti na mwenzake waliondoka lakini cha ajabu yule mwingine alirudi na kumwambia huyu kijana Mwenyekiti amechukua hatua nyingine kwani amenituma niwalete hawa Polisi.

Kweli kijana aliitikia wito wa Polisi na kuongozana nao mpaka kituoni na kilichonisikitisha sana huyu kijana alikuwa amepata ajali wakati anavuka barabara maeneo Studio Kinondoni na kuvunjika Mkono na Mguu pia ulipata shida kwani alipekwa kituo na POPII bila hata huruma.

Baada ya kwenda Polisi aliwekwa chini ya ulinzi na alipoulizia dhama Polisi alimjibu tafuta wadhamini dhamana ikowazi baada ya muda walikuja marafiki akawaomba wachukue barua ya dhamana kwa mwenyekiti flani baada ya muda walirudi na barua dhamana.

Ndo akapata dhamana na kesho yake jumatatu alitakiwa kurudi kituoni na aliporudi kituoni alikutana na Bibi Afya akiwa ni mkali sana kila alichokuwa akiongea ni vitisho tuu. Baada bibi alitajia kiasi cha Faini anayotakiwa kulipa aliomba bila mafaniki ili fikia mpaka Wenyeviti 2 wa mitaa mingine waliingilia Kati baada ya kujua uonevu anaofanyiwa.

Baada muda bibi aliondoka kama saa nne asubuhi na kururdi saa kumi pia alifika hapo aliomba apunguziwe faini lakini hakupunguziwa.

Bibi akawa anamwambia wewe unakosea unakula mwenyewe kama ungekuwa unakula na mwenyekiti haya yote yasingekukuta kwani unamabanda mengi.
Lilipoisha swala bibi afya mwenyekiti bado una kesi ya kujenga mabanda na kuyapangisha kwa watu wengine kwa hiyo kesho uje na wapangaji wako na mikataba yao.

Kesho hakuweza kwenda alipangiwa kurudi hospital kesho kutwa yake akaitwa tena Polisi akawa ana hitaji mikataba pia mwenyekiti akamwambia ukitaka haya mambo yaishe aachiwe mabanda mawili.

Yeye anasema baada kuona mwenyekiti sio mzuri alishafikia kuyabomoa hayo mabanda ili akajenge mabanda ya kufuga kuku wa nyama kwani anaufhoefu nao ktk kuwafuga.

Hili swala haliwapendizi watu wengi maeneo hayo wakiwemo wenyeviti wenzake pamoja wale wastafu pia Diwani mmoja Mstafu ambaye anajua juu ya uonevu wa huyu mwenyekiti aliyeshiriki mpaka kula michango ya Rambirambi za mwanachi wake.

Humu Jf kuna watu wengi wanapita kama Mku wa Wilaya Godfrey Gondwe na kitengo cha malalamiko Temeke Wilayani mkachunguze hili swala kwa watu wanaokaa kota na wanaofanyabiasha pale Tandika Transfoma na maeneo mengine juu ya huyu mwenyekiti anaitwa Peter Siro
 
uttoh2002

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
6,144
2,000
Ninaandika hapa nikiwa huzuni juu Madhila anayopitia huyu Kijana
Niende moja kwa moja katika Mada husika.
Huyu kijana najuana naye tangu miaka ya 2000 katika maeneo ninayoishi ambayo ni pembeni ya Kota za shirika la nyumba lakini hizo Kota waliuziwa waliokuwa wafanyakazi wa shirika husika.
Katika hizi kota kuna maeneo ya wazi na sehemu kubwa la eneo hili la wazi watu walikuwa wakimwaga takataka.
Pembezoni kuna kituo cha kupandia daladala na kushukia.
Hapa Standi kukawa kuna mahali vijana wanakutania wao wanaita maskani yaani kuna vibenchi walivijenga kwa ajili ya kukaa kwa ujumla ni vijana wastarabu.
Wengi wa vijana ni kuzaliwa hapa kota na wengine wa maeneo ya pembezoni pa hili eneo la kota.
Katika wale vijana kuna kijana mmoja alijenga Banda la mbao akafungua Grosary na huyu kijana sio mzaliwa wa kota wala maeneo ya pembezoni mwa Tandika yaani mtu kutoka Mkoani.
Grosary ikawa ni maarufu sana na wateja wakawa wanatoka sehemu mbalimbali pale anapotajiwa jina la grosary na hii grosary ilifikia mahali ikawa ina kesha yaani usiku kucha biashara inafanyika ya vinywaji na vyakula.Jina hiyo Grosary ni (CHINI YA MUTI TAKE AWAY)
Grosary ikakuwa kukawa mpaka Choo cha temporary ambacho kipo mpaka leo ambapo eneo limekuwa na mabanda mengi ya biashara tofautitofauti kwa ujumla mzuko watu wanaojipatia kipato wameongezeka hapo.
Na hawa wafanyabiasha wote pamoja na wateja wao,Abiria, Wapita njia ,Bodaboda na watu wanaoshinda hapa Choo kinachotumika ndio hicho.
Huyu baada ya kuona kuna frusa katika eneo husika aliongeza mabanda mengine matatu ya mbao na kuyapangisha kwa watu wengine.
Huyu kijana anaishi vizuri na watu wa kota na pembezoni mwa kota.Lakini ni kijana aliyepitia mengi magumu ya uonevu japokuwa sio mtu mwepesi kukubali kwani mtu mwenyekupenda kujua mambo na kuyafanyia kazi kwani kwa aliyopitia ni mengi sana kisa tuu sio mzawa wa kuzaliwa watu wa kota hawana shida naye ila tatizo ni hawa wa pembezoni ambao aliwakaribisha mwenyewe kutokana biashara yake na wengi wao marafiki zake.
Niache aliyoyapitia huko zamani twende kwa sasa hivi ambayo yamenifanya niandike hili andiko fupi juu yenu watoa ushauri.
Wiki iliyopita alinifuata nyumbani na kunieleza haya-
Kati Banda moja lililokuwa halina Mpangaji kwa kipindi kisichopungua mwaka,siku moja ktk hilo banda alimpata mtu wa kumpangisha lakini katika hilo banda pana choo na hicho kilikuwa kimejaa na baada kupewa fedha kesho yake aliongea na vijana walioko ktk hilo eneo ili wakizibue ni Choo cha Matairi ya magari. Walielewana na vijana kuanza kazi kuchimba na yeye akiwa pembembeni amekaa na watu wengine huku wakipiga stori.
Gafla alitokea Mtu akiwa anaongea na simu ili apofika pale niliona vijana wanaanza lining'onezana kama vile kuna jambo sio zuri limetokea pale.
Baada kumaliza kuongea na simu aliuliza mnachimba Choo akajibiwa na kijana mmoja kati ya wale wachimbaji hapana tunatapisha.
Aliyetoa kazi aliposikia anasema alisimama na kusogeleana na huyu mara akauliza vibali akamjibu hatuna vibali akamwomba samahani kwani akamwambia amezoea ikitokea kimejaa huwa ana tapisha akaomba msamaha. Mara baada ya muda kidogo alikuja Mwenyekiti wa Mtaa naye akauliza vibali akamwelezea na kuomba msamaha baada ya muda mwenyekiti na mwenzake waliondoka lakini cha ajabu yule mwingine alirudi na kumwambia huyu kijana Mwenyekiti amechukua hatua nyingine kwani amenituma niwalete hawa Polisi. Kweli kijana aliitikia wito wa Polisi na kuongozana nao mpaka kituoni na kilichonisikitisha sana huyu kijana alikuwa amepata ajali wakati anavuka barabara maeneo Studio Kinondoni na kuvunjika Mkono na Mguu pia ulipata shida kwani alipekwa kituo na POPII bila hata huruma.
Baada ya kwenda Polisi aliwekwa chini ya ulinzi na alipoulizia dhama Polisi alimjibu tafuta wadhamini dhamana ikowazi baada ya muda walikuja marafiki akawaomba wachukue barua ya dhamana kwa mwenyekiti flani baada ya muda walirudi na barua dhamana.
Ndo akapata dhamana na kesho yake jumatatu alitakiwa kurudi kituoni na aliporudi kituoni alikutana na Bibi Afya akiwa ni mkali sana kila alichokuwa akiongea ni vitisho tuu. Baada bibi alitajia kiasi cha Faini anayotakiwa kulipa aliomba bila mafaniki ili fikia mpaka Wenyeviti 2 wa mitaa mingine waliingilia Kati baada ya kujua uonevu anaofanyiwa.
Baada muda bibi aliondoka kama saa nne asubuhi na kururdi saa kumi pia alifika hapo aliomba apunguziwe faini lakini hakupunguziwa.
Bibi akawa anamwambia wewe unakosea unakula mwenyewe kama ungekuwa unakula na mwenyekiti haya yote yasingekukuta kwani unamabanda mengi.
Lilipoisha swala bibi afya mwenyekiti bado una kesi ya kujenga mabanda na kuyapangisha kwa watu wengine kwa hiyo kesho uje na wapangaji wako na mikataba yao.
Kesho hakuweza kwenda alipangiwa kurudi hospital kesho kutwa yake akaitwa tena Polisi akawa ana hitaji mikataba pia mwenyekiti akamwambia ukitaka haya mambo yaishe aachiwe mabanda mawili.
Yeye anasema baada kuona mwenyekiti sio mzuri alishafikia kuyabomoa hayo mabanda ili akajenge mabanda ya kufuga kuku wa nyama kwani anaufhoefu nao ktk kuwafuga.
Hili swala haliwapendizi watu wengi maeneo hayo wakiwemo wenyeviti wenzake pamoja wale wastafu pia Diwani mmoja Mstafu ambaye anajua juu ya uonevu wa huyu mwenyekiti aliyeshiriki mpaka kula michango ya Rambirambi za mwanachi wake.
Humu Jf kuna watu wengi wanapita kama Mku wa Wilaya Godfrey Gondwe na kitengo cha malalamiko Temeke Wilayani mkachunguze hili swala kwa watu wanaokaa kota na wanaofanyabiasha pale Tandika Transfoma na maeneo mengine juu ya huyu mwenyekiti anaitwa Peter Siro

1. Kafanya biashara nzuri mda mrefu.
2. Eneo sio Raskina.
3. Kajenga vyoo bila ruhusa.
4. Kapangisha bila mikataba.

# anakula mwenyewe?

Ni sawa kabisa akiondolewa, ukipata fursa ya mteremko wekeza kwingine, hautakula milele, hata ukiondolewa hapo unakuwa na ka kuanzia!

Hana haja ya kulalamika maana ni mhalifu kama wahalifu wengine tu!
 
maruudaniel

JF-Expert Member
Dec 19, 2020
342
500
1. Kafanya biashara nzuri mda mrefu.
2. Eneo sio Raskina.
3. Kajenga vyoo bila ruhusa.
4. Kapangisha bila mikataba.

# anakula mwenyewe?

Ni sawa kabisa akiondolewa, ukipata fursa ya mteremko wekeza kwingine, hautakula milele, hata ukiondolewa hapo unakuwa na ka kuanzia!

Hana haja ya kulalamika maana ni mhalifu kama wahalifu wengine tu!
Mku kipindi anajenga bado alikuwa Dogo hayo yote hakuyajua.
Yeye yuko tayari kuyabomoa ili kizuizi ni kwa Mwenyekiti na huyu migogoro sio kwa huyu tuu ipo mingi juu yake.
Ndo maana watu wa kota na wanaozunguka hili eneo wako pamoja na huyu Kijana aliyeyajenga
 
mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,842
2,000
Huyo kijana hajitambui. Kavamia eneo la wazi anapiga pesa na bado anataka kuwavimbia Viongozi. Muuulize hilo eneo alilojenga mabanda alilinunua wapi ama kodi anamlipa nani?? Kwa kifupi mwambie awe mpole vinginevyo hana chake hapo, kuleta hap jamvin mnamaanisha DC akayavunje mabanda yooote yakiwemo yakwake??
 
Kuyatoa haya mabanda hajakataa tatizo ni mwenyekiti hataki yeye ayatoe.
Mwenyekiti amempa sharti kijana akitaka yaishe wayagawe hayo mabanda mawilimawili yaani Mwenyekiti mawili na yy abaki na mawili.
Na yeye ameshaona ili kuwa na amani ni kuyabomoa na kwenda kujenda mabanda ya kufugia wa nyama .
Kwani hataki malumbano juu ya hilo ili anze ukurasa mpya wa ujasiriamali.
Asante
 
uttoh2002

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
6,144
2,000
Mku kipindi anajenga bado alikuwa Dogo hayo yote hakuyajua.
Yeye yuko tayari kuyabomoa ili kizuizi ni kwa Mwenyekiti na huyu migogoro sio kwa huyu tuu ipo mingi juu yake.
Ndo maana watu wa kota na wanaozunguka hili eneo wako pamoja na huyu Kijana aliyeyajenga

Mshauri kama Hataki kusumbuka asisikilize yeyote afanye utaratibu, aende kwa Mkurugenzi apate utaratibu na Aufuate!

Mambo ni rahisi sana Tanzania ukiyajulia!
 
Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
589
1,000
Kwani akifuata maelekezo ya mwenyekiti kuna ubaya gani? Ubishi mwingine hausadii! Sasa huyo kijana anataka aikimbie fursa kwa sababu ya ubishi wake!

Kwanza anatakiwa kujua, sehemu yoyote yenye ridhiki huwa ina vurugu za hapa na pale, na ukipenda kula, kubali kuliwa.

Namalizia kwa samahani, ukiona unatakiwa utoe rushwa ili mambo yako yasonge, wewe toa rushwa tu!
 
Mku Dogo amepitia mengi magumu ktk hilo eneo kwa sasa anaona akafuge kuku wa nyama kwani anaujulia zaidi na anaamini ndiko maendeleo yake yaliko.
Kwani anaona kuendelea kuwepo pale ni hatari kwake sio mahali salama tena kwa mtu anayeona mbele kwa hiyo afadhali amwachie mwenyekiti hilo eneo.
Mpaka anakuja kwangu alikuwa na mambo mawili yaani kuondoka Nchi na kuelekea Mozambiq ,Swaziland au Malawi Kwa kutafuta maisha kwani azijua hizi Nchi kiundani sana ila kinachorudisha nyuma ni Familia yake na shule kwa watoto wake.
Ndo mwisho akaja swala ufugaji wa kuku kwani aliwahi kufuga .
 
May 11, 2020
91
150
Mkuu usikaze shingo mwambie uyo dogo wayamalize kwa mazungimzo wakubaliane dogo anamakosa na sioni akitoboa akiendeleza ubishi na usikute ata tin no ya TRA hana akiendeleza ubishi ataumia zaidi hii dunia unaweza kuwa upande wa haki na ukaumia vilevile
 
maruudaniel

JF-Expert Member
Dec 19, 2020
342
500
Mkuu usikaze shingo mwambie uyo dogo wayamalize kwa mazungimzo wakubaliane dogo anamakosa na sioni akitoboa akiendeleza ubishi na usikute ata tin no ya TRA hana akiendeleza ubishi ataumia zaidi hii dunia unaweza kuwa upande wa haki na ukaumia vilevile
Kijana sio mmbishi ndo namtafutia ushauri huku ili maisha yaendelee
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom