Msaada wa ushauri juu ya hiki kiwanja

Smart AJ

JF-Expert Member
Mar 21, 2022
5,533
5,736
Zamani sana kabla mzee hajafa, alipewa shamba na rafiki yake ili alime ila sikujua kama rafiki yake hakujulisha familia yake, ni kiwanja kipo manispaa ni cha nusu eka hivi..

Imepita miaka zaidi ya 30 sasa na wote(mzee na rafikiye )wamefariki amebaki mama tu ambaye yeye bado analima.

Watu huwa wanaamini kuwa kiwanja hichi ni mali yetu ila sivyo. Mara nyingi tumekuwa tunawaza wapi tutawapata hawa ndugu au familia ya huyu mzee ila hatujui tunaanzia wapi.

Sijui itakuaje coz mama yangu ni wale watu wa imani sana huwa haamimi kwenye kula mali ya mtu.

Msaada wenu wakuu tukifanyaje hiki kiwanja ili kiwarudie wenye mali yao.
 
Back
Top Bottom